Sep 8, 2016
Mambo Ya Msingi Ya Kuzingatia Kabla Ya Kuacha Kazi.
Leo hii karibu kila mtu aliyeajiriwa
ukimuuliza je, unafurahia maisha ya kuajiriwa? Atakwambia hapana ila natamani
kujiajiri, na endapo utaendelea kumuuliza ni kwa nini unatamani kujiajiri?
Utamsikia anasema nataka kuwa huru na muda na pia nahitaji uhuru wa kipesa.
Majibu hayo kwa mtazamo wa wengi ni
sawa, ila kuna kitu ambacho ni vyema ukakijua kabla ya kuamua kuacha kazi na
kwenda kujiajiri.
Kujiajiri kuna hitaji ujasiri wa hali
ya juu sana maana kuna changamoto zaidi ya kuajiriwa. Hivyo nakusihi
ufikirie kwa umakini sana suala zima la kuacha kazi kabla kwenda
kujiajiri.
Na endapo utaamua kuacha kazi ya
kuajiriwa bila ya kufikiria ipo siku utakuja kujutia uamuzi wako. Hivyo ni
vyema ukafikiria mara mbili kabla ya kufanya maamuzi magumu.
Mambo ya msingi ya kuzingatia kabla
ya kuacha kazi.
1. Kuwa na nidhamu ya muda.
Kwa kuwa kwa sasa bado umeajiriwa, hivyo
huna jukumu la kufanya maamuzi ya matumizi ya muda, Bali unafanya kazi kutokana
na muda ambao muajiri wako ameamua yeye kukupangia kuweza kufanya kazi.
Na kwa kuwa umezoea kufanya kazi
kutokana na amri ya mwajiri wako, hata pale ambapo utaamua kuacha kazi fahamu
fika ya kwamba suala la kuwa na nidhamu ya muda kwako ni suala gumu, hivyo
unatakiwa kufanya jitihada zako binafsi kadri iwezekanavyo hasa katika matumizi
sahihi ya kufanya kazi hasa suala zima la uzalishaji wa mali au huduma.
Nazungumza suala zima la matumizi ya
muda kwani hapa ndipo ambapo tunapata makundi mawili ya watu waliofanikiwa na
wasiofanikiwa. Hivyo ni jambo jema kuhakikisha unazingatia matumizi sahihi ya
muda ili pindi utakapoacha kazi wewe ndiye ambaye utakuwa na jukumu la kupanga
muda wa kufanya kazi na ni muda gani utakuwa ni wa kupumzika. Pia ikiwezekana ongeza
matumizi sahihi ya muda mara mbili zaidi ya ulivyokuwa umeajiriwa.
2. Kutokuahirisha kufanya mambo ya msingi.
Utakuwa shahidi ya kwamba wakati
umeajiriwa suala zima la uahirishaji wa kufanya mambo ya msingi lilikuwa ni
suala gumu sana labda awe ameamua mwajiri wako. Kama ndivyo hivyo basi pale
ambapo utakuwa umeamua mwenyewe kuacha kazi na kuamua kufanya kazi mwenyewe
hivyo huna budi kuhakikisha ya kwamba suala zima la uhairishaji mambo linakuwa
ni suala ambalo halina nafasi katika maisha yako.
Ukiwa ni mtu wa kufanya kazi kwa
kuamua kutenda bila kuahiirisha vitu vya msingi ama hakika utafika kilele cha mafanikio
yako ndani ya muda mfupi. Ni vyema kulizingatia hili, kwani hili ndilo ambalo
limewafanya watu wengi ambao waliacha kazi kuwa na maisha duni zaidi, kwani
wengi wao walikuwa ni waahirishaji wazuri wa vitu vya msingi.
Endelea kutembelea dirayamafanaikio.blogspot.com
kila siku kwa ajili ya kujifunza na kuongeza maarifa yako.
Ndimi; Afisa mipango Benson Chonya.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.