Apr 22, 2016
Kitu Kinachokufanya Ushindwe Kutimiza Malengo Yako.
Bila shaka umewahi kuwaona
watu ambao katika maisha yao siku zote ni watu wasio na pesa na ni watu ambao
wanaishi maisha ya kutotimiza malengo
yao siku hadi siku. Umeshawi kujiuliza watu hawa tatizo kubwa walilonalo nini
linaowafanya waishi maisha hayo siku zote?Ni kitu ambacho pengine kimekuwa
kikikushangaza.
Ukija kuangalia ama
ukichunguza kwa makini utagundua kuwa watu hawa, ambao inaweza ikawa ni wewe pia, wamekuwa wakiishi
maisha ya kutokutimiza malengo yao sio
kwa sababu hawana pesa ama muda wa kutimiza malengo yao. Kitu kikubwa
kinachowafanya wasitimize malengo ni kukosa nguvu ya uzingativu katika malengo
yao.
Hiki ndicho kitu muhimu
wamekiwa wakikikosa katika maisha yao na kimewafanya waishi maisha magumu
yasiyo na pesa. Kwa kawaida, unapokosa nguvu ya uzingativu na kushindwa kutilia
mkazo kwa kujikumbushia malengo yako mara kwa mara kinachotokea kwako ni lazima
ushindwe kufikia malengo yako.
Watu wengi wenye mafanikio makubwa
wanajua ukweli huu na wanaufanyia kazi kila siku kwa kujikumbushia malengo yao
mpaka yanatimia. Kama unafikiri natania nenda kamuulize Thomas Edson na ugunduzi
wake wa glopu/balbu alikosea mara 9999 bila kuchoka hadi akaja kugundua kitu
ambacho kina manufaa kwetu mpaka leo.
Kama Thomas Edson angekata
tamaa na kushindwa kuweka nguvu za kutosha za uzingativu kwenye malengo yake
aliyojiwekea basi pengine leo hii dunia yote ingekuwa inalala giza. Kunapokuwa
na nguvu ya uzingativu na kuielekeza akili yako yote kwa kile unachokifanya
huwa kuna matokeo makubwa ya kimafanikio.
Nakumbuka nikiwa darasa la
sita, katika somo la sayansi mwalimu wangu mmoja alikuwa akitufundisha namna ya
kutumia kioo ambacho kilikuwa kipo katika mfumo wa lensi kuweza kuchoma vitu
kama karatasi. Alikuwa akichukua kioo kile na kukielekeza kwenye karatasi
ambapo baada ya muda kwa kukiweka kioo sehemu moja kilikuwa kinakusanya mwanga
wa jua na kuweza kuchoma karatasi.
Mwalimu Yule aliweza
kutufafanulia kuwa mwanga wa jua una
nguvu sana lakini kama umesambaa hauwezi kuleta madhara yoyote, mpaka ukusanywe
pamoja na kitu kama lensi ya kioo ndio unaweza ukaleta madhara na kuchoma vitu
kama karatasi. Kwa kupitia mfano huo hivyo ndivyo tulivyo katika maisha yetu.
Mara nyingi binadamu
tunazonguvu nyingi sana na kubwa ambazo tunauwezo wa kuzitumia na kutuletea
mabadiliko makubwa katika maisha yetu kama tutaziwekea nguvu ya uzingativu.
Yale mambo ambayo umekuwa ukishindwa mara kwa mara ukijakuangalia unashindwa
sio kwa sababu huwezi ila ni kwa sababu unakosa nguvu hii muhimu kwako.
Kama unataka kufanikisha
malengo yako na kuona ndoto zako zikiwa zinatimia ni jukumu lako wewe kuweza
kujifunza kutumia nguvu hii vizuri ya uzingativu ili ikuletee matokea chanya
unayohitaji. Hata kama umeshindwa mara ngapi kwa kile unachokifanya acha
kupoteza mwelekeo kwa kukosa nguvu hii muhimu kwako na mafanikio yako.
Kitu pekee kinachowafanya
watu wengi wawe waoga, wawe watu wa kuahirisha mambo, wakose uvumilivu na
nidhamu binafsi ni kutokana na kukosa
nguvu hii ambayo wakiwa nayo itawasaidia kufikia malengo yao waliyojiwekea.
Unapokosa uzingativu wa kulenga kile unachokitaka kiwe katika maisha yako,
inakuwa ni ngumu sana kufikia malengo yako.
Ili uweze kutimiza malengo
yako unahitaji kuwa na nguvu ya uzingativu hasa kwenye malengo yako iliyojiwekea
kila wakati. Kuwa na mafanikio siyo suala la bahati kama wengi wanavyofikiri ni
kitu cha kupanga na kuamua kisha kuweka nguvu zako zote huko, uwe na uhakika
malengo yako hapo yatatimia.
Nakutakia mafanikio mema,
endelea kutemblea DIRA YA MAFANIKIO kila siku kujifunza na kuhamasika, mpaka
maisha yako yaimarike.
IMANI
NGWANGWALU,
0713
048 035/dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.