Jun 4, 2015
Mambo 7 Yanayofanya Maisha Yako Kuwa Magumu.
Maisha tuliyonayo huwa sio
magumu sana kama wengi tunavyofikiri. Ugumu wa maisha mara nyingi huwa
tunautengeneza wenyewe bila kujua. Huwa ni watu wa kufanya maisha yetu magumu
kutokana na fikra ama maneno ambayo tunayasema na kujiambia mara kwa mara juu
ya maisha yetu. Kwa wengi huwa tuna kawaida ya kujiambia maisha yetu ni magumu,
hatujiwezi na wala hatuna haki ya kupata mfanikio makubwa.
Lakini sio maneno peke yake
tu hata matendo na mienendo na tuliyonayo kila siku, pia huweza kufanya maisha
yetu kuwa magumu kwa namna moja au nyingine. Kwa kadri tunavyozidi kujiambia
maneno hasi na kuwa na matendo ama mienendo mibovu, ndivyo tunavyojikuta
tukizidi kuharibu masha yetu. Hivyo tumekuwa tuna mchango mkubwa wa kubomoa
maisha yetu sisi wenyewe bila kuelewa ukweli wa hilo.
Ni wakati umefika wa kuweza
kutambua mambo yanaharibu maisha yetu. Hatuna haja tena ya kulaumu na kupiga
kelele kila wakati kuwa ‘Maisha yetu ni
magumu sana’. Inatakiwa tuijue kweli itakayoweza kutuweka huru na kutoka
kwenye ugumu wa maisha. Tuache tabia ya kung’ang’ania mambo yanayotuharibia
maisha yetu, vinginevyo hatutafika mbali. Mambo tunayotakiwa kuyajua na
yanayofanya maisha yetu kuwa magumu ni kama haya:-
1.
Kupoteza pesa zisizo za lazima.
Hiki ni kitu ambacho
kimekuwa kikiwatoa wengi katika mstari wa mafanikio. Wengi wetu mara kwa mara
tumekuwa tukijiingiza katika matumizi yasiyo ya lazima ambayo yanatupotezea
pesa nyingi. Pesa hizo zinapopotea huwa siyo rahisi sana kugundua kwa sababu ya
udogo wake na kutokujali.
Tuchukulie mara kwa mara
umekuwa ukiacha pesa ndogo ndogo zile unazoziita ‘chenji’ dukani. Na hiyo haitoshi umekuwa ukitoa ofa bila kujiuliza
kwa rafiki zako. Pesa za namna hii ikifika muda kama miezi miwili ama
mitatu zinakuwa nyingi, kiasi kwamba
kama ungezitunza ungeweza kuanzisha kitu cha maana cha kukusaidia.
Kwa matumizi kama haya kwa
kadri tunavyozidi kuyaongeza, ndivyo tutakavyojikuta tunazidi kupoteza pesa
nyingi na kufanya maisha yetu kuwa magumu siku hadi siku. Wengi wetu tunao
lalamika ‘Oooh maisha yangu ni magumu’
ukija kuchunguza kidogo, hao ndio huwa
wa kwanza kwa matumizi mabaya ya pesa zao pale wanapozipata.
Nini
Kifanyike Sasa?
Kwanza, tujaribu kujikagua
mwenyewe binafsi na kuangalia jinsi tunavyotumia pesa zetu. Kama matumizi ni ya
hovyo, ni muhimu kujirekebisha na kuwa na matumizi mazuri ya pesa yatakayoweza
kutuongoza kwenye maisha bora. Pili, tuwe tuna bajeti maalum inayotuongoza na
sio kutumia pesa tu kwa sababu eti zipo mfukoni.
2.
Kutumia muda mwingi kuwa na watu hasi.
