Apr 6, 2016
Hii Ndiyo Thamani Ya Kufanya Kazi Yako Binafsi.
Kuna tofauti kubwa sana iliyopo kati ya kazi na ajira, unashaanga
ndio ukweli huo. Tulio wengi huwa tunazama kazi kama ajira kumbe ni vitu viwili tofauti. Katika makala
yetu ya leo tutakwenda kuangalia tofauti hizo kati ya ajira na kazi na thamani
ya kufanya kazi.
Tukianza na kujua maana ya Kazi, kazi ni shughuli yeyote ile iliyo
halali au isiyo halali ambayo huifanya mtu kutokana na ujuzi, kipaji na ubunifu
ili kupata mapato na faida, ila katika mafanikio tunazungumzia kazi halali tu.
Ila ajira ni kile kitendo cha kuuza muda, ujuzi, ubunifu na
kumtumikia mwingine, hii hutokea kwa
kuwa wewe hujaamua kufanya kazi yako mwenyewe ila umeamua kuajiriwa. Daima
tukumbuke ya kuwa kazi ndiyo ambayo inayoanza kabla ya ajira . Ajira ni mizizi
ya utumwa nasema hivi nikiwa nina maana ya kwamba kwa kuwa hii karne ya ishiri
na moja baadala ya kuwaita watumwa basi wanaitwa wafanyakazi.
Leo ingekuwa ni tarehe moja
mwezi wa nne ungesema Afisa anaongopa,
sijaongopa na huo ndio ukweli usiopingika. Kuna baadhi ya watu wao huamini ya
kwamba bila ajira wao hawawezi kuishi jambo hilo halina ukweli wowote ndani
yake. Sina maana ya kusema eti kuajiliwa ni kubaya hapana, ila ukweli ni kwamba
ni lazima ufikiri nje boksi, yaani kitu kingine zaidi ya kutengemea kulipwa
mshahara ila ifike mahali na wewe ulipe watu mshahara.
JITUME ILI KUFANIKIWA ZAIDI. |
Watu wengi waliojiriwa wanasema Mwenyezi Mungu ibariki kazi ya mikono
yangu, Je Hiyo ni Kazi ya mikono yako au ya mwajiri wako? Ukitaka kusema hayo azisha kitu chako harafu
ndo useme Mwenyezi Mungu bariki kazi ya mikono yangu na baraka zitakuja kweli.
Daima tukumbuke ya kuwa binadamu ameumbwa ili kufanya kazi, ukisema wewe ni
mcha Mungu ni lazima ufanye kazi. Ukisoma katika Vitabu vya Dini vinatufundisha
ya kuwa, siku zote baraka za kiuchumi zinapatikana kwa kufanya kazi kwa bidii.
Pia mpango wa Mungu kwa watu wake baada ya kuwaumba ilikuwa ni watu
hao kwenda kuitawala nchi na sio watu. Kutawala nchi kwa maana ya kuwa
kuitazama nchi na vitu vilivyoko ndani yake katika uzalishaji kama vile ardhi
katika kufanya kazi za usalishaji. Kuna kitabu fulani cha kimafanikio
kiliandikwa ya kwamba hapa duniani kuna kila aina ya kitu ambacho mwanadamu
akikitumia vizuri atakuwa tajiri.
Ila tatizo kubwa ni kwamba watu waliopo ndani yake hawavitumii vitu
hivyo. Swali la kujiuliza je vitu hivyo Mungu alivyotupa vinakupa manufaa gani
au ndio unazidi kulaumu kwa kusema maisha ni magumu? Ukweli ni kwamba tumia
vitu vilivyopo ili kupata mafanikio makubwa.
Thamani ya kufanya kazi ni kama
ifuatavyo;
1. Thamani za kufanya kazi huja kwa kujituma na kufanya kazi kwa bidiii
siku zote.
Muda muafaka wa wewe kuamuamua kufanya kazi ndo huu sasa. Unapenda
kuendelea kuita boss maisha yako yote au kuitwa boss, usinipe jibu. Ila kumbuka
kukata kiu yako ya mafanikio kunywa kinywaji kinachoitwa bosi, ukifanya hivyo
kweli utakuwa bosi.
2. Ubunifu.
Thamani ya kufanya kazi huja kwa mtu kuwa mbunifu, Ubunifu huanza
kwenye wazo jipya, wazo ndio chanzo kikubwa na ndio siri kubwa iliyojificha
kupata utajiri. Siku zote ukumbuke ya kuwa ni mtu mwenye mawazo mapya yenye kuleta mafanikio
makubwa mbele yako. Kuwa mbunifu ili umiliki kazi yako ili uweze na wewe kuitwa
bosi maana inawezekana kabisa.
Makala imeandikwa na Afisa mipango
na maendeleo; Benson Chonya
Simu; 0757-909942
E-mail; bensonchonya23@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.