google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jun 3, 2016

Kama Utakwepa Kulipa Gharama Hizi, Huwezi Kufanikiwa.

No comments :
Hakuna kitu chochote ambacho unaweza ukakipata katika hii dunia pasipo kulipia gharama zake. Kila kitu ni lazima ulipie gharama za aina fulani ili ukipate. Asikudangaye mtu kwamba eti yapo mafanikio ya bure au ya kirahisi rahisi. Kila mafanikio yana gharama zake ambazo unatakiwa kuzilipia  kwanza ili kuyapata.
Kwa wale wanaokwepa kulipia gharama za mafanikio, ni wazi huwa hawafanikiwi. Matokeo yake hujikuta ni watu wa kulalamika na kulaumu kila hali. Ni gharama hizi ndizo ambazo tunakwenda kuziongelea katika makala haya. Ikiwa akwepa kulipia gharama hizi kwa namna moja au nyingine hakika, hutaweza kufanikiwa. Karibu sana na twende pamoja kujifunza ili kujua gharama hizo.
1. Kufanya kazi kwa bidii sana.
Kati ya kitu ambacho hutakiwi kukwepa kama unataka kufanikiwa ni kufanya kazi kwa bidii. Inatakiwa uweke nguvu zako zote kwa kile unachokifanya na si kufanya kwa mkono mlegevu. Ikiwa utafanya kazi kwa bidii hakuna kitakachokuzuia tena kufanikiwa.
Ili kulielewa hili vizuri, jaribu kuwaangalia watu wenye mafanikio jinsi wanavyofanya kazi. Tunaambiwa muda mwingine wanafanya kazi kwa muda hadi wa saa kumi na mbili. Tambua kama unataka kufika viwango vya juu vya mafanikio kufanya kazi kwa bidii ni gharama ambayo lazima uilipe.

Fany kazi kwa bidii zote, utafanikiwa.
2. Kutoa thamani.
Si kufanya kazi kwa bidii tu, ndipo kutakapokufanya wewe ufanikiwe, hapana. Unaweza ukafanya kazi kwa bidii sana lakini usifanikiwe ikiwa utafanya kazi zako bila kutoa thamani inayotakiwa. Ni lazima ufanya kazi zako huku ukitia thamani ya viwango vya juu, thamani unayotoa ndio inayokupa pesa.
Kwa mfano unaweza ukawa muumbaji, lakini ikiwa nyimbo zako utakuwa unatoa bila kuwa na thamani kubwa kwa wasikilizaji wako hazitasilikizwa na pia hutafanikiwa. Kwa hiyo, ni lazima kwako ujitoe kufanya kila linalowezekana kuhakikisha unatoa thamani kwenye nyimbo zako na hivyo ndivyo unakuwa umelipia gharama ya thamani.
3. Kubali kukosolewa.
Mbali na kufanya kazi kwa bidii na kutoa thamani, gharama nyingine ambayo unatakiwa ulipie ili ufanikiwe ni kukubali kukosolewa. Wengi huwa hawako tayari kukubali wanapokosolewa kwa wale wanayoyafanya. Huwa ni watu wakutaka kusifiwa sana.
Kwa kuwa unataka mafanikio, ikitokea watu wakawa wanakukosoa acha kuumia sana. Tumia kukosolewa huko kama kujirekebisha na kisha kuendelea kusonga mbele. Vinginevyo ukishindwa kulipa gharama ya kukosolewa ni rahisi sana kuacha kile unachokifanya kwa sabab ya hofu ya kukosolewa.
Kama nilivyoanza kusema mwanzoni mwa makala haya, ili ufankiwe ni lazima ulipie gharama, jiulize binafsi upo tayari kulipia gharama ili kufikia mafanikio yako. lkiwa haupo tayari itakuwa ni vigumu sana kufanikiwa kwako.
Tafakari juu ya hili na kisha chukua hatua za kubadili maisha yako kwa haraka sana.
DIRAYA MAFANIKIO inakutakia kila la kheri katika safari ya mafanikio. Na endelea kujifunza bila kuchoka, ukifanya hili utababadili sana maisha yako.

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 04 80 35,
Email; dirayamafanikio@gmail.com

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.