google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Apr 13, 2016

Tabia Zinazokuzuia Ushindwe Kupata Pesa Kwa Kiasi Kikubwa.

No comments :
Katika safari ya maisha ya mafanikio, kitendo cha kutengeneza pesa nyingi ni kitu au hatua ambayo kila mtu anataka aifikie. Bila shaka utakubaliana nami hakuna mtu ambaye haitaki pesa, kila mtu kuamka hadi kulala kwake shughuli zake nyingi karibu zote zinahusisha juu ya kupata pesa. Hiyo yote inaonyesha pesa inahitajika kwa namna yoyote ile kwa wingi na tena kwa kila mtu.
Lakini hata hivyo pamoja na kiu yote hiyo ya kutaka kuwa na mafanikio makubwa ya kifedha wengi wetu bado huwa hawafanikiwi. Unajua ni kwa nini? Ngoja nikwambie. Kwa kawaida huwa yapo mambo mengi yanayomfanya mtu huyu apate pesa nyingi na mwingine akose. Lakini leo hii nataka nikupe siri na kukwambia jambo moja tu linakufanya ushindwe kutengeneza pesa ya kutosha. Jambo hilo si lingine ni tabia.
Ndio. Nimesema ni tabia. Zipo tabia ambazo ukiwa nazo ni lazima zitakufanya ushindwe kutengeneza pesa kwa kiasi kikubwa. Ni tabia ambazo wengi tunazo na ni kweli zinaturudisha nyuma kwa kiasi kikubwa. Kwa kusoma makala haya, utajifunza tabia hizo ambazo zimekuwa kama kizuizi kwako na kukukufanya ushindwe kupata pesa kwa kiasi kikubwa. Karibu na twende pamoja kujifunza.
1. Tabia ya kushindwa kuifanya pesa ikuzalishie.
Kati ya kitu ambacho kinakuzuia ushindwe kutengeneza pesa nyingi, ni kule kushindwa  kuifanya pesa unayoipata ikuzalishie zaidi. Kwa mfano kama unapata shilingi laki tano kwa mwezi je, unaifanya vipi hiyo pesa ikaongezeka zaidi ya hapo? Kama unashindwa kuifanya hiyo pesa ikuzalishie zaidi, basi elewa hiyo ni moja ya tabia inayokufanya ushindwe kupata pesa kwa kiasi kikubwa.
Kitu cha kufanya kama hilo ndilo linalokuzuia, tafuta ni wapi au eneo lipi unaweza kuwekeza kwa pesa unayoipata. Ukishapata kitu hicho acha kupoteza muda kwa kujiuliza uliza na anza mara moja kutengeneza pesa kwa kuiweka kwenye uwekezaji. Kwa kujijengea tabia hiyo kutakufanya uzidi kutengeneza pesa za ziada. Jambo la msingi na la kukumbuka ifanye pesa yako ikuzalishie zaidi hata kama ni kiasi kidogo unapata

TOA THAMANI UTENGENEZE PESA ZA KUTOSHA.
2. Tabia ya kushindwa kutoa thamani.
Ni rahisi kushindwa kupata pesa kwa kiasi kikubwa kama pia utashindwa kutoa thamani kwa kile unachokitaka. Mara nyingi mafanikio yoyote yanaanza kwa kutoa thamani uliyonayo ndani mwako kwanza. Kwa mfano hapo ulipo kuna kiasi fulani cha pesa unachokipata kwa mwezi. Kiasi hicho cha pesa hakiji hivi hivi bali kuna thamani au kitu unachokitoa ndani mwako kinachopelekea upate pesa hiyo.
Kama tafsiri yake  iko hivyo, hiyo inamaanisha kwamba kama unashindwa kutoa thamani kubwa maana yake utashindwa kutengeneza pesa nyingi. Wengi  kutokana na kuishi kwa mazoea wamejikuta wakiwa ni watu wa kuishi maisha yale yale bila kutoa thamani kubwa sana. Kwa kufanya hivyo hujikuta ni watu wa kushindwa kutengeneza pesa nyingi karibu muda wote wa maisha yao.
3.Tabia ya kufanya mambo kwa ukawaida sana.
Sumu kubwa ya kufikia mafanikio makubwa na kushindwa kutengeneza pesa kwa kiasi kikubwa ni kufanya kazi kwa ukawaida sana, Watu wengi wana mazoea ya kufanya kazi kwa viwango vya kawaida. Ili uweze kufanikiwa na kutengeeza pesa nyingi maishani mwako, jifunze kufanya kazi kwa bidii zote bila kuchoka. Kwa kadri utakavyozidi kuongeza juhudi katika kafanya kazi kwa bidii itakufanya uzidi kutengeneza mpato makubwa sana.
Kama unafikiria natania, angalia watu ambao maisha yao yote wameyaweka kwenye kujituma huku wakiwa wamekubali kujifunza. Watu hawa mara nyingi wanatengeneza pesa nyingi sana kutokana na kile wanachokifanya kwa juhudi zote. Kwa hiyo  moja ya kitu kinachokufanya ushindwe  kutengeneza pesa nyingi sio mkosi au laana kama unavyofikiri bali ni kufanya kazi kwako kwa ukawaida. Jitume mara kumi ya hapo tuone ni nini kitakutokea kwenye maisha yako.
4. Tabia ya kuridhika mapema.
Kuna watu wana tabia hasa pale wanapopata mafanikio madogo tu, huwa ni watu wa kuridhika sana. Huwa ni watu wa kujiona wamefika na hata zile juhudi kubwa walizokuwa nazo mwanzo zinakuwa zinapotea kidogo kidogo kwa sababu ya mafanikio hayo. Unapokuwa na na tabia kama hii tambua kabisa hicho ni chanzo kikubwa sana kinachokufanya  ushindwe kutengeneza pesa nyingi.
Kwa mfano jaribu kuangalia baadhi ya wasomi wetu, akijenga nyumba na kununua gari kwao ndio basi. Maisha huwa kama yameishia hapo na hakuna juhudi kubwa tena wanayokuwa wanaifanya. Kitu cha kuelewa mafanikio sio nyumba wala gari peke yae. Tunatakiwa kufanya mambo makubwa zaidi ya hapo. Kama mafanikio ni nyumba tu sasa jambo la kujiuliza ni nani ayeishi kwenye tundu kama ndege, bila shaka hakuna. Hivyo acha kuridhika, ili utengeneze pesa za kutosha.
Kimsingi zipo tabia nyingi ambazo zinaweza zikakuzuia wewe ukashindwa kupata pesa kwa kiasi kikubwa na kukufanya usifikie mafanikio mkubwa. Lakini kwa kupitia makala haya hizo ni baadhi tu ya tabia hizo.
Ansante kwa kuwa msomaji mzuri wa DIRA YA MAFANIKIO lakini washirikishe wengine waendelee kujifunza kila siku kupitia mtandao huu.
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu;- 0713 04 80 35,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.