Apr 4, 2016
Hizi Ndizo Njia Mbili (2) Zenye Kukuhakikishia Mafanikio.
Kuna wakati unahitaji mambo mengi ya
kuyafahamu ili uweze kufanikiwa kimaisha.
Hivyo kwa kila jambo ambalo unataka likuletee mafanikio ni lazima ujue
ni kwa namna gani litakuletea mafanikio. Watu wengi tunaingia kufanya mambo ya
kimafanikio kwa njia za kawaida sana. Kitu hicho ambacho kinatufanya kila siku
tubaki mahali pamoja kila siku na kushindwa kusonga mbele kimafanikio. Lakini katika
makala haya nitakuibia siri mbili ambazo ukizifuata zitakufanya uweze
kufanikiwa.
Zifuatavyo
ni njia mbili zenye kukuletea mafanikio;
Kwa asilimia kubwa watu wengi hatupendi
kujifunza vitu vipya hasa kwa staili ya kusoma vitabu, magezeti, majarida na
vitu vingine ambavyo vitatufanya vituongezee maarifa na ujuzi. Ngoja nikupe ‘stori’ moja ambayo iliwahi kumpata
rafiki yangu wa karibu. Rafiki ambaye nilisoma kipindi cha nyuma. Mnamo miaka kadhaa baada ya kumaliza masoma
alipata ajira, baada ya hapo aliweza kupata jiko yaani (mke) ambaye walipendana
sana,
Siku moja katika harusi yake alizawadia zawadi
ya kitabu cha Mungu (Biblia) na rafiki yake wa karibu ambayo ndani biblia hiyo
ilikuwa na cheki yenye thamani ya fedha nyingi. Kwa kuwa rafiki yangu huyo hakuwa na tabia ya kusoma vitabu
na hajawahi kuisoma biblia ile ambayo alipewa hivyo hakuiona
cheki ile, kwa hiyo cheki ile aliisha muda wake bila yeye kujua. Mwisho
wa siku yule aliyempa biblia ile alikuja kumuonesha kwamba katikati ya biblia alimuzawadia zawadi ya cheki pia. Kwa kuwa yule rafiki
yangu hakuwa na kawaida kujisomea kitabu. Hivyo alikosa zawadi ya cheki yenye
thamani kubwa ya fedaha nyingi. Kisa
hiki kinatuonesha ni jinsi gani watu
tulivyo kuwa hatupendi kujifunza mambo mbalimbali kwa njia ya kusoma.
JIFUNZE JINSI UNAVYOWEZA KUPATA MAFANIKIO. |
Mafanikio ya kweli huja kwa mtu kuwa
tayari kujifunza vitu vipya kila siku.
Kiuhalisia ni kwamba watu wengi
wanaamini kujifunza ni mpaka uingine
darasani kitu ambacho sio kweli hata kidogo. Mtu anaweza Kujifunza
kwa kutazama vitu au shughuli na jinsi gani watu wengine wanafanya. Kuna
wakati mwingine unahitaji muda wa ziada, kila siku uweze kujifunza vitu hivyo.
Kama kweli unahitaji mafanikio weka ratiba kila siku ya kujifunza vitu vipya
vitakavyokufanya uongeze thamani kwa kile unachotarajia kiweze kutimiza malengo
yako.
Kuna swali dogo huwa najiuliza hivi wasanii wa
nyimbo wangekuwa wanasilisha kazi zao za kwa mashabiki zao kwa njia ya
maandishi ya kusoma ni wasanii wangapi tungekuwa tunawajua? Uhalisia wa jambo hilo ni kwamba ni wasanii wachache
mno ambao tungekuwa tunawafahamu kwa sababu wengi wetu hatupendi kusoma vitabu
na vitu vingine. Ewe mdau wa makala haya jaribu kuhakikisha ya kwamba kila
wakati unajifunza vitu vipya. Jiulize ni kitu gani ambacho umekipa kwa kila
siku kwa njia ya kujifunza?
Jambo
la pili jiulize maswali kwa kila jambo.
Kwa msaka maendeleo na mafanikio kuwa na tabia hii ya kujiuliza maswali ni kawaida.
Kama wewe huna utaratibu huu wa kujiuliza maswali inawezekana kwa asilimia
kubwa ikawa ndio sababu ya kubaki hapo ulipo. Ila kama kama unataka kufanikiwa
ni lazima ujilize maswali. Kama wewe ni mfanyabiashara, mkulima, mwanafunzi,
fundi au kazi yeyote ile jitahidi kuwa na uratibu wa kujiuliza maswali mfano.
Nifanye nini ili niweze kufanikawa kwa kuongeza wateja, je nifanye nini ili
kufaulu katika masomo yangu na maswali mengine mengi kama hayo.
Wakati unajenga utaratibu huo wa kujiuliza
maswali mwenyewe hakikisha kwa kila swali ambalo unajiuliza unapata majibu ya
maswali hayo. Nafikiri mpaka hapo utakuwa umenielewa vizuri. Kuna msanii mmoja
hapa nchini aliwahi kuimba ya kwamba utaratibu wake ni kuuliza why, hivyo hata
wewe jijengee utaribu huo utaona ni kwa jinsi gani utavyofanikiwa. Niliyoyasema
hapo juu yote ni uongo kama utashindwa kuchukua hatua, yatakuwa ukweli endapo
utaamua kuyaweka katika matendo
Asante sana kwa kuendelea kujifunza kupitia
mtandao wa Dira ya mafanikio. Mpaka
kufikia hapo sina la ziada tukutane tena katika makala ijayo.
Makala
imeandikwa afisa mipango na maendeleo ;Benson chonya
Simu;
0757-909942
Barua
pepe; bensonchonya@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.