Apr 21, 2016
Kinachokufanya Ushindwe Kufikia Uhuru Wa Kipesa Ni Hiki Hapa.
Kwa
wale wafatiliaji wazuri wa mtandao wetu wa dira ya mafanikio wiki iliyopita
katika moja ya makala zetu tuliongelea juu ya tabia ambazo zinaweza zikakuzuia
kupata kiasi kikubwa cha pesa unachokitaka. Kwa kifupi tuliona mchango wa tabia
hizo katika suala zima la kukuzuia wewe kupata pesa za kutosha. Leo katika
makala haya, mbali na tabia hizo tutaangalia kitu kingine cha kipekee ambacho
kina uwezo mkubwa wa kukufaya ushindwe kufikia uhuru wa kipesa hata kama
unaweka juhudi nyingi.
Najua
unatamani kujua kitu hiki ambacho kinauwezo mkubwa wa kukuzuia kupata pesa.
kama ni hivyo tulia, acha kuwa na haraka sana. Kumbuka kwamba wakati mwingine, linapokuja
suala la kukosa kile kiwango cha pesa unachotaka tatizo huwa sio ukosefu wa
pesa, au pesa hazitoshi kama wengi wanavyodai. Tatizo huwa ni moja tu ambalo ni
hofu ya kupata kiwango kile cha pesa unachokihitaji. Usishangae sana hili ndilo
tatizo lingine linalokufanya ushindwe kufikia uhuru wa kipesa unaoutaka.
Naona
hunielewi elewi vizuri na unajiuliza maswali mengi kwamba ninaongea kitu gani?
Sikiliza. Kama wewe ni mfanyakazi na unataka kujiajiri na umeona biashara fulani
ndiyo itakayokulipa moja kati ya maswali ambayo utakuwa unawauliza sana watu ambao
walishafanya hiyo bishara hiyo ni kwamba hivi nitapata kiasi hiki cha pesa kwa
mwezi. Unajua ni kiasi gani ambacho utakuwa unauliza? Ni ile pesa ambayo unataka
kujua kama itakuwa sawa na ile unayolipwa. Utakuwa una lengo la kulinganisha
mshahara na pesa unayoipata kwenye biashara.
Sasa
unapoona hivyo ujue hiyo ni moja ya hofu ambayo inaweza kukuzuia kufikia kwenye
uhuru wa kipesa. Unapochagua kufanya biashara fanya biashara kwa nguvu zote.
Kwa kadri unavyozidi kuendelea inakuwa inazidi kukua polepole na kuwa biashara
kubwa kuliko ulivyokuwa ukifikiri. Lakini suala la kujijengea hofu sana
litakuzuia kufikia uhuru wa kipesa usipokuwa makini. Waangalie wote wenye hofu
kama waapesa. Naamini unajua hwana pesa nalo. Hofu haina msaada wowote katika
maisha yako, hata wewe kama hofu yako ni kubwa huwezi kufikia uhuru wa kipesa
na huwezi pata pesa pia.
Ili
uweze kufikia uhuru wa kipesa jenga imani kubwa ndani yako ya kuamini kwamba
hilo kwanza linawezekana. Ukishajijengea hiyo imani anza kuchukua hatua. Kwa
kuchukua hatua, hiyo itakusaidia sana kufikia mafanikio makubwa. Acha kuruhusu
imani ya ‘siwezi’ ikakutawala ndani
yako. Kama utakuwa na imani hii basi itakuwa ni chanzo kimojawapo kikubwa cha
kukufanya ushindwe kufikia uhuru wa kifedha.
Kwa
leo tuishie hapa ila kumbuka endelea kujifunza kupitia mtandao huu wa DIRA YA
MAFANIKIO kila wakati.
Ni
wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu;- 0713 04 80 35,
Blog;-
dirayamafanikio.blogspot.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.