Sep 26, 2016
Mambo Muhimu Ya Kuzingatia, Ili Kujenga Hamasa Ya Kudumu.
Kuna
wakati katika maisha unaweza ukajikuta una wazo la kufanya biashara au una wazo
la kusoma kitabu au una wazo la kufanya kitu fulani kwa hamasa kubwa sana.
Lakini
kitu cha kushangaza pale tu unapoanza kufanya jambo hilo, hamasa hiyo huanza
kupungua kidogo kidogo na wakati mwingine hujikuta imeisha kabisa na wewe kujikuta
huwezi tena kuendelea.
Wakati
huo huo unakuwa unashangaa na kujiuliza sana, hamasa yote kubwa uliyokuwa nayo
imekwenda wapi? Hapa kuna wakati unakuwa huelewi kabisa ni nini kilichopoteza
hiyo hamasa?
Pia
hata hivyo, unakuwa tena unashangaa kuwaona watu wengine wakifanya kitu hicho
hicho, ambacho wewe umekishindwa. Tena unakuwa unajiuiza hamasa ya wao kufanya
inatoka kwao wapi? Wakati wewe umeshindwa?
Kumbe,
kitu usichokijua ni kwamba hamasa ni kitu ambacho huzaliwi nacho. Hakuna mtu
ambaye anazaliwa akiwa na hamasa ya kufanya kila siku zaidi ya wewe kuamua
kuitengeneza.
Inapofika
mahali unajihisi kabisa umekosa hamasa, tambua kabisa ipo namna ambayo unaweza
ukaiongeza hamasa hiyo. Lakini, kuongeza huko au kuchochea huko hamasa hakuji
hivi hivi tu, mpaka uzingatie mambo muhimu ya kujenga hamasa.
Yafuatayo
Ni Mambo Muhimu Ya Kuzingatia, Ili Kujenga Hamasa Ya Kudumu.
1. Anza kwa kidogo.
Kwa chochote kile unachotaka kukifanya hata
kama unahamasa nacho kubwa vipi, anza kidogo. Hiyo itakusaidia kutokuta tamaa
au kukupunguza hamasa, endapo itatokea umepata matokeo ya tofauti.
Kwa jinsi unavyoanza kwa kidogo inakuwa sio
rahisi kwako, kukosa hamasa kwa urahisi. Inatokea hivyo kwa sababu kila siku
unavyofanya kwa kidogo, unakuwa unajitengenezea nguvu ya mwendelezo wa kusonga
mbele.
Tafuta sababu ya kufanya. |
2. Fanya jambo hilo kwa sababu.
Chochote unachokifanya ili kikujengee hamasa
ya kudumu ni lazima uwe na sababu ya kufanya. Kosa wanalofanya watu wengi,
sababu zinakuwa sio nzito sana au hazijitoshelezi.
Je, unaweza ukajiuliza binafsi, hilo jambo
unalolifanya sasa, ni sababu ipi inayokuongoza hadi ukalifanya? Je, ni kwa sababu
ya pesa au kwa sababu unalipenda au kwa sababu unataka kusaidia jamii?
Ukishajua sababu inakuwa sio rahisi kwako kukata tamaa, hata pale yanapotokea mazingira ya kukatisha tamaa.
Ukishajua sababu inakuwa sio rahisi kwako kukata tamaa, hata pale yanapotokea mazingira ya kukatisha tamaa.
3. Kuwa na maono.
Wakati wengi wetu hamasa inapungua kwa sababu
ya kushindwa kuwa na maono maalumu ya kule tunakokwenda na kile tunachokifanya.
Lakini ikiwa maono yako wazi, ni rahisi kudumisha hamasa yako wakati wote.
Jaribu kujiuliza kama hicho unachokifanya
kitakupa faida kubwa sana na pesa nyingi huko unakokwenda, je unaweza ukakiacha
kwa urahisi? Ukiwa na picha ya namna hiyo itakusaidia sana wakati wote
kujijengea hamasa ya kudumu maishani mwako.
4. Tengeneza tabia ya mwendelezo.
Kuna siku tunajikuta kweli tumechoka na hatuwezi kufanya
lile jambo tunalolifanya na akili inakuwa inatuambia tulia, utafanya kesho. Ukikubali
kuisikiliza hiyo sauti, utapotea.
Kuwa na tabia ya kukifanya kile unachokifanya
kila siku hata kama ni kwa dakika kumi tu inatosha. Haijalishi umejisikia au
haujisikii wewe fanya. Tengeneza
mwendelezo wa kufanya kila siku(Consintence). Ikiwa utafanya hata pale ambapo
hujisikii kufanya ni lazima utajenga hamasa yako sana.
5. Tumia kushindwa kama chanzo cha hamasa kubwa.
Hata inapotokea pale unaona kama umeshindwa,
tumia kushindwa huko kama sababu kubwa ya kuelekea kwenye mafanikio yako.
hakuna mtu ambaye hashindwi kwenye safari ya mafanikio.
Achana na habari ya kulalamika pale
unashindwa zaidi ya kujifunza. Ukishalijua hilo, jifunze sana kutokana na
makosa yako na chukua hatua ya kuweza kuendelea mbele hatua kwa hatua.
Kwa kuzingatia mambo hayo machache, hivyo
ndivyo unavyoweza ukajikuta umejenga hamasa ya kudumu wakati wote katika maisha
yako.
Endelea
kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama
makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la
Whats App ili uweze kujifunza. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO YANGU, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA
KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni
wako rafiki,
IMANI
NGWANGWALU,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.