Apr 7, 2016
Siri 10 Kwa Nini Watu Wengi Hushindwa Kutimiza Malengo Yao.
Kila mtu ana malengo na mipango mingi ya kufanya kila siku
katika maisha yake. Lakini kitu cha kujiuliza mbona mipango na malengo ya wengi
huwa hayatimii kama ilivyokusudiwa? Katika makala hii ya leo ungana nami nikupe
siri 10 za kwa nini wengi hushindwa
kutimiza malengo yao japo wanajitahidi kila siku kufanikisha malengo hayo
lakini hayatimii?
1.Kushindwa kubadili tabia katika matumizi ya pesa na muda. Watu
wengi hawana nidhamu katika matumizi ya pesa na muda.
2. Kutokuwa na bajeti katika matumizi ya pesa.
3. Kutokujua tofauti kati ya mahitaji muhimu na mahitaji ya
lazima. Hivyo kujikuta wanatumia pesa nyingi kataka vitu vya muhimu na kuacha vitu vya lazima.
4. Kuwa na matumizi makubwa kuliko vipato vyao. Hali
inayopelekea watu kuwa na tabia za udokozi,wizi na hatimae kuwa mafisadi.
ISHI KWA MALENGO SAHIHI, UTAFANIKIWA. |
5. Kutegemea chanzo kimoja tu cha mapato. Mtu kutegemea mshahara
pekee au kiduka kidogo alichofungua bila kubuni mradi mwingine hii ni hatari
sana.
6. Kukosa malengo sahihi katika maisha, Utakuta mtu hajui
afanye nini na aache nini katika maisha yake anakuwa yupo yupo tu ilimradi yupo
duniani.
7. Kukosa mwendelezo katika mambo yakufanya. Utakuta mtu akipata
hasara anakata tamaa kabisa na kuacha kufanya au akipata faida kubwa anaridhika
na kwenda kutumbua kwanza hadi pesa iishe ndipo akumbuke tena kufanya.
8. Kukosa ufuatiliaji na utekelezaji wa mipango na malengo
anayojipangia. Anaishia kusema tu kwa mdomo tu nitafanya hivi na vile hadi
mwaka unaisha.
9. Kukosa imani katika jambo au malengo aliyopanga. Anahofu katika
kufanya jambo kwa sababu anaweza pata hasara, Anaweza kata mtaji. Atalogwa na
watu watamwonaje akifanya mradi au biashara ile.
10. Kukosa taarifa sahihi kwa muda sahihi. Hapa ndipo kiini cha
kukosa mafanikio kilipo. Kamwe huwezi kupata mafanikio katika jambo lolote lile
mpaka upate taarifa sahihi. Huwezi kuoa au kuolewa na mtu usiyekuwa na taarifa
zake sahihi, huwezi kulima zao ambalo hujui utamuuzia nani, Huwezi kujenga
nyumba wakati hujaonana na fundi ujenzi akupe taarifa na vitu gani
ununue,huwezi kwenda chuoni kusomea fani ambayo hujui utaajiriwa na nani, Huwezi
kufanya sherehe usiyojua gharama zake utazimudu? TAARIFA TAARIFA TAARIFA.
Asante kwa kunifatilia, kumbuka kuchukua hatua.
Ni wako rafiki katika kusaka mafanikio na kuonyesha njia za
mafanikio Shariff Hamisi Kisuda maarufu mzee wa Nyundo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.