Apr 18, 2016
Maswali Ya Kujiuliza Ili Kupata Mafanikio.
Wakati mwingine hauhitaji nguvu nyingi katika kusaka mafanikio, ila
unahitaji akili za kufikiri ili kuyapata hayo mafanikio. Ukishapata hayo
mafanikio ndipo unapohitaji nguvu nyingi katika kufanya kazi. Inawezakana ukawa
hajanielewa, ngoja nikueleweshe ni kwamba kila kitu kinaanza na kufikiri hapa
ndipo wazo linapoanza kutengenezwa. Wazo hilo likishakamilika ndipo unapohitaji
nguvu katika kufanya kazi.
Mpenzi msomaji wa makala hii siku ya leo tutangalia katika kujua umuhimu wa kufikiri
ili kupata mafanikio. Mara kadhaa nimekuwa nikiandika ya kuwa watu wengi
tumekuwa na maisha yaleyale ambayo yanatufanya tusisonge mbele kimafanikio hii
ni kwa sababu tumekuwa tunafikiri mambo ya kawaida sana.
Mambo ambayo unahitaji kujiuliza
ili kupata mafanikio.
1. Unataka kuwa na nani?
Hili ni swali la muhimu sana la kujiuliza uwe unayetaka mafanikio
zaidi. Mfano wewe ni mwanafunzi wakati unasoma katika masomo yako je umewahi
kujiuliza unataka kuwa na nani katika maisha yako ya hapo baadae? Pia na wewe
mfanya biashara katika maisha yako umewahi kujiuliza unataka kuishi maisha
gani? Je, biashara yako unataka iweje baada ya miaka kadhaa? Je, unataka kuwa
hapo ulipo au unataka kuwa mfanyabishara mkubwa au mdogo?
Ukishajiuliza maswali hayo lazima ujiulize tena sifa hizo unazo au
huna? na kama huna sifa hizo unazipata wapi? Ewe unayesoma makala haya shusha
pumzi kisha twende sawa hebu jione upo
mahali baada ya muda fulani ndoto zako zimetimia. Kimsingi ni kwamba
hayo yote yanakupa nafasi nzuri ya kujua malengo yako na kujua ni kitu gani
ambacho unakihitaji katika maisha yako.
Jiulize maswali ya msingi ili kufanikiwa. |
2. Unataka kutatua matatizo yapi?
Kwenye kutatua matatizo ndipo pesa zilipo. Unashangaa wala
usishangae pia haujakosea kusoma. Ulimwengu wa leo ni ulimwengu wenye matatizo
mengi ambayo yanahitaji majibu na mtoa majibu ni wewe. Unatoa macho ndio wewe
ndiye mtoa majibu ya changamoto zinazowakabili watu. Badilisha mkao uliokaa
kisha tuendelee, aliyegundua facebook leo hii katatua tatizo la watu na
kutukutanisha watu pamoja na kuifanya dunia kuwa kinganjani mwako na
tunafurahia maisha hayo, mtu huyo leo ni miongoni mwa watu matajiri ulimwenguni
kwa sababu aliweza kusoma mazingira na kuona watu tuna changamoto yeye akaja na
changamoto.
Kutatua changamoto za watu hauhitaji mifano kutoka kwa wazungu ila
kila jambo unalotaka kulifanya kumbuka liwe linatoa majibu ya changamoto ya
watu. Wewe unayefanya biashara ya kuuza chipsi endelea na kazi hiyo maana unasaidia
unatatua tatizo la njaa kwa haraka zaidi, kitu cha msingi ongeza ubunifu katika
kazi yako ili kuongeza wateja wengi zaidi. Huo ni mfano tu ila kumbuka
kutatutua matatizo ya watu ili kupata pesa.
Hadi kufikia hapo afisa sina la ziada, kitu cha msingi na cha
kukumbuka ni kwamba endelea kufuatilia makala za kimafanikio ili uweze
kufanikiwa zaidi.
Imeandikwa na : Afisa mipango na
maendeleo Mr. Benson chonya
Simu: 0757-909942
Barua pepe;
bensonchonya23@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.