google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jan 15, 2016

Acha Kusahau Kufanya Mambo Haya Kwenye Maisha Yako.

No comments :
Habari rafiki na mpenzi msomaji wa DIRA YA MAFANIKIO ni imani yetu kubwa ya kwamba umzima wa afya na unaendelea na harakati za kuboresha maisha yako. Kama ilivyo kawaida yetu tunakukaribisha tena ili kwa pamoja tuweze kushirikiana kujifunza juu ya mafanikio.
Katika siku ya leo tutaangalia mambo ya msingi ambayo hutakiwi kusahau kuyafanya kwenye maisha yako. Kabla hatujaendelea naomba nikukumbushe kwamba, mara nyingi wengi wetu kuna wakati hujikuta tuna nia kubwa ya kutoa au kusaidia wengine waliokaribu nasi.
Hata kama sio kila siku ila kutoa msaada kwa wengine hasa pale nafasi inapopatikana ni kitu ambacho wengi wanakipenda. Hebu jaribu kufikiria zile nyakati za sikuu kubwa kama mwaka mpya ama ‘valentine day’, bila shaka wengi wetu hutaka kutoa zawadi kwa wale waliokaribu zetu.
Je, unafikiri ni kwa nini hali hii huwa iko hivyo, kwa karibu kila mtu kujisikia mhemuko wa kutaka kutoa zawadi fulani kwa aliyekaribu naye? Ni kati gani ambacho huwa kinasababisha? Kwa kawaida huwa zipo sababu nyingi, lakini  mojawapo ya sababu hizo ni kama zifuatazo;-
§  Tunakuwa tunatoa kwanza ili kuonyesha kwamba tunajali…
§  Tunatoa ili tuweze kuona furaha ya kukubaliwa…
§  Pia tunatoa kwa kutegemea faida ya baadae kwa wale tunawaotolea mambo hayo…
Kama nilivyosema sababu zake huwa zipo nyingi kulingana kati ya mtu mmoja na mwingine na ni jambo zuri kuonyesha kwa wale waliokaribu nao.

MAONO NI LAZIMA KWENYE SAFARI YA MAFANIKIO.
Pamoja na uzuri wote huo ambao huwa tunauonyesha sana kwa wale waliokaribu yetu kuwa tunawajali na tunawapenda. Lakini kuna mambo ambayo huwa tunasahau sana kujipa sisi wenyewe kwanza. Haya ndiyo mambo yaliyotakiwa tuwe tunajipa sisi wenyewe kwanza ili kufanikiwa.
Unaweza ukasema ‘Aaah sasa Imani unataka kuleta ubinafsi’ sio hivyo haya ni mambo ya lazima kujipa na kujitolea wewe kila wakati bila kuchoka kwani ndio msingi wa maisha yako ya mafanikio. Naamini una nia ya kufanikiwa, kama ni hivyo, acha kusahau kufanya mambo haya kwenye maisha yako.
Jambo la kwanza.
Kitu ambacho hutakiwa kusahau kujipa kwenye maisha yako kila siku ni Hamasa. Unatakiwa kujifunza kujipa au kujitolea hamasa kila siku bila kuchoka. Kwa kadri unavyozidi kuwa na hamasa kubwa ndivyo ule ‘moto’ wa mafanikio unakuwa unawaka ndani yako.
Wengi wanakuwa wanashindwa kufanikiwa kwa sababu ya kukosa ile hamasa kubwa ambayo inaweza ikawafanya wakasonga mbele. Hamasa inakuwa ni kama mafuta ya kukusaidia kuweza kuendelea na safari ya mafanikio bila kuchoka siku zote. Hili ni jambo la kwanza ambalo hupaswi kulisahau kujipa.
Jambo la pili.
Mbali na hamasa jambo lingine ambalo unatakiwa kujipa na kutolisahau katika maisha yako ni maono (Vision). Ni lazima siku zote uwe na maono makubwa juu ya maisha yako. Ni lazima ujue baada ya miaka fulani utatakuwa wapi. Bila maono maisha yako yanapotea bure.
Kwa hiyo kila wakati jipe tathmini kwa kuangalia maisha yako. Hiki ni kitu kizuri sana kitakachoweza kukusaidia kujiweka katika nafsi nzuri ya kufanikiwa. Watu wote ambao mara nyingi ni wabeba maono maisha yao huwa ni ya mafanikio makubwa sana.
Jambo la tatu.
Najua tayari umeshajifunza juu ya umuhimu wa kujipa hamasa na maono. Jambo la tatu ambalo unatakiwa kujipa kila siku ni ukarimu. Siku zote katika maisha yako jaribu kuwa mtu wa ukarimu. Acha kuishi maisha kama dumbwana fulani hivi ambalo halina maana, hiyo haitakusadia sana.
Ishi maisha ya kuwajali na kuwakarimu wengine. Kwa kadri utakavyozidi kufanya hivyo utajikuta unazidi kujenga uaminifu mkubwa na mafanikio yatakuwa upande wako daima.
Kila siku kumbuka kujikumbusha mambo hayo kwani ni mambo ambayo unatakiwa kujipa kila siku bila kuchoka.
Nikutakie siku njema na mafanikio mema yawe kwako daima.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Simu; 0713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.