google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jul 11, 2020

Je, Unahitaji Kufanya Biashara Na Hujui Ni Biashara Ipi Ya Kufanya? Soma Hapa Kujua Ni Biashara Ipi Ya Kuifanya Sasa?

8 comments :
Wapo watu ambao mara nyingi hujiuliza ni biashara gani wafanye katika maisha yao ambayo itaweza kuwaingizia pesa nyingi ya kutosha. Ni wazo ambalo hutokea kutokana na pengine kuona kila biashara wanayoitazama  kwa wakati huo kama hailipi. Hali hiyo husababisha mkanganyiko mkubwa wa mawazo ambao husababisha wabaki njia panda.
Kama imeshawahi kukutokea hali kama hii kwa namna moja au nyingine makala hi ni muhimu sana kwako kuisoma. Kwa kusoma makala hii inakuonyesha kwa uwazi orodha za biashara ambazo unatakiwa uzifanye ukiwa katika mazingira uliyopo. Karibu kila biashara ipo hapo, kazi ni kwako kuchagua mojawapo unayoipenda na kuifanya, acha kulalamika tena kuwa huelewi nini cha kufanya.
Twende kwa pamoja kuzijua biashara hizo ambazo unauwezo wa kuzifanya na kukufikisha kwenye mafanikio makubwa:-
1. Kutengeneza na kuuza chaki.
Hii ni moja ya biashara nzuri unayoweza kuifanya na soko lake liko juu. Unaweza ukanunua mashine yako za kutengeneza chaki na kisha ukaanza kuzisambaza kwenye stationary  au mashuleni. Uzuri wake mashine hizi za kutengenezea chaki gharama yake pia sio kubwa sana ni ya kawaida tu ambayo hata wewe unaweza kuimudu. Hii inaweza ikawa ni sehemu mojawapo ya kuingizia kipato chako.

