Jul 29, 2016
Unachokiamini Ndicho Unachopokea Na Kufanya.
Mwanafalsafa mmoja aliwahi sema “You
cannot do beyond what you know and you cannot know beyond what you believe...therefore what you believe determines what you know and do”
Huwezi kufanya nje ya unavyojua
na huwezi kujua nje ya unavyoamini...kwa hiyo unachoamini kinapelekea kujua
kwako na kufanya kwako.
Hebu sisi tuchambue haya maneno muhimu matatu:-
Hebu sisi tuchambue haya maneno muhimu matatu:-
Unachoamini.
Watu huamini tofautitofauti juu ya sababu za wao kuwa vile walivyo.Mwingine
atakwambia yupo katika hali ya kushindwa kufanya vizuri kwa sababu ya mtu
fulani,au jambo fulani lililowahi kutokea maishani mwake.
Mwingine anaamini kuwa ni kwa sababu tu bado hajachukua hatua ya
kubadili hali yake. Huyu wa pili ana kheri ingawa wote wawili wapo sahihi
kufikiria hivyo kwa sababu ndivyo wanavyoamini.
Kwa mujibu wa mwandishi Orison Swett Marden "What we sincerely believe regarding ourselves is true for
us". Tunachokiamini kuhusiana na sisi wenyewe ni sahihi kwetu.
Unachokijua.
Kwa kawaida mwanadamu yeyote hawezi kufanya jambo bila kutafuta
maana(they search for meaning) bila kujali chanzo cha hiyo maana na kama maana
hiyo ni sahihi au sio sahihi...hutaka tu kuona anachofanya kina msaidia kwa
namna fulani.
Maana yangu hapa ni kwamba ni muhimu kutumia asili hiyohiyo
kutanua uwezo wa kujua ZAIDI ili kupata maana kubwa zaidi kuliko kuishia
kung'ang'ania maana moja uliyoipata juu ya jambo husika.Kusoma vitabu,kuuliza
na kusikiliza wengine kwa makini huongeza uwezo wa mtu kujua zaidi.
Unachofanya.
Mtu yeyote timamu lazima afanye jambo kwa kuangalia maslahi
yanayotokana na kuwekeza nguvu yake hapo.Vinginevyo ataachana nalo na kuangalia
ustaarabu mwingine.
Kwa hiyo kwa mtu mwenye lengo la kufanya vizuri iwe katika
masomo, biashara, kilimo, michezo, mahusiano, ufundi nk ni muhimu kuzingatia
ngazi hizo tatu muhimu zinazotegemeana LAKINI mlango mkuu ni kubadilisha
UNACHOKIJUA.
Jenga tabia ya kutamani kujua vitu vipya, mbinu mpya na mwelekeo
mpya ili uweze kufika unapotamani kufika siku moja.
Imeandikwa na Moses Mkemwa
(Uncle Moses)
0757717572
(Uncle Moses)
0757717572
Jul 28, 2016
Jinsi Ya Kutengeneza Chili Sauce.
Kama utakuwa ni mfutialiaji mzuri wa mtandao huu, siku chache zilizopita tuliweza kukulete makala ambayo ilikuwa inahusu ni jinsi gani unaweza kutengeneza tomato souce, namshukuru Mungu kuna watu wengi walichukua hatua na sasa wameanza kutengeneza pesa kupitia utalamu huo wa utengenezaji wa tomato souce.
Nakusihi hata wewe ambaye unasoma makala haya leo uweze kuchukua hatua mathubuti juu ya somo hili la leo na kuona ni wapi ambapo na wewe utatengeneza pesa kupitia somo hilo, maana somo hili si kwa ajili ya kukupa hamasa bali ni kwa ajili ya vitendo na kutengeneza pesa, nakuomba urudie kwa mara nyingine kusoma aya hii, maana kiukweli somo hili ni hili ni pesa mkononi.
Afisa mipango kwa moyo wa ajasiri nimeamua kukuletea somo hili ili nikutoe katika kundi la watu ambao wanalalamika kwamba Maisha magumu, ajira hakuna, mara serikali ya awamu hii inabana na sababu nyinginezo kama hizo, ambazo kwa upande wangu huwa naziona ni stori nyoka tu.
Weka maandalizi yako mapema. |
Pasipo kumung'unya maneno, wala kushika simu yangu kuangalia kama kuna meseji au kuna mtu kanipigia, wala bila ya wewe kukuchosha nadhani niende moja kwa moja kwenye maada amabayo siku majawabu tosha ya wewe kupata pesa.
Yafutayo ndiyo mahitaji kwa ajili ya kutengenezea chili souce;
a) Pilipili mbuzi nyekundu robo 1/4 kilo.
b) Nyanya kilo moja.
c) Kitunguu swaumu kikubwa kimoja.
d) Mafuta ya kula vijiko 7 vya chakula.
e) sukari vijiko viwili vya chai.
f) maji ya moto kikombe kimoja cha chai.
g) vinega vijiko 3 vya chai.
Baada ya kuandaa mahitaji hayo ya jinsi ya kutengeneza chili souce, twende kuona moja kwa moja jinsi ya kutengeneza chili souce
HATUA YA KWANZA.
-Kata Pilipili kuondoa mbegu.
-menya nyanya kuondoa mbegu pia.
-menya vitunguu swaumu kisha
vikatekate viwe katika vipande vidogo vidogo.
Nb; baada ya kumaliza hatua hiyo ya maandalizi chukua Brenda, kisha saga mchanganyiko wote wa malighafi ambazo nimezianisha kwenye hatua ya kwanza. Saga mchanganyiko huu mpaka uone imetoka rojo laini.
HATUA YA PILI.