Muda mwingi tumekuwa
tukiishi maisha na watu hasi ambao wamekuwa wakiturudisha nyuma sana. Tumekuwa
tukiishi na watu hawa wanaotukatisha tamaa na kutuonyesha kila aina ya ubaya
katika maisha yetu. Kwa kuendelea kuishi na watu hawa, ndivyo ambavyo tumekuwa
tukijikuta tukifanya maisha yetu kuwa magumu zaidi.
Watu hawa wamekuwa wana
nguvu kubwa hasi, ambayo imekuwa ikituvuta na kujikuta tukitenda mambo mengi kwa
mkabala hasi na kuharibu maisha yetu. Ni watu ambao tumekuwa tunao, tukiishi
nao kila siku. Inawezekana wakawa ni ndugu, jamaa au hata marafiki zetu wa karibu
sana ambao tumekuwa tukishirikiana nao kwa mambo mengi.
Kipi
kifanyike sasa?
Kikubwa ni kuanza kuanza
kuishi na watu chanya ambao kwa vyovyote vile watatusaidia kutufikisha kwenye
ndoto zetu bila kigugumizi. Chagua watu marafiki ambao utafurahia kuwa nao na
wataweza kukusaidia kukufikisha kwenye ndoto. Kuwa chanya ni siri mojawapo
nzuri ya kukufikisha kwenye mafanikio.
3.
Kupoteza muda sana.
Hili ni moja ya jambo muhimu
ambalo limekuwa likitupoteza na kutuvuruga bila kujua. Hii yote huwa inakuja
ama kutokea kutokana na wengi wetu kujikuta ni watu wa kupoteza muda bila
sababu ya msingi. Kitu usichojua kwa kadri unavyozidi kupoteza muda wako,
ndivyo unavyozidi kupoteza maisha yako na kuzidi kufanya maisha yako kuwa
magumu zaidi.
Kwanini hii huwa iko hivyo?
Hii ni kwa sababu muda wako unahusika sana katika shughuli nzima ya uzalishaji.
Hivyo kwa vyovyote vile kwa kadiri unavyopoteza muda wako, ndivyo ambavyo
unapoteza masaa ya uzalishaji. Ukijaribu kuchunguza utagundua ukweli huu kuwa
wengi wetu ni watu wa kupoteza muda bila sababu ya msingi.
Ni
nini cha kufanya sasa?
Ili utuweze kuondokana na
hali hiyo ni vyema tukajifunza kutunza muda wetu na kwenda na ratiba. Ni lazima
tujue muda fulani tutakuwa wapi na tunafanya nini? Siyo suala la kuamka tu na
kujiendea. Kwa kufanya hivyo, tutakuwa tunauokoa muda mwingi ambao utatusaidia,
badala ya kuupoteza na kuwa majuto kwetu.
4.
Kuahirisha mambo.
Kwa sehemu wengi wetu
tumekuwa kama ni watu wenye ugonjwa
fulani kuhusu hili. Tumekuwa ni watu ambao kila mara tunaahirisha kazi ambazo
tulitakiwa kuzifanya mara moja, pengine hata bila sababu. Hata tu pale
inapotokea kazi nyepesi nayo pia huweza kuahirisha na kusogezwa mbele zaidi.
Kwa maisha hayo ya
kuahirisha kwa uhakika na ukweli uliowazi hatuwezi kufanikisha lolote katika
maisha yetu. Hili ni mmoja ya jambo dogo lakini ambalo limekuwa likifanya maisha
yetu kuwa magumu. Jaribu kufikiri kazi zote ambazo umewahi kuziahirisha jinsi
ambavyo kwa baadae zinavyoweza kuwa ngumu kutokana na uharaka unaokuwa nao.
Kitu
cha kufanya ili usiahirishe mambo yako tena.
Jambo lolote lile tunalotakiwa
kulifanya kwa namna yoyote ile, hatutakiwi kuwa wepesi wa kulisogeza mbele. Kwa
kulisogeza mbele, tutambue kuwa, tutakuwa tunaleta ugumu bila ya sisi wenyewe
bila kujua. Tufanye mambo yetu leo leo na tuachane na habari ya kesho hiyo
itakuwa inatupotezea muda mwingi.
