Sep 20, 2016
Faida Kubwa Za Kujijengea Mtazamo Chanya.
Kuna jambo kubwa sana ambalo linaweza
kubadili maisha yako ndani ya muda mfupi, ambalo siku ya leo ni vyema
kulifahamu, na si kulifahamu tu bali kuamua kulichukua jambo hili na kulifanya
libadili maisha na jambo lenyewe si jingine bali ni mtazamo ulionao.
Mtazamo ni vile ambavyo unaamini
huenda ikawa ni katika fikra chanya au fikra hasi. Lakini katika makala haya
nitazungumzia umuhimu wa kuwa na mtazamo chanya, kwani mitazamo ya watu ndio
ambayo humueleza kwa undani zaidi ni kwa njisi gani mtu alivyo kutokana na vitu
ambavyo anavyovifanya na asivyovifanya.
Na jambo hilo huleta tofauti uliyopo
kati ya walinacho na wasionacho, na tofauti hiyo ni kwamba waliofanikiwa wao
wanaamini ya kwamba katika dunia hii hakuna kisichowezekana ila watu ambao hawajafanikiwa
wao huamini ya kwamba mambo mengine hayawezekani hii ni kutokana wao
hukata tamaa mapema zaidi kabla ya kuanza kufanya, hali hii hutokea kwa sababu
watu wengi ambao maisha yao duni huishi kwa kuogopa sana wakati ujao.
Jenga mtazamo chanya, ukusaidie. |
Pia akili za mwanadamu zimetawaliwa
kwa kiwango kikubwa na vitu ambavyo havionekani, hapa ndipo lile somo la kujipa
majibu hasi linapofanya kazi, kwa vitu ambavyo anaviwaza ambavyo kimsingi bado
havijawekwa katika utekelezaji.
Kwa mfano unakuta mtu ana mawazo
mengi ambayo ukiyatazama kwa "jicho la tofauti" mawazo hayo yatawezwa
kubadilishwa na kuwa katika matendo yana uwezo mkubwa sana wa kubadilisha
maisha ya mhusika huyo kwa asilimia mia moja, ila changamoto kubwa pindi mtu
awazapo huanza kuja na vikwazo ambavyo kimsingi huwa na vitu ambavyo havimpi
nguvu ya kuthubutu kutenda jambo hilo.
Hii huwa ni ishara mawazo yetu huwa
ni chanya mara nyingi lakini suala zima la utekelezaji wa suala hilo huwa ni
kikwazo kikubwa, lakini nikwambie neno moja ya kwamba kuanza sasa unahitaji
ubongo wa ziada.
Unaweza ukajiuliza ubongo wa ziada
labda ni kuwa na ubongo mwingine, la hasha sina maana hiyo ila ukweli ni kwamba
uanze kufikiria katika akili nyingine ambayo itakufanya uwe mpya, katika fikra
mpya hususani suala zima la kuwa na mtazamo chanya.
Inawezekana ukajiuliza unawezaje kuwa
mtazamo chanya?
Suala zima kuwa mtazamo chanya huwa
linatokana na kujiuliza katika mambo ambayo unayofanya, je mambo hayo yana
matokeo gani katika maisha yako na watu wengine?
Watu ambao wanakuzungua huwa
wanatazamo gani juu yako? Na mara zote ikumbukwe ya kwamba maisha yako
yanatazamwa kwa asilimia kubwa na watu wengine, watu wanaokuzunguka
wakikutazama katika jicho chanya hata kile kitu ambacho unakifanya kinaweza
katika kuwa bora zaidi.
Ifike pahala jamii ambayo inakutazama
wakufikirie kwamba ni mtu chanya, kufanya hivi kutakufanya uweze kujitangaza
jina na kujiongezea thamani.
Amua sasa kutenga muda wa kujiuliza
mambo ya msingi ambayo yatakusaidia kuwa na mtazamo chanya kwa kila jambo
amabalo unakiwaza au ambalo unalitenda. Pia ikumbukwe ya kwamba ni vyema
ukaamua kubadili maisha yako kwa kuwa na mtazamo sahihi.
Afisa mipango Benson Chonya.
0757909942
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.