Ukishamaliza kusaga mchanganyiko huu hapo juu jambo ambalo unatakiwa kulifanya ni;
*Chukua sufuria yenye nafasi ya kutosha kwa ajili ya kupika mseto huu.
*Weka sufuria yako jikoni, iache kwa sekunde kadhaa ili ipate moto pia kama kuna maji katika sufuria yaweze kukauka.
*Baada ya kuona sufuria yako imekwisha kupata moto, chukua mafuta ya kula yaweke kwenye sufuria, yaache yachemke.
* mafuta yakichemka chukua mseto wako mwagia katika sufuria yako, koroga mseto huo kuelekea upande mmoja kwa dakika 30 huku mseto huo ukiendelea kuchemka.
* Baada ya dakika 30 epua mseto huo na uuache upoe, kisha funga katika vifungashio kwani mseto huo utakuwa umeshakuwa chili souce.
Mpaka kufikia hapo utakuwa umekwisha kutengeneza chili souce ambayo inafaa kwa ajili ya matumizi ya binadamu kwani ni salama kwa ajili ya afya yetu.
Endelea kufuatilia mtandao huu Wa DIRA YA MAFANIKIO kwani uongozi wa mtandao huu umeandaa masomo mazuri kwa ajili yako, ambayo yatakufanya uweze kufanikiwa katika maisha yako.
Ndimi; Afisa mipango; Benson chonya
Email; bensonchonya23@gmail.com
0757909942
Jul 27, 2016
Je! Wajua Ni Kwa Nini Mpaka Leo Malengo Yako Hayajatimia?
Moja
yachangamoto ambayo inawakabili watu wengi ni kwamba ni wazuri sana wa kusema
kuliko kuchua hatua, hapa nina maana ya kwamba kila mmoja anapenda kuona matarajio
yake yanatimia.
Hata
hivyo, kutokana na imani hiyo imepekelekea watu wengi sana kubaki na maisha
yale yale kila siku. Unajua ni kwanini? Basi nakusihi ufuatane nami kwani
nataka nikijuze siri ambayo watu wengi hawaijui juu ya upangaji wa malengo.
Ipo
hivi niliwahi kufanya uchunguzi mdogo katika kazi yangu ya uhamasishaji mahali
fulani, moja ya mada ambayo nilikuwa naizungumzia siku hiyo ilikuwa inahusiana
na jinsi gani unavyoweza kutimiza
malengo yako na kila mmoja ilionekana kufurahia somo hilo. Kila mmoja
wetu ambaye ulikuwepo siku hiyo ilionekana dhahiri anayo ndoto ambayo inasukuma
kufikia kilele cha mafanikio.
Ndipo
nikachukua jukumu la kutaka kujua kila mmoja aliyekuwepo siku hiyo ni nini
ambacho anadhamiria katika maisha yake? Kila mmoja alieleza kwa mapana kutoka
na dhamira inavyomsukuma kutoka nafsini kwake. Baada ya kumaliza zoezi hilo la
kujua kila mtu lengo lake, ndipo nikawataka watu hao hao waandike kuhusiana na
njia ya kutimiza ndoto hizo.
Moja
ya maajabu ambayo niliyaaona ni kwamaba watu wengi ni wazuri sana wa kusema
nataka kuwa mtu fulani lakini linapokuja suala la utekelezaji wa jambo hilo
hapo ndipo ukakasi hujitokeza unajua ni kwanini? Niligungundua ya kwamba watu
wengi wana ndoto lakini hawajui mbinu za kutekekeza, hata wale ambao wanajua ni
wepesi sana wa kukuta tama.
Ndipo
nikawambia ya kwamba kwa jambo lolote ambalo unalitamani liwe kweli ni lazima
ujue mbinu ya utekelezaji wa jambo hilo hususani kwa kujifunza na ikiwezekana
kulipa gharama, lipa gharama kwa kuwa hakuna maisha ya kimafanikio ambayo
hayana gharama.
Pia
ikumbukwe ya kwamba katika kujifunza hukohuko kuna changamoto zake, changamoto
hizo hizo ndizo ambazo huwafanya watu wachache waweze kuhimili mikiki ya jambo hilo, na hawa ni watu ambao
wamefanikiwa katika sayari hii. Hata hivyo kwa asilimia kubwa ambapo wengi wetu
ambao ndio tupo humo huwa hatupo tayari kuvumilia mikikimikiki ya changamato
ambazo mara nyingi hujitokeza katika mambo amabayo tunayafanya.
Wengi
wetu tupo tayari kuahairisha mambo na
kuleta visingizio visivyokuwa na maana yeyote ile, kwa mfano unakutana na mtu
anakwambia anataka kufanya biashara fulani lakini changamoto yake kubwa ni mataji. Kimsingi ukichunguza changamoto hiyo
utagundua ya kwamba ni sababu yatima, nikiwa na maana ya kwamba huna haja ya
kuacha kufanya jambo fulani eti kwa sababu ambazo hazina msingi wowote.
Tuende
mbele turudi nyuma na kuyatafakari maisha ambayo tunayaishi leo hii, ni kwanini
yapo vile vile? Ni wakati wako muafaka ewe msomaji ambaye unasoma makala haya
kuweza kutafakari kwa umakini jambo hili japo kwa dakika chache na kuendelea
kutafakari juu ya maisha yako.
Tafakari
ni kwanini mpaka leo hii hujatimiza malengo yako? Kama umepata jibu, zama tena
katika halmashauri yako ya kichwa tafakari tena je unahisi sababu ambazo
umezipata ni za msingi au sio za msingi?
Kama umekwisha pata majibu inua macho yako mbiguni, tazama mbigu inavyong`ara
kisha tafakari tena na uje na majibu ya kina je unachukua hatua gani kwa hayo
yote uliyowaza? Usinibe majibu.
