Sep 16, 2016
Tabia Zinazoathiri Maisha Yako Ya Kimafanikio.
Tafiti ambazo zimewahi kufanywa na wanasoikolojia mbalimbali
kuhusu maisha ya mwanadamu na mazingira yake hususani suala zima la mafanikio,
zilitoa majibu ya kwamba maisha ya mwanadamu yanaathiriwa kwa kiwango kikubwa
na vitu vikubwa viwili ambavyo ni;
Jambo la kwanza ni kuishi kwa kukariri.
Suala hili ndilo ambalo limekuwa limeathiri maisha ya wengi kwa
asilimia kubwa sana. Watu wanashindwa kuishi kulingana na jinsi ambavyo dunia
inakwenda kasi.
Hebu tunawatazame wafanyabiashara wangapi ambao leo hii ambao
walianza kufanya biashara tangu muda mrefu kabla ya kukua kwa teknolojia
hususani masuala ya mitandao ya kijamii ambao leo hii wanatumia mitandao hiyo
ya kijamii katika kuzitangaza bidhaa au huduma zao?
Acha kuishi kwa kukariri |
Kimsingi ukifanya tathimini utagundua ni wachache sana. Unajua
ni kwanini wapo wachache? kwa sababu wameshazoea na kuishi maisha ya kukariri
huku wakiamini ya kwamba kutumia mitandao ya kijamii ni suala gumu kwao.
Hii ni ishara ya kwamba imani waliyonayo ni ngumu sana ambayo
hawawezi kubadilika hata kupelekea wao kutokuamini ya kwamba wanaweza
kujitangaza kupitia mitandao ya kijamii. Imani waliyonayo ni kwamba kutumia
mitandao ya kijamii ni suala la kupoteza muda.
Lakini ukweli haupo hivyo ndugu yangu mwenye tabia kama hizo,
tambua na elewa ya kwamba kuna watu ambao inabidi wakutambue kwa shughuli
ambayo unaifanya ambao kimsingi wanaishi mbali na sehemu ulipo.
Ewe mfanyabiashara acha kuishi kimazoea na kuamini ya kwamba
mahali ulipo sasa panatosha, ila amini ya kwamba ipo haja leo ya kujua ya
kwamba wapo baadhi ya wadau wanapenda kujua hicho ambacho unakifanya.
Jambo la Pili ambalo linaathiri Maisha ya wengi ni kuishi
kimazoea.
Kuishi kimazoea ndiko kunakotufanya tuishi kwa manung'uniko na
masikitiko hasa katika maisha haya ya kila siku. Hebu tazama kwa mfano utawala
huu wa awamu ya tano jinsi ambavyo unafanya kazi kila mmoja kwa nafsi yake
moyoni ana yake ya kusema, unajua ni kwanini kwa sababu watu wengi tulikwisha
kuzoea kuishi maisha ya kimazoea sana, hivyo tunajikuta kwa asilimia kubwa
tunashindwa kuendana na kasi hiyo na tunabaki tunalalamika kwa sababu
tulishazoea kuishi kimazoea.
Kuishi kimazoea ni kubaya sana mpenzi msomaji wa makala haya kwa
sababu pindi changamoto yeyote ijitokezapo kwetu huwa ni kikwazo kikubwa cha
kuweza kulifikia lengo. Leo hii ukimkuta mtu ambaye anafanya jambo fulani na
ukamshauri afanye jambo jingine atakataa, unajua ni kwanini atakataa? atakataa
kwa sababu amezoea kufanya jambo lake la awali hivyo kubadili kufanya jambo
jingine kwake hutengeneza hofu ya kushindwa.
Ndugu yangu ambaye kwa hali yeyote ile unataka kufanikiwa, na si
kufanikiwa tu, bali kufanya mafanikio yako yamguse kila mmoja wetu kwa namna
moja ama nyingine hakikisha ya kwamba usiishi katika misingi ambayo ni ya
kukariri au kuishi katika mtazamo wa kimazoea, kwani kufanya hivi ni kujiua
mwenyewe.
Nakusihi tena kwa kukumbusha ujio wako hapa dunia si kwa bahati
mbaya ila ni kwa kusudio maalum amini ya kwamba wewe ni zaidi ya matajiri
wakubwa waliopo sasa, pia tumia muda mwingi kumshukuru Mungu kwa kukupa hekima
na akili ya kuweza kufikiri, pia muombe akupe ujasiri wa kuweza kutenda mambo
kwa fikra na mitazamo chanya.
Endelea kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com
kila siku. Kama makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu
kwenye kundi la Whats App ili uweze kujifunza. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO YANGU, kisha ikifutia na jina
lako kwenda 0713 048035 ili
uanganishwe.
TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ndimi: Afisa mipango Benson Chonya
0757909942
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.