Apr 19, 2016
Matumizi Mabaya Ya Fedha Ni Adui Wa Mafanikio Yako.
Kuna wakati mwingine Katika maisha yetu ya kila siku tunasema pesa
ndio kila kitu. Ni kweli lakini kuwa na pesa bila wazo mahususi katika matumizi
ni sawa na kuzima moto kwa chafya. Unashangaa huo ndio ukweli watu wengi
tunapata pesa lakini hatujui tuitumie vipi pesa hiyo ili iweze kujizalisha. Zipo
sababu nyingi ambazo zinasababisha matumizi mabaya ya fedha.
Pesa hii ina majina mengi hii ni kutokana na mahali husika wapo
wanaita pesa ni sababuni ya roho, mtonyo, mapene, ankara na majina mengine mengi. Leo katika makala haya nitakwenda kukuelezea
juu ya matumizi mabaya ya pesa yanayofanya kila siku tuwe katika hali ya
umaskini.
Yafuatayo ndiyo matumizi mabaya ya
pesa.
Kutokuwa na mpangilio wa matumizi
ya pesa.
Moja ya changamoto kubwa inayowakumba wengi wetu ni kwamba hatuna
mapangalio sahihi juu ya matumizi ya fedha. Tupo baadhi yetu ambao hutamani
kila kitu ambacho tunakiona mbele yetu na kukinunua hata kama ulikuwa hauna mpango
wa kununua kitu hicho. Tupo baadhi yetu tukiwa tunatembea tukiona hiki na kile
ni lazima tununue hiyo siyo nidhamu ya fedha.
Pia kuna baadhi ya watu wakipata mishara utajua tu kwa kuona
matumizi yao wanayoyafanya. Kufanya hivyo ni Kujirudisha nyuma mwenyewe jambo
la msingi la kufanya juu ya matumizi sahihi ni kuwa na mpangilio mzuri wa pesa
nunua kitu ambacho umepanga kununua. Pia Hakikisha ya kwamba kila pesa
unayoipata na kuitumia Unaiandika katika daftari lako la kumbumbuka hii
itakusaidia kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha maana utakuwa unajua kila
faida na hasara ya jambo unalolifanya.
Kuwa makini na mpangilio wa pesa. |
Kukopa pesa hovyo.
Hili ndilo kosa kubwa ambalo linawaelemea watu wengi sana. Nadhani
utakuwa shaidi mzuri ni jinsi gani!
madeni yanavyowatesa au yanavyokutesa. Wapo baadhi ya watu wanakopa pesa
katika taasisi za kifedha lakini hawana elimu ya kutosha juu ya mikopo hiyo
hasa katika kuangalia mkopo utakuwa na faida au hasara. Wengi Hawaelewi
kuhusiana na mkopo hasa swala zima la kulipa riba.
Utashangaa kwa mfano mtu anakopa shilingi laki tisa na anatakiwa
kurudisha milioni moja ndani ya mwezi mmoja. Kwa kuwa pesa hiyo haukujua juu ya
riba hiyo pindi unaposhindwa kuirejesha utajikutana unaunguna na wale wanaosema
pesa ni shetani.
Maana yangu ni kwamba kukopa sio kubaya ila jaribu kupata elimu ya
kutosha juu ya mikopo na jaribu kufanya uchunguzi wa mkopo hasa swala la riba.
Jaribu kufanya mlinganisho kutoka taasisi moja na nyingine hii itakusaidia
kujua ni mkopo gani unakufaa. Tukiachana maswala ya mikopo katika mataasisi ya
kifedha wapo baadhi ya watu ni wakopaji wazuri kwa watu wengine kama vile nguo,
viatu na pesa. Usiwe na madeni ambayo yamezidi kwa kiwango kikubwa kwani kuwa
na madeni kwa kiasi kikubwa yanakurudisha nyuma kwa namna moja au nyingine.
Mwandishi: Afisa mipango na Maendeleo Benson
Chonya
Mawasiliano
simu; 0757- 90 99 42
Barua pepe; bensonchonya23@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.