Mmmh,
sawa labda nisiendelee kuongea sana, maana naweza nikakupoteza kabisa ila cha
msingi ni kwamba tafakari hayo machache kisha uchukue hatua mathubuti za
kiutendaji. Hata hivyo nikazie kwa kusema ya kwamba mara zote ukiwa na malengo
usiishie kusema tu, bali onyesha njia sahihi za utekezaji. Kufanya hivi kutukupa
mwelekeo tosha kwa upande wako kwa kuonesha ni nini! Ambacho unatakiwa kuwa
nacho? Na baada ya muda gani!
Huenda
bado ukawa haujanielewa nazungumzia masuala ya uwezo wa utekelezaji wa jambo
hilo. Maana tunafahamu ya kwamba ili yaitwe mafanikio kuna njia ya kufikia
mafanikio hayo kwa mfano kujifunza kutoka kwenye vitabu, video, semina na watu
wengine ambao kiujumla wamekwisha fanikiwa. Nikakumbushe kwa mala nyingine kuwa
ni lazima uwe na picha kamili ya kule ambapo unataka kuelekea.
Nikushuru
sana kwa kusoma makala haya, lakini shukrani zangu zangu zitakuwa zimekamilika
endapo utachukua hatua kwa hayo ambayo umekwisha yasoma kwenye makala haya.
Nikusihi ya kwamba ulichojifunza mshirikishe mwenzako kama ambavyo mimi nmefanya
kwako.
Endelea kujifunza kupitia dirayamfanikio.blogspot.com kila siku.
Ndimi;
Afisa mipango Benson Chonya
Blogu;
dirayamafanikio.blogspot.com
Simu; 0757909942
Jul 26, 2016
Hatua Nne Za Kukua Kwa Biashara Yako.
Ili
biashara yako iweze kukua na kukupa mafanikio ni lazima ipitie katika hatua nne
muhimu. Hizi ni hatua ambazo biashara yoyote ile, ili iweze kuleta mafanikio, ni
lazima ipitie hapo bila kuruka hata hatua moja.
Kama
ulivyo umuhimu wa hatua za malezi kwa mtoto kuanzia kutambaa hadi kukimbia na
pia hatua hizi ni muhimu katika mafanikio ya biashara hivyohivyo. Ikiwa ikatokea
hatua moja imerukwa ni rahisi kwa
biashara husika kupoteza mwelekeo au kufa kabisa.
Mpaka
hapo bila shaka utakuwa umeona ni kwa jinsi gani hatua hizi zilivyo za muhimu
katika kukua kwa biashara. Ni hatua ambazo zinampa mfanyabiashara uzoefu wa
kukua siku hadi siku na kupelekea biashara kuleta mafanikio mkubwa.
Je,
hatua hizo ni zipi?
Zifutazo Ni Hatua
Nne Za Kukua Kwa Biashara Yako.
1.
Hatua ya mbegu (Seed stage).
Katika
hatua hii, mara nyingi mjasiriamali anakuwa yupo katika hatua ya kujaribu wazo
la biashara yake kama linafanya kazi au la. Ni hatua ambayo humfanya
mjasiriamali ajaribu mambo mengi ikiwa pamoja na hali ya kuchunguza soko jinsi lilivyo.
Pia
hii ni hatua ambayo biashara kwa namna yoyote ile huhitaji pesa ili iweze
kusonga mbele. Kwa kifupi hii ni hatua inayohitaji umakini sana kwa sababu ndio
msingi na mwanzo wa mafanikio wa hatua zingine zinazofuata. Ikiwa umakini
utapotea hapa ni lazima biashara ife.
2.
Hatua ya kuchipua ( Start-up stage).
Baada
ya kujaribu wazo lako na kuona wazo linafanya kazi, hatua inayofuata baada ya
hapo ni hatua ya kuchipua kwa biashara. Hii ni hatua ambayo sasa unaanza
utekelezaji wa wazo lako. Ni hatua ambayo unakuwa unatafuta wateja wako
mwenyewe sasa.
Katika
hatua hii pia mjasiriamali, ni lazima ujifunze jinsi ya kupata mrejesho kwa
wateja wako. Ni lazima ufahamu wateja wako wanataka nini au hawataki nini ili kufanya maboresho.
Unapozidi kuwa makini katika hatua hii ni lazima idadi ya wateja wako
itaongezeka na biashara itakua pia.
3.
Hatua ya kukua ( Growth stage).
Mara
baada ya bidhaa zako kuwa sokoni, ikiwa utaona bidhaa zako zinatakiwa kwa
wingi, elewa kabisa hapo biashara yako hiyo ina dalili tosha ya mafanikio kwa
kukua.
Sasa
kaika hatua hii, hiki ndicho kipindi ambacho mjasiriamali anatakiwa kuanza
kuangalia ushindani na wafanyabiashara wengine. Ikiwa ikatokea umeweza kumudu
vizuri katika hatua hii, basi ni wazi mafanikio kwenye biashara yako ni lazima
yaonekane.
4.
Hatua ya kukomaa ( Maturity stage).
Hapa
katika hatua hii, biashara yako inakuwa imemudu kuweza kukabiliana na ushindani
wa kila aina. Hiki ni kipindi ambacho biashara yako inakuwa inajitatanua na
kutengeneza matawi katika sehemu zingine tofauti.
Kwa
kifupi, hii ni hatua ambayo mjasiriamali anayaona mafanikio yake kwa sehemu
kubwa. Lakini hata hivyo ni hatua ambayo mjasiriamali pia hatakiwi kulewa zaidi
ya kuendelea kuweka juhudi hadi kufanikiwa zaidi na zaidi.
