google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Nov 17, 2015

Vifungo Ambavyo Jamii Inakufunga.

No comments :
 Leo napenda kusema msemo mmoja, "JARIBU KUJIFUNZA KUTOKA NJE YA PULIZO". Pulizo ni kama vile puto au Bubble kwa kingereza. Ukilitazama pulizo, hewa ikiwa ndani yake haitoki tena nje. Hivyo kuwa ndani ya pulizo au puto kunamaanisha kuwa kifungoni. Hivyo kauli hiyo inamaanisha jifunze kutoka kifungoni katika kutafuta dhumuni lako la maisha. 

Kifungoni ni wapi? Je ni kama mahabusu? Hapana, nikisema kifungo ninakuwa ninamaanisha pale ambapo panakunyima uhuru au unapokosa nafasi ya kuwa wewe kama wewe. Pulizo ni kama vile kifungo cha kidunia ambacho kila mmoja wetu anakuwa ndani yake. Mfano kifungo hicho kinaweza kuwa ni:-

·         Wasiwasi wa wakati ujao,
·         Dhana unayoifahamu juu ya mafanikio katika maisha,
·         Kulazimisha kupendwa na kila mtu,
·         Kulazimisha kumfurahisha kila mtu,
·         Kulazimisha kuwa mkamilifu,
·         Maneno ya watu,
·         au Imani ambayo hauna uhuru au uhakika nayo.

TOKA KWENYE KIFUNGO HIKI.
Kila mmoja wetu katika jamii ambayo amekulia, kuna mengi ambayo jamii imemfundisha na kumuambia kuwa ndio jamii inavyopaswa. Mfano 

·         Jinsi ya kuishi,
·         Jinsi ya kuvaa,
·         Jinsi ya kula,
·         Kipi cha kula na kipi cha kutupa, 
·         Dini/Imani gani ipo sahihi,
·         Wewe ni nani na kwanini upo hapa,
·         Miziki, Television na vyombo vingine vya habari visemavyo,
·         Matangazo yakikuambia kipi cha kununua au cha muhimu na bora kuliko vingine,
·         Maana ya mafanikio ni nini,
·         Kazi gani ni ya maana kuliko nyingine na mengi ambayo jamii imeona ni mazuri kwao basi nao hupenda yawe mazuri kwako.

Ni jambo zuri sana kwani ni jamii inajitahidi kukujali na kukufundisha kile ambacho inaona ni haki. Lakini je wewe utajuaje kama jamii ipo sawa? Je kama ni kutokana na kutofahamu kwao ndio kunapelekea mitazamo hiyo? Ni vyema kuisikiliza jamii inasema nini lakini pia nawe ni vyema kuutafuta ukweli wewe kama wewe, na ndio maana upo hapa ulimwenguni. Kama hakuna umuhimu wa wewe kuwepo ni kwanini upo? Lazima kuna sababu ya msingi. 

Jamii inatuweka kwenye pulizo, hivyo ni vyema kutoka nje ya pulizo ili kuufahamu ukweli. Ukweli hauwezi kuufahamu kwa kuambiwa tu bali nawe unapaswa uuthibitishe. Je aliyeanzisha ukweli huo aliambiwa na nani? Kwanini na wewe usiutafute? Kwa kuacha kulazimisha mambo unaweza ukajikuta unajifunza mengi sana kuhusiana na maisha kwa ujumla, na ikakusaidia kutafuta dhumuni lako la maisha.
 

Kama unatafuta dhumuni lako la maisha kwa kutegemea jamii ikuchagulie dhumuni la kuishi utamaliza maisha yako hujaishi maisha yako bali unaishi maisha ya wenzako. Ili kuijua safari yako ina malengo gani toka nje ya pulizo na chunguza ndani mwako unapenda nini na jamii inakuambia nini. Mfano kuna anayependa kuwa daktari lakini wazazi wanamwambia awe fulani. Sio kwamba wazazi wamekosea, nao wapo sahihi. Jitahidi uwaelewe kwani kuna wakati mtu hukuchagulia maamuzi kwa kukulinda na kwa kutumia akili aliyonayo yeye, hivyo nawe unapaswa kutambua ni kwanini mtu anakupa mtazamo fulani na kisha amua mtazamo wako kiusahihi na bila kubishana au kumdharau mtu. Heshimu kila mtu na tambua mchango wa kila mtu katika maisha yako.


Makala hii imeandikwa wa Apolinary Protas wa JITAMBUE SASA BLOG. Kama una maoni au ushauri wasiliana na Waandishi wa makala hii kwa email jitambuesasa@gmail.com

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.