Apr 15, 2016
Mambo Yanayokufanya Ukose Furaha Kwenye Maisha Yako.
Kila kitu
tunachokifanya katika maisha yetu kinalenga kupata furaha ya kweli. Tunatafuta
pesa, tunajenga nyumba nzuri, tunanunua gari nzuri, tunaoa au kuolewa na
wachumba wazuri kwa sababu ya furaha.
Furaha
ya kweli inapokosekana katika maisha, kwa wengi kunakuwa hakuna maana ya kuishi
tena ndio maana umeshawahi kusikia kuna wengine wamejiua lakini hiyo yote baada
ya kuona furaha halisi wanaikosa kwenye maisha yao.
Lakini kwa
mujibu wa tafiti nyingi zinaonyesha kwamba, pamoja na binadamu kuisaka furaha
hiyo usiku na mchana lakini kuna wakati furaha hiyo huwa inakosekana kutokana
na mambo mabalimbali yanajitokeza.
Ili kuijenga
furaha hiyo tena na kwa muda mrefu kitu cha kufanya kwanza ni lazima ujue mambo
hayo yanayoweza kukupotezea furaha.
Kwa kusoma
makala haya utajua mambo ya msingi yanayokupotezea furaha kwenye maisha yako.
1. Watu wanaokurudisha nyuma.
Mara nyingi
ni vigumu sana kukubali ukweli wa mambo hasa kama kuna watu wanaokuumiza. Watu hawa
watakuumiza moyo na kuiona dunia yote chungu kwako.
Nini
cha kufanya?
Kitu kimojawapo
cha kufanya ili usiendelee kuumia acha kuwaweka watu hao kichwani mwako. Kama kuna
sehemu walikurudisha nyuma basi hiyo imeisha, wafute kichwani mwako na anza
maisha mapya.
Kumbuka,
maisha yako unaweza ukayafanya upya na kuwa bora tena.
Toa mawazo hasi akilini mwako, uishi maisha ya furaha. |
2. Mawazo hasi.
Kuwa na
mawazo hasi kila wakati hukufanya ujione hufai na isitoshe unaweza kukonda
kabisa.
Unapokuwa
na mawazo hasi yanakufanya ujione wakati mwingine unashindwa kwenye karibu
kwenye kila jambo.
Nini
cha kufanya?
Toa
mawazo yako hasi yaliyo kwenye kichwa chako. Muda wote jione mshindi na beba
vitu vya kukusaidia ikiwemo pamoja na kujisomea vitu chanya.
3. Kujishusha sana.
Kujikosoa,
kujishusha na kujitilia shaka, ni mambo ambayo yanaweza kukuumiza sana na
kukukosesha furaha kama utaendelea na kujikosoa huko.
Kitu gani
kinachotokea? Kwa mfano unapojikosoa unakuwa tena huwezi kufanya kitu chochote
cha kukusaidia. Kwa sababu kila unachotaka kufanya umeshajiwekea mipaka tayari.
Nini
cha kufanya?
Tambua
maeneo bora kwako na yafanyie kazi. Pia jipongeze kwa mafanikio madogo
uliyowahi kupata na weka malengo tena ya kukufanikisha.
4. Kuchukulia mambo kwa ujumla.
Kama kuna
mtu amekufanyia kitu kibaya au hajakufanyia kama ulivyotaka, usichukulie kama
mtu huyo ndivyo alivyo na ukaanza kuumia.
Chochote
kinachokutokea kwenye maisha yako kiwe kizuri au kibaya usikichukulie kwa ujumla
wake. Fikiri mara mbili kwanza kabla hujajitolea hukumu, vinginevyo utaumia sana.
Nini
cha kufanya?
Jifunze
kuona mambo yanavyokwenda kwa uhalisia wake. Na usichukulie kwa ujumla sana.
Hiyo itakusaidia kujenga furaha ya muda mrefu.
5.
Kujiwekea kumbukumbu mbaya kwenye akili yako.
Chanzo kingine
cha kukufanya uzidi kukosa furaha ni kuendelea kujiwekea kumbukumbu mbaya zilizotokea
hasa kwa kipindi cha nyuma.
Kama kuna
jambo baya lilikutokea kipindi cha nyuma liache kama lilivyo, lakini kwa kuling’ang’ania
litakusababishia kuendelea kukosa furaha kwenye maisha yako.
Huna haja
ya kuweka kumbukumbu sana na mambo yanayokuumiza akili mwako kwa muda mrefu.
Nini
cha kufanya?
Kuanzia
sasa jaza ubongo wako mambo mapya ili kutoa mambo ya zamani ambayo yameujaza
ubongo wako kwa muda mrefu na yanakuumiza. Kwa kujaza ubongo wako utajenga
furaha upya ya maisha yako.
Endelea kujifunza kupitia DIRA YAMAFANIKIO kila siku. Ni wako rafiki Imani Ngwangwalu. Mawasiliano +255 713 048 035.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.