Kumbuka,
hizo ni hatua muhimu nne ambazo biashara yako ni lazima ipitie ili iweze kukua
na kukuletea mafanikio. Hata hivyo, hizi ni hatua ambazo zinategemeana sana. Kushindwa
kwa hatua moja, ni dalili tosha inayoonyesha pia na hatua zingine zitashindikana
kufanikiwa.
Kitu
cha kujiuliza wewe upo katika hatua ipi? Kwa hatua yoyote uliyopo itakusaidia
kujua kama utafanikiwa au la!
Endelea
kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kujifunza kila siku.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki,
Imani
Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,
Email;
dirayamafanikio@gmail.com
Jul 25, 2016
Sheria Tatu (3) Za Mafanikio (3 Laws Of Success).
Uhali gani mpenzi wa makala haya, ni
matumaini yangu makubwa umzima wa afya kabisa, katika makala hii natakaka
tujikite zaidi katika kujua sheria ambazo zitatufanya tuweze kutimiza
ndoto zetu.
Mara kadhaa umekuwa ukizoea kuona ya
kwamba mahali palipo na sheria lazima pawe chombo au mtu wa kuzisimamia ili
sheria hizo ziweze kutekelezeka kirahisi.
Lakini katika sheria za ya mafaniko
huwa ni kinyume kwa sababu haina haja ya kuwepo chombo au mtu wa kukuongoza
isipo kuwa wewe mwenyewe ndiye nahodha wa Maisha yako.
Maana tunaambiwa ya kwamba hatima ya
maisha yetu tunayo wenyewe. Hiyo ina maanisha kwamba sheria za mafanikio zipo,
uwe unajua au hujui, ila unapovunja sheria hizo lazima uadhibiwe na ulimwengu.
Leo katika makala haya, Afisa mipango
nataka nikushirikishe na wewe sheria tatu tu za mafanikio. Ikiwa ikatokea
ukazitumia sheria hizo uwe na uhakika utafanikiwa.
Zifuatazo Ndizo Sheria Tatu Za Mafanikio.
1. Fikiri (think).
Kila mwanadamu ana uwezo binafsi
ambao amezaliwa nao kwa ajili ya kufiri, lakini fikra hizo hizo hutofautiana
baina ya mtu mmoja na mwingine, hata siku moja hakuna mtu ambaye atafanana
uwezo wa kufikiri na mtu mwingine.
Hata hivyo kila kitu chochote ambacho
unakiona leo hii yupo mwazilishi wa kitu hicho. Hapa ina maana ya kwanza
yupo yule mwanzilishi wa kitu na yupo yule ambaye ni mtaalamu kwa ajili ya
kufanya marekebisho ya kitu hicho andapo kitukuwa hakipo sawa.
Vilevile katika kufanya vitu ambavyo
tunaviona leo vinazidi kuwa katika ubora huohuo hutuna budi kutazama vitu hivyo
katika jicho la tofauti sana, inawezekana bado hujanielewa ila ukweli ni huu
upo utofauti mkubwa kati ya kufikiri na kuwaza.
Mara kadhaa endapo utamsikia mtu
anasema nilitaka kufanya hiki na kile lakini hakijaenda kama alivyokuwa amepaga
ujue fika mtu huyo ni alikuwa anawaza tu. Lakini ukweli ni kwamba ukitaka kufika
kilele cha mafanikio yako huna budi kuweza kufikiri mambo kwa hali juu sana na
sio kuishia kuwaza tu.
Unajua ipo hivi hapa ulimwenguni
hakuna kazi ngumu kama ya kufikiri vitu vipya, na kama nilivyosema hapo awali
ya kwamba kila binadamu ana uwezo wake binafsi ambao amezakiwa nao kwa ajili ya
kufikiri, hapo sasa inategemeana ya kwamba unafikiria nini ?
Je ni mawazo chanya au mawazo hasi?
Tafakari kidogo kisha ugundue juu ya jambo hili .Hata hivyo wapo baadhi ambao
wamefanikiwa kimtazamo hata kimaisha watu hawa wao walifikiri mambo ya msingi
katika mtazamo chanya, ndivyo hivyo ambavyo leo inatupasa mimi na wewe kuweza
kutazama katika mtazamo huo huo ili tuweze kufanikiwa zaidi.
Kwa kuongezea pasipo kumung'unya
mdomo wala kuharibu silabi za matamshi, kila kitu ambacho unakifijiria ambacho
kipo katika mtazamo chanya huna budi kukiandika katika sehemu ambayo mara
kadhaa utakuwa unakiona, kufanya hivi kutakufanya uweze kufikiri kwa kina zaidi
ni kwa jinsi gani ambavyo unaweza ukakitekeleza kitu hicho. Mara kadhaa ukitaka
kufanikiwa zaidi kumbuka kufikiri tofauti.
2. Panga (plan).
Jambo la pili ndugu msomaji wa mada
hii, ni kwamba baada ya kufanya tafakari juu ya jambo lako huna budi kukaa
chini na kutengeneza mpango kazi kwa ajili ya utekelezaji wa jambo hilo. Katika
kupanga mpango kazi wa kile ambacho umekifikiria kitakupa picha kamili juu ya
kile ambacho unatamani kukifanya, hii ikiwa na maana ya kwamba kitakuwa na
matokeo chanya au matokeo hasi.
Kwa mfano labda unataka kufanya
biashara, ni lazima uwe na mpango wa kibiashara (business plan) ambayo itakupa
picha kamali ya jinsi ya biashara yako itakavyokuwa, kufanya hivi ni chachu ya
kufika mahali ambapo unatamani kufika.
Pia yamkini unatamani kufanya jambo
fulani kwa hapo mbeleni hivyo tumia muda huu kupanga mambo ya msingi
yatayokwenda kukufanikishia jambo lako. Maana kuna usemi ambao unasema ukikosea
kupanga mambo ya msingi umekwisha kufeli mambo yako.
