Apr 12, 2016
Unaweza Kubadilisha Maisha Yako Kabisa Ukiamua Na Kufanya Hivi.
Moja kati ya kosa kubwa ambalo watu wengi wanafanya
katika maisha yao ni kule kuamini kwamba hawawezi kufanya mambo fulani na
badala yake uwezo huo wamewaachia watu wengine. Kwa mfano utakuta mtu
anakwambia hawezi kufanikiwa kwa viwango vya hali juu sana kwa sababu hana
uwezo huo lakini ingawa kiuhalisia sio kweli.
Chochote unachokitaka katika maisha yako, unaweza
kukipata ikiwa utauamini uwezo mkubwa ulio ndani yako. Una uwezo mkubwa sana ndani
yako usioelezeka ambao ukiutumia unaweza kukupa chochote ukitakacho kama tu
utachukua hatua. Lakini kama utaendelea kuamini huwezi kufanikiwa ni wazi kabisa hutaweza kufanikiwa. Utapata kile unachokiamini akilini mwako.
Jiulize kama kuna watu wengine wanaweza kufanikiwa kwa
nini wewe ushindwe kufanikiwa? Wanaofanikiwa kumbuka ni watu wa kawaida wenye
macho, miguu, nywele, akili na kila kitu sawa na wewe. Kitu ambacho pengine
wamekuzidi ni maamuzi na kiu ya kufanikiwa
kwao. Kama ni hivyo fanya uamuzi sahihi wa kufanikiwa.
Kama fulani aliweza kufanikiwa na wewe unaweza pia kufanikiwa ukiamua.
Kama Oscar Pistorius mwanariadha mlemavu aliweza
kufanya hivyo na kufanikiwa wewe pia unaweza kufanikiwa kwa hali yoyote
uliyonayo.
Kama Ben Carson mwandishi wa vitabu aliweza
kufanikiwa akitokea kwenye mazingira magumu ya kimaskini na wewe unaweza.
TUMIA AKILI YAKO VIZURI KUKUFANIKISHA. |
Kama Aliko Dangote aliweza kufanikiwa na kufikia
viwango vya juu vya utajiri duniani pia na wewe unaweza kufanikiwa.
Kama Nick Vujicic akiwa kwenye hali yake ya ulemavu
ameweza kufanikiwa na wewe una uwezo huo wa kufanikiwa.
Una kila kitu na uwezo mkubwa wa kufanikisha kila
unachokihitaji katika maisha yako.
Kuwa makini sana…usijishushe wala kujiangalia hasi
hasi yaani kujiangalia hufai au kwamba huwezi kufanikiwa. Ipo nafasi kubwa ya
kufanikiwa kwako tena. Hakuna kinachoshindikana ikiwa utaamua kuifungua akili
yako na kubadilika.
Kama kuna sehemu umeanguka amua kuamka tena na wala usikate tamaa. Rekebisha makosa yako,
jifunze kwa wengine na songa mbele. Ishi kwa ndoto zako kila siku na jione kama
msindi kwa kile unachokiendea.
Tambua mabadiliko yote unayoyataka kwenye maisha
yanaanza na akili yako kwanza. Kile unachokifikiri na kukibeba sana kwenye
akili yako mara kwa mara ndicho kinachotoa hatma ya maisha yako.
Kama ulikuwa unafikiri umechelewa kufanya
mabadiliko katika maisha yako, haujachelewa. Anza kufanya mabadiliko kwenye
akili yako kwanza kila siku baada ya muda utabadili kila kitu kwenye maisha
yako na hakuna kitu cha kukushinda.
Kumbuka kama wengine wanaweza na wewe unaweza
kufanikiwa pia.
Unao uwezo wa kuwa mtu wa tofauti.
Unao uwezo wa kufanikiwa.
Unao uwezo mkubwa wa kuwa nyota wa maisha yako.
Hakika unaweza, ikiwa utachukua hatua na kukubali
kujifunza.
Ansante kwa kusoma makala haya na endelea kujifunza
kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila wakati.
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Email;- dirayamafanikio@gmail.com
Blog;- dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.