Feb 15, 2018
Mbinu Za Kujitengenezea Maisha Mengine Nje Ya Ajira.
Inawezekana ukawa umeajiriwa na miaka nenda na miaka rudi
hujawahi kufanya kitu cha msingi, au inawezekana bado umeajiriwa na unasubiri
mafao tu. Ninachotaka kukwambia ni kwamba ni lazima uwe na akili nyingine ya
ziada itakayokufanya uweze kutengeneza maisha mengine zaidi ya ajira uliyonayo.
Na hayo maisha mengine ili uweze kuyaishi hayo unaweza kujikita
katika kufanya biashara au kujiingiza katika suala zima la kufanya
ujasiliamali. Haiwezekani ukaendelea kuishi kwenye ajira tu peke yake miaka
nenda rudi, kipo kipindi uwe na uhakika utakwama kama usipoingia kwenye
ujasiriamali.
Na ili uweze kufanya hivyo unatakiwa kufanya
mambo yafutayo;-
1. Dhibiti matumizi yako ya pesa.
Moja kati ya matatizo
ambayo yanayowakumba watu waliojariwa ni kwamba wanashindwa kudhibiti matumizi
yao ya fedha, Wengi wao wanashindwa kufanya hivyo kwa sababu wana imani hata
pesa ikisha mwisho wa mwezi wana uhakika wakupa pesa nyingine.
Kwa minajili hiyo ndio maana watu hao wanashindwa kuanzisha
miradi ya msingi na hivyo kupelekea watu wao kuwa na matumizi mengi ya pesa. Hivyo
ili uweze kuanzisha mradi wako ukiwa umejiliwa hakikisha unadhibiti kiwango
chako cha matumizi ya pesa katika kila mshahara unaopata.
2. Usitegemee kipato kimoja.
Jambo la pili ni kwamba ukiwa bado umeajiliwa hakikisha ya kwamba hutegemei
kipato kimoja cha kukupatia pesa, bali kuwa na vyanzo vingi vya kuweza
kujingizia kipato wewe mwenyewe. Ili kufanya hivyo ni vyema ukajikita katika masuala
ya ubunifu na ujasiliamali kwa ujumla.
Kubaki na kipato kimoja ni hali ya hatari sana kwako. Unatakiwa
una vipato vingi ambavyo vitakuwezesha wewe kuweza kuishi maisha nje ya ajira. Ikiwa
hautafanya hivyo itabaki kwako hadithi ya kutokufanikiwa. Ni muhimu sana
kutengeneza vyanzo vingi vya pesa ili kuishi maisha nje ya ajira.
3. Tumia mshahara kuanzisha mradi.
Katika hili ni kwamba ili uweze kujitengezee maisha mengine nje
ya ajira, kwa hicho kiwango kidogo au kikubwa cha mshahara unachokipata
hakikisha ya kwamba unatenga asilimia fulani kwa jinsi utavyoona wewe ili
kuanzisha mradi wako binfsi itakayokufanya ufurahie maisha unayoishi.
Mpaka kufikia hapo hatuna na ziada tukututane tena siku nyingine
hapa DIRA YA MAFANIKIO kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
Ndimi afisa mipango Benson Chonya,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.