3. Fanya (do).
Baada ya kufanya tafakari ya kina,
pia baada ya kupanga namna ya kutekeza, jambo la tatu huna budi kuanza kutenda
jambo hilo, si kutenda tu! Bali kutenda kwa njia tofauti na ulivyozoea kutenda
au watendavyo watu wengine.
Pia kwa jambo lolote ambalo unataka
kulifanya, au umekwisha kuanza kulifanya ili uone ya kwamba jambo hilo lina matokeo
kiasi gani ni lazima ukipende jambo hilo haijalishi lina changamoto kiasi
gani.
Kwa mfano unafanya biashara
haina haja ya kutumia nguvu katika kutafuta wateja bali unachotakiwa ni
kuongeza thamani katika bidhaa au huduma, kufanya hivi wateja watakuja wao
wenyewe, kwa sababu moja ya tabia ya wateja wengi wana tabia ya kuambiana hasa
ni wapi ambapo hutolewa huduma nzuri. Narudia kusema tena penda kutoka ndani ya
dhamira yako kwa jambo lolote ambalo unalifanya, maana hapa ndipo mzizi wa mafanikio
yako ulipo.
Ni matumaini yangu makubwa ya bila
shaka tumeelewana vizuri, na nikuhakikishe tu kwamba endapo ulichokisoma hapo
juu utakwenda kukiweka katika matendo basi mafanikio yanakuja kwako kwa
asilimia zote.
"Naamini katika kujifunza"
kama na wewe unaamini hilo tukutane tena siku nyingine katika makala ijayo.
Ndimi; Afisa Mipango; Benson Chonya.
Email; bensonchonya23@gmail.com
Phone no; 0757909942
Jul 22, 2016
Mambo Ya Msingi Unayotakiwa Kujua Kuhusu Ujasiriamali, Kabla Hujaacha Kazi.
Inawezekana
umechoshwa sana na kazi unayoifanya na una hamasa kubwa ya kutaka kuwa
mjasiriamali kwa kujiajiri. Kama hayo ndiyo mawazo yako, kwanza hongera sana,
kwani unachagua njia sahihi itakayokufikisha kwenye ndoto zako za kweli.
Nasema
hivyo kwa sababu, watu wenye mafanikio makubwa duniani ni wajasiriamali na si vinginevyo.
Lakini pamoja na kwamba umekuwa umechagua njia sahihi ya kukufikisha kwenye
ndoto zako, ipo haja ya wewe kujua mambo ya msingi kwenye ujasiriamali kabla
hujaingia huko.
Kwa
kujua mambo hayo itakusaidia wewe kujiwekea misingi imara itakayokufanya
usitetereke. Naamini kwa kusoma makala haya, itakusaidia usiwe na maamuzi ya
kukurupuka ikiwa upo kazini na unataka kuachana na kazi yako na kuingia kwenye
ujasiriamali moja kwa moja.
Sasa
bila kupoteza muda, twende pamoja kujua mambo ya msingi unayotakiwa kujua kuhusu
ujasiriamali, kabla hujaacha kazi.
1. Ujasiriamali unataka kujituma sana.
Hakuna
ubishi katika hili kama umemua kuwa mjasiriamali wa kweli ni lazima kujituma
sana kila siku. Bila kufanya hivyo hutafika kilele cha mafanikio. Kuna wakati
unatakiwa kufanya kazi kuliko kawaida ili kuweza kufikia kilele cha mafanikio
yako.
Kama
upo kazini na unataka kuingia kwenye ujasiriamali huku ukiamini utakuja
kujiachia sana utakuwa unajipoteza. Hivyo, unachotakiwa kujua kama una mpango
wa kuacha kazi na kuingia kwenye ujasiriamali, elewa unaingia kwenye kambi
inayokutaka kujituma sana ili kuweza kufanikiwa.
Kujituma ni muhimu sana kwa mafanikio ya mjasiriamali yeyote. |
2.Ujasiriamali
hautakupa uhuru wote.
Kama
ilivyo kwa mwajiri wako kuna wakati anaweza kukubana, halikadhalika nao ujasiriamali
uko hivyohivyo. Hata kama unafanya kazi ya kwako kuna mambo ambayo huwezi kuwa
huru kwa asilimia zote, kwani ukifanya hivyo utapoteza mengi.
Kuna
kipindi ambacho utatakiwa kuamka asubuhi na mapema. Pia kuna wakati itatakiwa
kujinyima baadhi ya mambo ili kufikia mafanikio yako. Hiyo yote hutokea, kwani
bila kufanya hivyo, utakaa sana kwa muda mrefu eneo moja bila kufanikiwa, kwa
sababu utakuwa kama unazunguka tu.
3.
Ujasiriamali unataka juhudi ya kujifunza kila siku.
Ili
uweze kuwa mjasiriamali bora na mwenye mafanikio ni lazima ukubali kujifunza
kila siku. Kila wakati ubongo wako ni lazima upokee vitu vitakavyokusaidia
kukubadilisha wewe ili ukubaliane na hali yoyote ya shindani.
Mjasiriamali
wa kweli ni yule anayekubali kujifunza na kurekebisha udhaifu wake pale
unapohitajika. Kujifunza huko hakuishii kwenye maandishi peke yake ila mpaka
kwenye vitendo. Binafsi jiulize upo tayarii kujifunza kila siku? Kama ni ndiyo
endelea na safari yako ya ujasiriamali bila kuchoka.
4.
Hutakiwi kukata tamaa mapema.
Unapoamua
kuwa mjasirimali na kuchagua njia yako mwenyewe, kitu cha kimojawapo cha cha
kukijua, ni kwamba hutakiwi kukata tamaa mapema. Kuna wakati mambo na
mipango yako inakuwa inakwenda hovyo sana lakini unatakiwa kuvumilia bila
kuchoka.