2. Kufungua duka la kuuza asali.
Uzuri wa bidhaa hii muda mwingi soko lake lipo juu. Ni biashara ambayo unaweza ukaifanya kwa kuagizia asali kutoka kwa wakulima kama nilivyo mimi na kisha kuanza kuiuza moja kwa moja katika vipimo vinavyotakiwa.
Kama huwezi kufungua duka hili unaweza ukafanya mbadala wake ukaenda kutengeneza mizinga wewe mwenyewe na kuwafuga. Pia hii ni biashara ambayo ni nzuri kwako kukuingizia kipato kikubwa kwa urahisi.
3. Kuanzisha biashara ya kuuza vyakula katika matamasha mbalimbali.
Hapa siyo lazima uwe na Hotel au Mgahawa ndiyo uanzishe biashara ya namna hii. Kikubwa unahakikisha unakuwa makini na sherehe katika eneo ulilopo. Kama ni kuweka mawakala watakao kusaidia kukujulisha kuwa eneo fulani kuna sherehe ya aina fulani na siku fulani itakuwa nzuri zaidi kwako kuchangamkia tenda hizo mapema.
4. Kujenga nyumba za kulala wageni.
Kama mtaji wako unaruhusu hii ni moja kati ya biashara nzuri kuifanya. Ni biashara ambayo hahitaji kukimbizana sana ukishamaliza kujenga, zaidi unatakiwa kuweka mfumo sahihi wa kusimamia na kuanza kuingiza pesa. Na kwa bahati nzuri kwa Tanzania yapo maeneo mengi ambayo yanauhitaji mkubwa wa huduma hii. Ni Biashara nzuri kuifanya hata kama umri umeenda, kwa sababu haihitaji mkimbizano mkubwa.
5. Kutengeneza matoroli/mikokoteni na kuikodisha.
Katika hili  hapa unatakiwa kutengeneza kwa idadi unayoitaka na unamwachia kijana ambaye anaikodisha huku ukiendelea na majukumu mengine. Unaweza ukaiona ni biashara ndogo lakini fuatilia kwa waliowekeza nguvu na mawazo yao hapo wakwambie kile wanachokipata utashangaa.
6. Kuazisha huduma ya AIRTEL MONEY, MPESA, TIGOPESA, EZYPESA.
Hakuna ubishi hii ni moja ya huduma ambayo imezagaa kila eneo na watu wengi wanaihitaji. Kikubwa ni juhudi yako na kuzingatia eneo uliloweka biashara yako liwe hasa la mzunguko mkubwa zaidi kukuwezesha kufanya biashara hii vizuri.
7.  Kupamba maharusi na kumbi za harusi/sherehe.
Pia unaweza ukajiingiza hapa na kushughulika na kupamba tu maharusi. Kama hujui sana ni kitu cha kujifunza pia, kisha unachangamkia sherehe zinazojitokeza mjini.
8. Kuanzisha kilimo cha kisasa.
Wengi wanaposikia kilimo kichwa kinakataa. Lakini ikiwa utawekeza kwenye kilimo cha kisasa na cha kitaalamu ambacho unategemea kumwagilia zaidi, uwe na uhakika unatoka. Yapo mazao mengi unaweza ukalima lakini mojawapo ni kitunguu. Inaweza ikawa ni njia rahisi ya kufikia mafanikio yako  kuliko unavyofikiri.
9. Mashine za kusaga na kukoboa nafaka.
Pia unaweza ukajitengenezea kipato chako na kuwa kikubwa na cha uhakika kwa kufunga mashine hizi. Kila siku watu wanahitaji kula hivyo ukifunga mashine hizi ni rahisi sana kupata wateja wa kuwauzia unga na kupata  faida. Na uzuri mahindi ya kusaga yanapatikana maeneo mengi kwa wingi kama kule Kibaigwa (Dodoma), Gairo(Morogoro), Kiteto(Manyara) na maeneo mengine mengi kama Iringa na mbeya.
10. Yadi kwa ajili ya kupaki magari.
Kitu unachotakiwa hapa ni kununua kiwanja na kukigeuza kuwa yadi ambapo magari yanakuwa yanapaki iwe kwa kulala au kwa muda. Kila gari linalokuwa linapaki linakuwa linatozwa kiasi fulani cha pesa ambacho kinakuwa ndiyo hiyo huduma unayoitoa.
Zipo aina nyingi sana za biashara ambazo unaweza ukazifanya na kukuingizia kipato. Katika Orodha ya kipande cha makala hii kinachoendelea zimebaki biashara zaidi 110 ambazo sijaziweka hapa kutokana na ufinyu wa nafasi. Kuzijua zinazoendelea na ufafanuzi wake  unaweza ukaniandikia email kwenda diramafanikio@gmail.com nitakutumia mara moja.
ILA KAMA YOTE HAYO UTASHINDWA KUPATA LA KUFANYA WEWE UTAKUWA UMESHAPOTEA, ENDELEA NA UTARATIBU WAKO WA KUILAUMU SERIKALI.
Tunakutakia ushindi katika safari yako ya mfanikio, ila kumbuka daima tupo pamoja mpako maisha yako yaimarike.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
0713 048 035,






8 comments :

  1. SAFI SANA NDUGU YANGU UMETUFUNGUA PAKUBWA,HIZ NI ELIMU MUHIMU SANA WAKATI MWINGINE BIASHARA KAMA HIZI WATU WENGI HUZIDHARAU KUMBE HUWA NA KIPATO KIZURI SANA.ASANTE

    ReplyDelete
  2. ok ni vzr,,kuhusu mpesa mtaji unaweza kuwa shillingi ngapi,,!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. kuusu mpesa sio biashara ambayo mtaji wake unaitaji uwe mdogo yani ukiwa na sehem yenye mzunguko mzuri kibiashara unatakiwa usipngue chini ya 1mil cash and flot 1mil apo kidogo utakua na msingi ambao unaweza ukaendana na mazingira uliopo

      Delete
  3. Mungu akubaliki hakika mitazamo mizuri yenye mashiko.....

    ReplyDelete
  4. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  5. kwakweli mtu ukizingatia kwenye hii blog asee mtu unaweza ukafanya mambo makubwa sana sema kinachotuponza watu wengi hatuna subra yan tunapenda kufanyaj mambo bila kuwaza malengo yetu ni yapi ndo tunapofel apo tu na umu 65% biashara zilizotajwa so za mtaji mdogo yani mtu umekosa kabisa unatakiwa uwe na ata 1mil apo utakua umesogea kwenye lengo sio mm ndo nasema ivo ila kutokana na maelezo ya blog ila tunashukur kwa kutufumbua manaake mtu unaweza ukawa na mtaji ila kila unachojalibu kutaka kufanya unajiona unaenda kufeli ko kusoma uku kunatusaidia sana nn tufanye🙏

    ReplyDelete
  6. Asante mkuu nimepata elimu moja makini Sana

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.