Apr 13, 2016
Tabia Zinazokuzuia Ushindwe Kupata Pesa Kwa Kiasi Kikubwa.
Katika safari ya maisha ya mafanikio, kitendo cha kutengeneza
pesa nyingi ni kitu au hatua ambayo kila mtu anataka aifikie. Bila shaka
utakubaliana nami hakuna mtu ambaye haitaki pesa, kila mtu kuamka hadi kulala
kwake shughuli zake nyingi karibu zote zinahusisha juu ya kupata pesa. Hiyo
yote inaonyesha pesa inahitajika kwa namna yoyote ile kwa wingi na tena kwa
kila mtu.
Lakini hata hivyo pamoja na kiu yote hiyo ya kutaka
kuwa na mafanikio makubwa ya kifedha wengi wetu bado huwa hawafanikiwi. Unajua
ni kwa nini? Ngoja nikwambie. Kwa kawaida huwa yapo mambo mengi yanayomfanya
mtu huyu apate pesa nyingi na mwingine akose. Lakini leo hii nataka nikupe siri
na kukwambia jambo moja tu linakufanya ushindwe kutengeneza pesa ya kutosha. Jambo
hilo si lingine ni tabia.
Ndio. Nimesema ni tabia. Zipo tabia ambazo ukiwa
nazo ni lazima zitakufanya ushindwe kutengeneza pesa kwa kiasi kikubwa. Ni tabia
ambazo wengi tunazo na ni kweli zinaturudisha nyuma kwa kiasi kikubwa. Kwa kusoma
makala haya, utajifunza tabia hizo ambazo zimekuwa kama kizuizi kwako na kukukufanya
ushindwe kupata pesa kwa kiasi kikubwa. Karibu na twende pamoja kujifunza.
1. Tabia ya
kushindwa kuifanya pesa ikuzalishie.
Kati ya kitu ambacho kinakuzuia ushindwe
kutengeneza pesa nyingi, ni kule kushindwa
kuifanya pesa unayoipata ikuzalishie zaidi. Kwa mfano kama unapata
shilingi laki tano kwa mwezi je, unaifanya vipi hiyo pesa ikaongezeka zaidi ya
hapo? Kama unashindwa kuifanya hiyo pesa ikuzalishie zaidi, basi elewa hiyo ni
moja ya tabia inayokufanya ushindwe kupata pesa kwa kiasi kikubwa.
Kitu cha kufanya kama hilo ndilo linalokuzuia,
tafuta ni wapi au eneo lipi unaweza kuwekeza kwa pesa unayoipata. Ukishapata
kitu hicho acha kupoteza muda kwa kujiuliza uliza na anza mara moja kutengeneza
pesa kwa kuiweka kwenye uwekezaji. Kwa kujijengea tabia hiyo kutakufanya uzidi
kutengeneza pesa za ziada. Jambo la msingi na la kukumbuka ifanye pesa yako
ikuzalishie zaidi hata kama ni kiasi kidogo unapata
TOA THAMANI UTENGENEZE PESA ZA KUTOSHA. |
2. Tabia ya kushindwa kutoa thamani.
Ni rahisi kushindwa kupata pesa kwa kiasi kikubwa
kama pia utashindwa kutoa thamani kwa kile unachokitaka. Mara nyingi mafanikio yoyote
yanaanza kwa kutoa thamani uliyonayo ndani mwako kwanza. Kwa mfano hapo ulipo
kuna kiasi fulani cha pesa unachokipata kwa mwezi. Kiasi hicho cha pesa hakiji
hivi hivi bali kuna thamani au kitu unachokitoa ndani mwako kinachopelekea
upate pesa hiyo.
Kama tafsiri yake
iko hivyo, hiyo inamaanisha kwamba kama unashindwa kutoa thamani kubwa
maana yake utashindwa kutengeneza pesa nyingi. Wengi kutokana na kuishi kwa mazoea wamejikuta
wakiwa ni watu wa kuishi maisha yale yale bila kutoa thamani kubwa sana. Kwa
kufanya hivyo hujikuta ni watu wa kushindwa kutengeneza pesa nyingi karibu muda
wote wa maisha yao.
3.Tabia ya
kufanya mambo kwa ukawaida sana.
Sumu kubwa ya kufikia mafanikio makubwa na
kushindwa kutengeneza pesa kwa kiasi kikubwa ni kufanya kazi kwa ukawaida sana,
Watu wengi wana mazoea ya kufanya kazi kwa viwango vya kawaida. Ili uweze
kufanikiwa na kutengeeza pesa nyingi maishani mwako, jifunze kufanya kazi kwa
bidii zote bila kuchoka. Kwa kadri utakavyozidi kuongeza juhudi katika kafanya
kazi kwa bidii itakufanya uzidi kutengeneza mpato makubwa sana.
Kama unafikiria natania, angalia watu ambao maisha
yao yote wameyaweka kwenye kujituma huku wakiwa wamekubali kujifunza. Watu hawa
mara nyingi wanatengeneza pesa nyingi sana kutokana na kile wanachokifanya kwa
juhudi zote. Kwa hiyo moja ya kitu
kinachokufanya ushindwe kutengeneza pesa
nyingi sio mkosi au laana kama unavyofikiri bali ni kufanya kazi kwako kwa
ukawaida. Jitume mara kumi ya hapo tuone ni nini kitakutokea kwenye maisha
yako.
4. Tabia ya
kuridhika mapema.
Kuna watu wana tabia hasa pale wanapopata mafanikio
madogo tu, huwa ni watu wa kuridhika sana. Huwa ni watu wa kujiona wamefika na hata
zile juhudi kubwa walizokuwa nazo mwanzo zinakuwa zinapotea kidogo kidogo kwa
sababu ya mafanikio hayo. Unapokuwa na na tabia kama hii tambua kabisa hicho ni
chanzo kikubwa sana kinachokufanya
ushindwe kutengeneza pesa nyingi.
Kwa mfano jaribu kuangalia baadhi ya wasomi wetu,
akijenga nyumba na kununua gari kwao ndio basi. Maisha huwa kama yameishia hapo
na hakuna juhudi kubwa tena wanayokuwa wanaifanya. Kitu cha kuelewa mafanikio
sio nyumba wala gari peke yae. Tunatakiwa kufanya mambo makubwa zaidi ya hapo. Kama
mafanikio ni nyumba tu sasa jambo la kujiuliza ni nani ayeishi kwenye tundu
kama ndege, bila shaka hakuna. Hivyo acha kuridhika, ili utengeneze pesa za
kutosha.
Kimsingi zipo tabia nyingi ambazo zinaweza zikakuzuia
wewe ukashindwa kupata pesa kwa kiasi kikubwa na kukufanya usifikie mafanikio
mkubwa. Lakini kwa kupitia makala haya hizo ni baadhi tu ya tabia hizo.
Ansante kwa kuwa msomaji mzuri wa DIRA YA MAFANIKIO
lakini washirikishe wengine waendelee kujifunza kila siku kupitia mtandao huu.
Ni wako rafiki,
Imani
Ngwangwalu,
Simu;- 0713
04 80 35,
Email-; dirayamafanikio@gmail.com
Blog;- dirayamafanikio.blogspot.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.