Ukiingia
kwenye ujasiriamali halafu huku ukawa una roho ile ya kukata tamaa mapema hutafika
popote. Kwa hiyo ingia kwenye ujasiriamali ukiwa tayari kwa lolote. Ikitokea hasara
vumilia na kisha chukua jukumu la kuweza kusonga mbele bila kukata tamaa.
Hayo
ndiyo mambo ya msingi unayaotakiwa kujifunza kabla hujaingia kwenye
ujasiriamali. Chukua hatua sitahiki za kubadili maisha yako na endelea
kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki,
Imani
Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,
Email;
dirayamafanikio@gmail.com
Jul 21, 2016
Kitu Unachotakiwa Kuanza Nacho Ili Kujitengenezea Utajiri.
Watu Wengi
wanatafuta utajiri kwa udi na uvumba, japo wengine wachache wanapata na walio
wengi wanakosa na kukata tamaa. Jambo
ambalo ni dhahiri kabisa ni kwamba, watu wengi tunaanza safari ya kutafuta
utajiri kwa kutumia vituo tofauti fofauti na mbavyo vingi havitufikishi kwenye
huo utajiri. Kwahiyo, kitu cha
kujiuliza je? Safari Yetu ya
kutafuta utajiri inapaswa kuanzia wapi?
Katika utafiti na uzoefu wangu nimegundua kwamba, UTAJIRI unaanzia kwenye Fikra.Na "Fikra ni Nguvu Pekee inayoweza kuzalisha utajiri wa kuonekana kutoka kwenye vitu visivyoonekana. Fikra, hichi ndicho kitu unachotakiwa kuanza nacho ili kujitengenezea utajiri.
Kila Kitu unachokifanya sasa hivi kimeanza kama wazo kutoka ndani yako. Hakuna matendo utakayotenda bila kuanzia kwenye fikra (Mawazo). Kwahiyo, ukiwaza kwa namna fulani, basi ujue kwamba utapata utajiri wa namna fulani sawa na ulivyowaza mwanzoni kabla ya kupata utajiri huo.
Fikra au mawazo,
ndio kitu pekee ambacho huweza kukusukuma kufanya vitu fulani fulani ambavyo ndivyo
huweza kukuletea utajiri. Utajiri
sio dhambi, bali ni sehemu ya Maisha, tumeletwa hapa duniani kuweza kutawala
vilivyopo na kama ukiweza kuvitawala vizuri ni lazima utakuwa tajiri.
Unachohitaji ni
kuweza kugeuza ndoto yako kuwa kweli. Wakati
ukifanya yote hayo, kumbuka Kuwa, wewe ni mtu mwenye thamani kubwa sana
isiyokuwa na mwisho. Hata
kama wewe unajiona sio mtu mbunifu, hata kama ulishashindwa huko nyuma, hata
kama unafikiri umeshajaribu kila Kitu ila ukashindwa, jua kwamba bado una nafasi
Kubwa ya kupata Chochote unachotaka.
Huwezi kuishi maisha
unayoyataka, huwezi kuishi maisha yenye uhuru kama huna utajiri. Huwezi
kuinuka na kufikia juu kwenye chochote unachofanya kama Kweli huna uhuru wa
kipato. Ndio Maana ni muhimu sana Kwako Kuwa tajiri.
Kwa Kawaida
binadamu tunazo nia tatu ambazo nazo tunaishi, yaani mwili, akili Na roho. Njia
hizi ndizo utengeneza maeneo muhimu ambayo utuongoza Kuishi ama maisha ya
utajiri au maisha ya umaskini. Maeneo
hayo yote matatu ni muhimu sana katika kuishi maisha yenye mafanikio na furaha. Ni
Lazima mwili Uwe na utajiri, akili iwe ya utajiri Na Roho pia iwe na utajiri, hapo
ndipo itawezekana wewe kuifikia ndoto yako ya utajiri.
Lengo la maisha yetu
ni maendeleo yaletwayo na utajiri na wala si Kitu kingine. Msingi
mkuu wa maisha ni kuendelea kupiga Hatua za kusonga mbele.
Kama kila Kitu kwenye maisha kinakazana kuwa zaidi ya kilivyo sasa, iweje wewe leo uendelee kuwa hivyo miaka na miaka yote? Mti unakazana kukua zaidi ya ulivyo sasa.
Na Wewe Binadamu pia ni Lazima ukazane kuwa bora zaidi ya ulivyo sasa kwa maeneo yote muhimu ya maisha yako. Katika harakati zako za kutafuta utajiri, Lazima kuhakikisha Kuwa fikra zako zinakuwa safi muda wote. Unatakiwa kutumia nguvu ya utashi wako kuzuia akili yako isilishwe mambo ya Umasikini, na ifanye akili yako ibaki imeshikiria imani na kusudi la maono ya kile unachotaka kufanya au kuumba.
Kama kila Kitu kwenye maisha kinakazana kuwa zaidi ya kilivyo sasa, iweje wewe leo uendelee kuwa hivyo miaka na miaka yote? Mti unakazana kukua zaidi ya ulivyo sasa.
Na Wewe Binadamu pia ni Lazima ukazane kuwa bora zaidi ya ulivyo sasa kwa maeneo yote muhimu ya maisha yako. Katika harakati zako za kutafuta utajiri, Lazima kuhakikisha Kuwa fikra zako zinakuwa safi muda wote. Unatakiwa kutumia nguvu ya utashi wako kuzuia akili yako isilishwe mambo ya Umasikini, na ifanye akili yako ibaki imeshikiria imani na kusudi la maono ya kile unachotaka kufanya au kuumba.
