Apr 11, 2016
Mambo Mawili (2) Yenye Kuleta Mafanikio Kwa Haraka.
Kuna wakati ni lazima utambue baadhi ya mambo ya msingi
yatakayokufanya uweze kufanikiwa katika maisha yako. Mafanikio
ninayoyazungumzia ni yale ya kila shughuli ambayo unaifanya ili mradi tu iwe
halali katika jamii na inatambuliwa kisheria. Leo nataka kutumbua majibu ya
kimafanikio ya kibiashara, kazi, masomo na mambo mengine. usishangae wala
hujakosea kusoma yapo majipu ya kimafanikio ambayo yanatukwamisha tusiweze
kufanikiwa. Tafadhari shusha pumzi kisha twende sawa katika makala hii
utakwenda kuelewa vizuri.
Haya ndiyo mambo ya kuyafanya ili uweze
kufanikiwa;
Kujitambua.
Hili ni tatizo kubwa kwa watu wengi sana. Kujitambua ndio suala
ambalo watu wengi hatunalo. Tafiti zinaonesha ya kuwa mtu mzima ana miaka kumi
nane, pia watu wengi wanaamini kuwa katika kipindi cha umri huo
mtu ndio anaanza kujitambua, ila ukifuatilia kwa watu walio wengi katika
umri huo utagundua hakuna ukweli, kama ni kweli watu waliofika umri wa miaka 18
kweli wanajitambua kwa maana ya kuanza kupata mafanikio. Mbona ndio kuna wimbi
kubwa la watu wanaolalamika kuhusu maisha?
Lakini kiuhalisia umri huo kwa hapa nchini ni umri wa kuwa na meno
thelethini na mbili na kuruhusiwa kwenda kununua pombe ambazo mwanzo alikuwa
haruhusiwi kununua, unacheka huo ndio ukweli usiopingika. Maana yangu ni kwamba watu wengi tunachelewa sana
hasa katika swala la kujitambua. Wengi wetu tupo katika kipindi cha kuamini ya
kwamba ipo siku ndio tutaanza kufanya kitu fulani. Bado tunaishi katika misingi
ya kuwa tegemezi na kuamini kuwa vijana
ni taifa la kesho kitu ambacho sio kweli.
WEKA VIPAUMBELE VYA MAISHA YAKO. |
Shutuka ewe mwanajamii hasa kijana huku ukujiuliza wewe ni nani? na
unataka kufanya nini ili uweze kufanikiwa na sio kusubiri muda fulani ndio
uanze kuyasaka mafanikio. Tuendele na ufafanuzi ukiwa ni miongoni mwa vijana
wanaosema ya kuwa huu ni muda wa kula
ujana basi endelea ili uje umeze uzee vizuri. Wimbi kubwa la watu ambao
wanalalamika kuhusu maisha ni vijana, lakini vijana hao hao pindi wapatapo pesa
hawana nidhamu sahihi juu ya matumizi ya pesa hizo. Mfano leo hii mtu anakuwa
na pesa nyingi sana baada ya siku chache utamsikia anaita pesa ni shetani kwa
sababu zimeisha zote bila kufanya kitu cha maana. Nataka kukwambia ewe msomaji
wa makala hii mwenye tabia kama hizi, ya kuwa pesa sio shetani ila matumizi
yako ndio shetani.
Tambua ya kuwa maisha mazuri ya kesho huandaliwa na leo yako
ukiendelea na tabia ya kusema bado upo upo, basi utaendelea kuwepo kama friji
ambalo limetulia tu ndani. Ewe kijana mwenzangu kwa kuwa unahitji mafanikio ya
kweli basi ni muda sahihi wa kujua wewe ni nani na ni nini? cha kufanya ili
uweze kufanikiwa katika maisha yako. Pia katika safari ya mafanikio kumbuka ya
kuwa njia ya mkato ndiyo njia ndefu na yenye maisha mafupi hivyo jitahidi
kutafuta mafanikio yako kwa njia iliyo halali.
Weka vipaumbele.
Katika maisha ni kwamba ni lazima ujue ni vitu gani unataka
kuvifanya. Weka mikakati ambayo ni kwamba haitaishia njiani, kila jambo ambalo
unalolifanya hakikisha ya kwamba hukatishi safari hiyo, kuna usemi unasema zege hailali, basi hakikisha na wewe
unafanya mambo ambayo unapata matokea chanya ya jambo hilo. Kama alivyo askari
akiwa vitani basi na wewe uwe hivyo hivyo kwamba hakikisha unapambana na
changamoto zote ambazo zitajitokeza mbele yako.
Makala imeandikwa; Benson Chonya
Simu: 0757-909942
E-mail; bensonchonya23@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.