Sep 29, 2016
Msingi Imara Wa Mafanikio Yako.
Ipo faida kubwa maishani mwako endapo
utaamua leo kuchukua hatua mathubuti ya kutaka kufanikiwa. Tupo hivi tulivyo
kwa sababu hututaki kuchua hatua sitahiki za kiutendaji kwa yale yalipo akilini
mwetu na kuyaweka katika matendo. Watu wana maarifa lakini suala la kuyaweka
maarifa hayo katika matendo.
Kuwepo kwa hali hii ndiyo ambayo inasababisha
kuweza kuyatamani mafanikio na si kuyaishi. Hata hivyo moja ya siri nzito ya
mafanikio yako husukumwa na kiu kubwa sana aliyonayo mtu kutaka
kufanikiwa, lakini kiu hiyohiyo huendana na msukumo na nia thabiti ya kuyaweka
yale unayoyajua katika matendo.
Nasisitiza hili kwa sababu moja kubwa
watu wengi wanaishi maisha ya kawaida kwa sababu wameamua hali hiyo kutokea,
lakini ili kuondokana na hali hii huna budi leo hii kuacha kuishi kikawaida kwa
sababu wewe sio mtu wa kawaida.
Huenda ukawa unajiona wewe ni mnyonge
katika maisha kwa sababu labda uliwahi kufeli kwenye jambo fulani ambalo
ulitegemea ya kwamba litakupa matokeo chanya lakini matokeo yake yakawa kinyume
chake. Lakini Amini usiamini ila ukweli ni kwamba watu wengi ambao wamefanikiwa
wao walikuwa ni watu ambao hawakutaka kuishi kikawaida.
Hivyo hajalishi umefeli kwa kiwango
gani ila lakini iambie nafsi yako ya kwamba wewe si mtu wa kukata tamaa bali ni
mtu wa kusonga mbele kivitendo zaidi.
Tengeneza msingi bora wa mafanikio yako kwa kuamua kutokuwa wa kawaida. |
Kuishi kikawaida ni sumu sana katika
maisha yako. Wapo baadhi ya watu wamefeli kimaisha kwa sababu walikatishwa
tamaa na watu wengine, huenda ukawa ni wewe ambaye unasoma makala haya ila
ukweli ni kwamba maisha halisi ya kwako unayo wewe na si mtu mwingine
haijalishi watasema nini ? Ila we songa mbele kivitendo ila pale unapofanikiwa
wabaki midomo wazi. Maana dunia hii imejaa wakatishaji tamaa.
Na kila mara tuzidi kuukumbuka ule
usemi mtamu ambao unasema usiwambie watu ndoto yako, bali waosheshe ndoto hiyo
kwa vitendo zaidi. Kwani kuwashirikisha watu juu ya ndoto yako, wapo baadhi ya
watu endapo utawaambia jambo lako asilimia kubwa watakwambia haiwezekani.
Pia kwa kuwa maneno yana nguvu sana
utajikuta kweli umeshindwa kuifanya hiyo ndoto yako . Simama imara kila mara
kwa sababu wewe ni mshindi katika ulimwengu huu.
Kabla sijaweka nukta siku ya leo,
nikandamizie maneno haya ya kwamba ili uweze kushinda vita vya umaskini,
hautitaji uongozi imara kama ambavyo tumekalilishwa mashuleni, ila unahitaji
kuwa bora kwa jambo lolote unalolifanya.
Kama ni biashara hakikisha unazalisha
bidhaa yenye ubora kila mara, ukifanya hivi ni chachu kubwa sana ambayo
itafanya wateja waongezeke wenyewe na si kuwa na kiongozi bora katika eneo lako
unaloishi.
Nasema masuala haya ya uongozi
kwa sababu idadi kubwa wanahusisha masuala ya maisha yao kuwa magumu na
masuala mazima ya uongozi, lakini ukweli ni kwamba ukifanya uchunguzi wa
kutosha juu ya maisha yako utagundua ni nini ambacho nasema.
Maisha yako kuwa magumu usiyahusishe
na masuala ya uongozi, bali tafakari katika kila kona ambayo unafanya kazi kwa
kufikiri ni namna gani unaweza kuwa bora? Ukipata majawabu sahihi ya jinsi ya
wewe kuwa bora hiyo siri kubwa ambayo ipo kwako ya wewe kufanikiwa.
Kama ni mwanafunzi fikiri jinsi
ambavyo utakuwa bora katika taaluma yako, kama wewe ni msanii katika eneo
lolote lile fikiri ambavyo utaweza kufanikiwa na sio kushirikisha imani potofu
kutofanikiwa kwako na imani ambazo sio za msingi.
Dunia ni pana ila kwa maneno machache
sana, kwa leo niishie hapo tukutane mara nyingine ambapo tutazidi kuelimishana
masuala mazima ya mafanikio. Hivyo nikunong'oneze badili mfumo wa maisha yako
kwa kuwa na fikra sahihi.
Endelea kujifunza kupitia
dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama makala hii
imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili
uweze kujifunza. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO
YANGU, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI
KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Na; Afisa mipango Benson Chonya,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.