Kamwe
usizungumze: Jitahidi
usizungumzie kuhusu matatizo yako ya ya zamani kifedha kama Ulikuwa nayo; usiyafikirie
kabisa. Usizungumze kuhusu umaskini wa wazazi wako au ugumu wa maisha yako ya
huko nyuma. Kufanya lolote Kati
ya hayo ni kujiweka katika umaskini kwa wakati Huu ulionao sasa.
Weka umakini na
mambo yote yanayohusiana nao kado au nyuma yako kabisa. Linda
mazungumzo yako: Kamwe
usizungumze kuhusu masuala yako au chochote kile kwa namna ya kuvunja moyo au
kukatisha tamaa. Kamwe usikubali uwezekano wa kushindwa au kuzungumza kwa namna
inayoashiria kushindwa.
Unatakiwa
kutozungumza Kuhusu nyakati kuwa ngumu au mazingira ya Baza Kama Vile una
mashaka. Nyakati zinaonekana kuwa ngumu kwa
wale walio na usawa wakushindana na wenzao. Lakini,
wewe unayetafuta utajiri wako hunabudi kuanza kujifunza maisha yale ambayo
unashindana na malengo yako au ndoto zako basi.
Kumbuka siku zote Mafanikio ni
mchakato siyo tukio . Kwahiyo,
Kama Wewe umeweza kujifunza Kitu Chochote kipya na cha Thamani kutoka kwenye
makala hii ni Wazi kwamba Tayari umeanza mchakato wa kuelekea mafanikio.
Jul 20, 2016
Mambo Ya Msingi Kuzingatia Katika Kilimo Cha Alizeti.
Alizeti hulimwa kwa wingi katika
mikoa ya Shinyanga, Singida, Dodoma, Iringa, Tabora, Morogoro, Ruvuma, Mbeya,
Arusha, Manyara, na Rukwa. Zao hili hulimwa kwa ajili ya chakula na biashara.
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA WAKATI WA
UZALISHAJI
Kuchagua aina bora ya mbegu. Chagua aina bora ya mbegu inayovumilia magonjwa,
wadudu, inayotoa mazao mengi na kiwango kikubwa cha mafuta. Vilevile chagua
aina ya mbegu ambayo hukomaa kwa wakati mmoja ili kurahisisha uvunaji.
KUWEKA MBOLEA
Rutubisha udongo kwa kutumia mbolea
za mboji na samadi ili kupata mazao mengi na bora.
KUDHIBITI WADUDU NA MAGONJWA
Alizeti hushambuliwa na magonjwa ya majani, mizizi na masuke ambayo husababisha upungufu wa mavuno. Hivyo ni muhimu kuyadhibiti ili kupata mavuno mengi na bora. Pia ndege hupunguza mavuno kwa kiasi cha asilimia 50 au zaidi. Njia ya kudhibiti ndege ni kwa kuwafukuza na kupanda mbegu zinazokomaa mapema.
Alizeti hushambuliwa na magonjwa ya majani, mizizi na masuke ambayo husababisha upungufu wa mavuno. Hivyo ni muhimu kuyadhibiti ili kupata mavuno mengi na bora. Pia ndege hupunguza mavuno kwa kiasi cha asilimia 50 au zaidi. Njia ya kudhibiti ndege ni kwa kuwafukuza na kupanda mbegu zinazokomaa mapema.
MAANDALIZI KABLA YA KUVUNA;
UKAGUZI
Kagua shamba kuona kama alizeti imekomaa. Alizeti hukomaa kati ya miezi minne hadi sita tangu kupanda. Wakati huo punje huwa na unyevu wa asilimia 25. Ni muhimu kuvuna alizeti mapema ili kuepuka mashambulizi ya panya, mchwa na ndege waharibifu.
UKAGUZI
Kagua shamba kuona kama alizeti imekomaa. Alizeti hukomaa kati ya miezi minne hadi sita tangu kupanda. Wakati huo punje huwa na unyevu wa asilimia 25. Ni muhimu kuvuna alizeti mapema ili kuepuka mashambulizi ya panya, mchwa na ndege waharibifu.
DALILI ZA ALIZETI ILIYOKOMAA
Suke hubadilika rangi kutoka manjano na kuelekea kuwa nyeusi. Viuwa vya pembeni mwa suke hunyauka na hubadilika kutoka rangi ya manjano na kuwa ya kahawia.
UVUNAJI, UKAUSHAJI NA UBEBAJI
Suke hubadilika rangi kutoka manjano na kuelekea kuwa nyeusi. Viuwa vya pembeni mwa suke hunyauka na hubadilika kutoka rangi ya manjano na kuwa ya kahawia.
UVUNAJI, UKAUSHAJI NA UBEBAJI
Vifaa vya kuvunia na kubebea kutoka
shambani
Kisu, Vikapu, Magunia, Matenga Vifaa vya kukaushia, Maturubai, Mikeka, Kichanja bora, Vyombo vya usafiri kutoka shambani, Matoroli, Matela ya matrekta, Mikokoteni ya kukokotwa na wanyama, Magari KUVUNA Alizeti huvunwa kwa kutumia mikono ambapo suke hukatwa kwa kutumia kisu.
Kisu, Vikapu, Magunia, Matenga Vifaa vya kukaushia, Maturubai, Mikeka, Kichanja bora, Vyombo vya usafiri kutoka shambani, Matoroli, Matela ya matrekta, Mikokoteni ya kukokotwa na wanyama, Magari KUVUNA Alizeti huvunwa kwa kutumia mikono ambapo suke hukatwa kwa kutumia kisu.
Pia mashine (combine harvester)
hutumika kuvunia alizeti katika nchi zinazolima alizeti kwa wingi. Masuke ya alizeti
huwekwa kwenye vikapu ambavyo hutumika kusomba alizeti ndani ya shamba. Kisha
alizeti hufungashwa kwenye magunia na kusafirishwa hadi nyumbani tayari kwa
kukausha.
