Apr 5, 2016
Mambo Manne (4) Ya Kuyatazama Sana Ili Kupata Na Kukuza Mtaji Wako.
Kuna wakati mwingine watu wengi huwa tunakosea
sana kwa kutazama na kufikiri ya kuwa mtaji ni pesa peke yake kwa ajili ya kufanzisha biashara. Kumbe kuna
vitu vingine ambavyo ni vya kuvitazama
ili huo mtaji uweze kukua na kufanya kile ambacho unakihitaji ili kutimiza
malengo yako. Leo katika makala hii nitakwenda kukueleza kinaga ubaga ili uweze
kufahamu ya kwamba kabla ya kuwa na mtaji ni lazima ujue misingi hiyo
itakayokusaidia kutimiza ndoto zako. Kwani endapo utakosa misingi hiyo hata
ukiwa na mtaji kiasi gani biashara utayoishazisha haitaishi miaka mingi.
Yafuatayo
ndiyo mambo ambayo mtu anayahitaji ili kupata
na kukuza mtaji;
1. Akili
Kisaikolojia binadamu wote wana akili ila
tatizo linakuja katika uwezo wa
kufikiri, kuamua na kutenda. Kimsingi ni kwamba watu wengi wanashindwa kutimiza
malengo yao kwa sababu ni watu wavivu wa kufikiri. Watu wengi wanashindwa
kugeuza maarifa waliyo nayo yawe bidhaa au huduma.
Kwa mfano mtu anayefanya biashara ya kupika chakula na kupata kipato, mtu huyu hawezi kufikiri
kufungua darasa kwa ajili ya kuwafundisha wanafunzi waweze kupika na yeye aweze kupata kipato zaidi. Tatizo
linakuja ulichonacho hutaki kukifanya kikuongezee kipato zaidi. Ukitaka
kufanikiwa zaidi ya hapo ulipo jambo la msingi ni fikiri chanya kwa kubadili
mtazamo ulionao.
UBUNIFU NI SILAHA YA MAFANIKIO. |
2. Nguvu.
Hapa sizungumizii nguvu ya kuwa na misuli ya
kupigana bali nazungumzia ili uweze kuwa kile unachokitaka lazima utumie nguvu
ulizonazo katika kufanya kazi kwa bidii na maarifa ili kuzalisha huduma na
bidhaa bora. Watu wengi tuna hulka ya
kuwa wavivu katika kufanya kazi na hii inatupelekea tunazidi kuwa ni watu
wakutumia kuliko kuzalisha. Wakati
mwingine tunalalamika ya kuwa maisha ni magumu huku tukisahau kuwa sisi ndio
wagumu katika katika kufanya kazi. Jambo la msingi ni kwamba badili mtazamo kwa
kutumia nguvu ulizonazo katika kuzalisha kuliko kutumia tu.
3. Kipaji
Katika maisha ya mafanikio kuna vitu viwili.
Kitu cha ambacho unatakiwa kufahamu ya kwamba ili uweze kufanikiwa ni lazima
uwe na machaguo mawili yaani plan A na plan B ili uweze
kufanikiwa. Mpango wa kwanza ni jinsi gani unaweza kutumia ujuzi ulionao ili
kufanikiwa na mpango wa pili ni jinsi gani ya kutumia kipaji ulichonacho ili
uweze kutimiza ndoto zako. Watu wengi hawaviishi vipaji vyao kwa sababu ya
sababu mbalimbali.
Kwa mfano jiulize wakati ukiwa mdogo ulikuwa
unapendelea kufanya nini zaidi? kama
umefikiliria kwa umakini utakuwa umepata
jibu na je kitu hicho bado unacho au
unafanyia kazi katika kukufanya ndoto ziwe kweli? Ukifikiria kwa umakini utagundua ni kwamba
watu wengi hatuna vipaji hivyo tena . Lakini tafiti nyingi zinaonesha ya kwamba
watu ambao wanatuzunguka ndio ambao wanasabibisha kufa kwa vipaji hivyo.
Nasema
hivo nikiwa na maana ya kwamba watu wanaotuzunguka wakituona tunafanya jambo fulani
, watakukemea na kukuambia achaa! hicho kitu unachokifanya kitakufanya ushindwe
kusoma na sababu nyingine nyingi ambazo hazina ukweli ndani yake.
Ila laiti kila mmoja angetumia vizuri kipaji
chake alichopewa na mwenyezi Mungu katika maisha yake walalamikaji tungepungua
ambao huwa tunasema maisha ni magumu na tungepata mafanikio zaidi. Kumbuka kutumia
kipaji ulichonacho ili kuongeza wigo mpana wa kupata kiapto ili kutimiza ndoto
zako.
4. Ubunifu.
Kila kitu kinahitaji ubunifu ili kuona kina
tija katika maisha yetu. Kwa kila jambo ambalo ulifanya linahitaji ubunifu.
Ubunifu ambao nina uzungumzia siku ya leo ni ule wa kutengeneza kitu kipya au
huduma au kuongezea thamani katika kitu ambacho tayari unakifanya.
Ili kuongeza thamani na kupata kile unachokihitaji jaribu kuwa
ndio mtu wa kwanza muundaji wa kitu hicho. Katika jambo hili unaweza kutumia
kipaji ulichonacho kuwa mbunifu. Ubunifu ni lazima uwe wa peke yako. Ili kuweza
kutimiza ndoto zako za kimafanikio jaribu kuyatazama mambo kwa jicho la tatu.
Wewe ambaye umesomea kuwa mhasibu
ili kuweza kufanikiwa zaidi ni lazima ufikiri zaidi ya kuwa mhasibu kwa
kuwa mbunifu ili uweze kutimiza malengo yako ambayo umejiwekea. Kuishi kwa
kutengemea mshahara au hicho unachokifanya kukuingizia pesa hakikotoshi fikiri
nje ya boksi kwa kuwa mbunifu zaidi ama hakika utafanikiwa.
Asante sana kwa kusoma makala hii mpaka
kufikia hapo sina la ziada tukutane tena katika makala ijayo ili kuweza
kujifunza zaidi.
Mwandishi;
Benson chonya
Simu;
0757-909942
Barua
pepe; bensonchonya23@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.