5.
Kuwa msemaji na mlalamikaji sana.
Hakuna mtu atakayeweza
kusimama na kupigania maisha yetu kama wengi tunavyofikiri. Maisha yetu ni
maisha yetu hata iweje yatabaki kuwa yetu na sisi ndiyo waamuzi wa mwisho wa
kutaka maisha yetu yaweje. Wengi wetu kwa kutokujua hujikuta ni watu wakulaumu
tu kuwa maisha yetu yamechangiwa kwa kiasi kikubwa ama kuharibiwa na wengine.
Kwa kulalamika kwetu hivyo
haiwezi kusaidia hata tufanye nini, zaidi kutufanya tuzidi kurudi nyuma bila sisi
wenyewe kujitambua. Tangu tuanze kulalamika tujiulize tumebadili maisha yetu
kwa kiasi gani? Nina uhakika hakuna kitu ambacho tumebadilisha zaidi tu ya
kuweza kuumia na kuteseka na kulalamika kwetu huko.
Tufanyaje
sasa?
Kitu cha kufanya hapa ni
kuchukua hatua chanya yenye nia halisi ya kubadilissha maisha yetu. Tuache
kufanyia kazi kwenye midomo na ni lazima tuchukue hatua kwa vitendo tena kwa
haraka vitakavyoweza kutubadilisha na hali zetu kwa sasa na baadae.
6.
Kutaka Kufanya mambo mengi kwa pamoja.
Ni kweli wengi wetu huwa
tuna nia ya kutaka kufanya mabadiliko makubwa katika maisha yetu. Mabadiliko
ambayo huwa tunataka ni kuona kuwa maisha yetu tuliyonayo yanabadiklka ikiwezekana
kwa haraka tena sana. Kutokana na wengi wetu kuwa na kiu hiyo hapo ndipo huwa
tunajikuta tukifanya mambo mengi kwa wakati mmoja.
Kwa kufanya mambo hayo kwa
wakati mmoja ndivyo ambavyo wengi huweza kujikuta ufanisi ukipungua na
kushindwa kufanikisha hata malengo yetu. Hili ndilo kosa ambalo pia hupelekea
wengi kuanza kuishi maisha magumu kutokana na mambo mengi kutoleta matunda
yaliyotarajiwa.
Kipi
kifanyike?
Pamoja na kuwa tuna nia
kubwa ya kufanikiwa kitu kimojawapo cha muhimu cha kuanza kufanya ni kuhakikisha kuwa hatufanyi mambo mengi kwa
wakati mmoja. Ni bora tukafanya mambo kwa wakati ili kuleta manufaa zaidi.
7.
Kutaka kuepuka makosa sana.
Kama tutakuwa tunaishi
maisha ya kuogoapa sana kutokukosea na kutaka tuwe tu sahiihi muda wote, basi
ni wazi kuwa hatutaweza kufika mbali sana katika mafanikio yetu. Kutokana na
hili la wengi kupelekea kuepuka makosa hujikuta ndivyo ambavyo maisha yatu kuwa
magumu zaidi.
Kwa kifupi hayo ndiyo mambo
yanaweza kufanya maisha yetu yakawa magumu kwa namna moja ama nyingine. Kitu cha
kufanya tuchukue hatua zaidi ili kuweza kubadilisha maisha yetu.
Tunakutakia kila la kheri
katika safari yako ya mafanikio, endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa elimu
na maarifa bora yatakayoboresha maisha yako.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA
MAISHA YAKO YAIMARIKE,
IMANI
NGWANGWALU,
0713
048035,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Asante nimepata somo
ReplyDeleteGood
ReplyDeleteSee
Asante
ReplyDeleteAyseeee
ReplyDeleteHaya masomo yapewe nafasi mashureni aise
ReplyDelete