KUKAUSHA
Kuna hatua mbili za kukausha alizeti;
kukausha masuke na kukausha mbegu za alizeti. Kukausha masuke . Masuke
hutandazwa kwenye kichanja bora katika kina kisichozidi sentimita 30 ili yaweze
kukauka vizuri. Vilevile huweza kutandazwa kwenye maturubai, mikeka au
sakafu safi. Lengo la hatua hii ni kukausha masuke ya alizeti ili kurahisisha
upuraji.
KUPURA Upuraji hufanyika baada ya
kuhakikisha kuwa masuke ya alizeti yamekauka vizuri. Masuke ya alizeti hupurwa
kwa kutumia mikono ambapo mbegu hutenganishwa kwa kupiga masuke taratibu
kutumia mti. Ni muhimu kupiga masuke taratibu ili kuepuka kupasua mbegu. Pura
kwenye kichanja bora, maturubai au mikeka.
KUKAUSHA MBEGU
Mbegu za alizeti hukaushwa juani kwa
kutandazwa kwenye vichanja bora, maturubai, mikeka au sakafu safi. Tandaza
mbegu katika kina kisichozidi sentimita 4 ili ziweze kukauka vizuri.
Lengo la hatua hii ni kukausha mbegu baada ya
kupura ili kufikia kiwango cha unyevu kinachotakiwa kwa hifadhi salama ambacho
ni asilimia 8.
JINSI YA KUTAMBUA MBEGU ZILIZOKAUKA
VIZURI
Kufikicha mbegu
Mbegu zilizokauka
maganda yake hutoka kwa urahisi zinapofikichwa. Kumimina kwenye chombo kama
debe, Mbegu zilizokauka hutoa mlio mkali zinapomiminwa kwenye vyombo
hivyo. Mbegu zilizokauka hung’ara Kutumia kipima unyevu. Mbegu zilizokauka
vizuri kipimo huonyesha asilimia 8.
KUPEPETA NA KUPEMBUA
Kupepeta na
kupembua hufanyika ili kuondoa takataka kama vile mawe, wadudu, mapepe, mbegu
zilizooza au kupasuka. Mbegu za alizeti hupepetwa kwa kutumia ungo au mashine
zinazoendeshwa kwa mkono, injini au umeme. Mashine hizi zina uwezo wa kupepeta
na kupembua kilo 60 hadi 350 kwa saa kutegemea aina ya mashine na ukubwa wa
mashine yenyewe
KUHIFADHI
Alizeti iliyopurwa huhifadhiwa katika
hali ya kichele kwenye maghala bora, yaani vihenge, sailo au bini. Alizeti ya
kuhifadhi kwenye maghala ya nyumba ifungashwe kwenye magunia na ipangwe kwenye
chaga kwa kupishanisha. Ili kurahisisha kazi ya kukagua ghala, acha nafasi ya
mita moja kutoka kwenye ukuta. Ziba sehemu zote za ghala ili kuzuia panya
kuingia.
Panya hupenda sana kula punje za
alizeti, na husababisha upungufu mkubwa wa punje ambao husababisha upotevu wa
asilimia 30 kwa kipindi cha miezi mitatu ya hifadhi. Asilimia ya upotevu
inaweza kuwa kubwa zaidi kutegemea idadi ya panya na upatikanaji wa vyakula
vingine kwa wakati huo. Matumizi ya Mbegu za Alizeti Mbegu za alizeti hasa
zenye mistari zinaweza kuliwa baada ya kukaangwa au kukaushwa. Pia zinatumika
katika utengenezaji wa mikate. Mbegu za alizeti husindikwa kupata bidhaa ya
mafuta.
KUSINDIKA MBEGU ZA ALIZETI KUPATA
MAFUTA
Vifaa
Mashine ya kukamua mafuta
Chujio safi
Ndoo
Vifungashio
Sufuria
Mizani Malighafi
Mbegu za alizeti
Maji
Chumvi
NJIA YA KUKAMUA MAFUTA
Chagua mbegu bora za alizeti
Zianike kwenye jua kwa muda wa saa 1
hadi 2
W eka kwenye mashine ya kukamulia ya
daraja au Ram
Kamua mafuta
Chuja mafuta kwa kitambaa au chujio
safi
Pima mafuta yaliyokamuliwa.
Ongeza maji na chumvi. Katika lita 10
za mafuta weka lita moja ya maji na gramu 200 za chumvi.
Weka mafuta kwenye chombo cha
kuchemshia (sufuria)
Chemsha hadi maji yote yaishe
Sauti ya kuchemka ikiisha ni dalili
kuwa maji yamekwisha.
Ipua, acha yapoe, kisha chuja kwa
kitambaa safi au chujio
Fungasha kwenye vyombo safi na vikavu
na vyenye mifuniko
W eka lakiri na lebo
Hifadhi kwenye sehemu safi, kavu na
yenye mwanga hafifu.
MATUMIZI
Mafuta hutumika katika mapishi
mbalimbali na yana virutubishi vifuatavyo: - Mafuta gramu 100 Nguvu kilokalori
900
WASTANI WA MAVUNO YA ALIZETI KWA EKARI MOJA.
Ukipata shamba zuri ekari moja ya alizeti huweza kukupatia
kati ya magunia5-10 kutegemeana na aina ya mbegu uliyotumia na pia namna shamba
lako ulivyolihudumia.
Kwa maswali na
majibu kuhusu kilimo bora cha kisasa kitakachokutoa kwenye umaskini pamoja na
ufungaji wa hema(Green House) na Drop irrigation, unaweza ukawasiliana na
mtaalamu wetu wa kilimo Ndugu John Mabalaga kwa mawasiliano 0754 282 448.
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)