Sep 22, 2016
Jinsi Ya Kukabiliana Na Changamoto Ili Kupata Mafanikio.
Kila mmoja anahitaji mafanikio makubwa kwa kile anachokifanya
siku zote, japo tatizo huwa ni namna ya kukabiliana na changamoto zinazomsonga
ili asifike malengo.
Kuna wakati mwingine tunajikuta tunakata tamaa baada ya kuona
baadhi ya changamoto zinatokea na kuzuia mafanikio ambayo tumejipangia.
Changamoto hizi zimekuwa zikijitokeza katika biashara, elimu, kazini hata mara
nyingine kufiwa na mtu ambaye ulikuwa una mtegemea kwa namna moja ama nyingine
pamoja na changamoto nyingine nyingi.
Wakati mwingine changamoto zikitokea, wengi hukata tamaa na muda
mwingine kujiona hufai kuendelea kuishi. Wapo wanaofikia hatua ya kukufuru kwa
kutoa kauli kama vile Mungu anapendelea, dunia haina usawa na maneno mengine
mengi yanayofanana na hayo.
Lakini wasichokielewa watu ni kwamba changamoto ni njia ya
kufikia mafanikio tunayoyahitaji. Pia changamoto huja ili kupima imani na uwezo
wako kama kweli unaweza kupambana vitani.
Kabiliana na changamoto mpaka uzishinde. |
Zifuatazo ni baadhi ya njia ya jinsi ya kukabiliana na
changamoto katika maisha ya kila Siku;
Kwanza, zikubali changamoto; Kama nilivyoeleza hapo awali,
changamoto ni lazima zitokee katika safari yako ya mafanikio, hivyo hakikisha
na kisha utafute mbinu zakuweza kupambana nazo.
Unaweza kuanzisha biashara, lakini katikati ya safari ukakimbiwa
na wateja, jambo la msingi ni kufanya uchunguzi ni nini kimesababisha hali
hiyo, ili uweze kuchukua hatua badala ya kulalamika na kuwanyoshea vidole
wengine kwa kuona wao ndio chanzo.
Epuka kukimbilia kwenye imani za kishirikina au mitazamo potofu
kama vile chuma ulete, nguvu za giza na mengineyo mengi kwani kufanya kinyume
chake kwa kuamini imani hizo si kutatua tatizo bali ni kuliongeza tatizo.
Pili, tafuta washauri. Nafahamu ya kwamba baadhi yetu tuna watu
wa karibu ambao huwa tunawaeleza shida zetu. Mfano wazazi, ndugu, marafiki na
wengineo.
Pia unaweza kuwatumia viongozi wa dini kwa jambo linao kutatiza,
kwani ni watu ambao wana nguvu sana katika jamii hususani suala zima la masuala
ya ushauri hasa katika mambo yanayotutiza katika kufikia malengo yetu. Pia
unaweza kujifunza kupitia mafunzo mbalimbali kama vile semina kwani kufanya
hivyo utaweza kupata majibu ya changamoto zinazokukabili.
Vile vile katika utatuzi wa changamoto, watu wengi huwa
tunakosea sana. Huwa tunaanza kuangalia matokeo ya jambo, badala ya kuangalia
vyanzo ya matokeo hayo.
Nitaomba kukupa ufafanunuzi wa nukta hii kwa kuangalia mfano
mdogo wa ugonjwa wa mlipuko maarafu kama kipindupindu ambao umekuwa ukizuka
sana maeneo kadha wa kadha ikiwepo na jiji la Dar-es-salaam, ambapo kila
kipindi cha muda fulani huzuka na kuwaathiri watu wengi.
Tatizo kubwa la ugonjwa huu ni kuwa siku zote tunatibu
matokeo, yaani unapotikea viongozi serikalini wanajihimu kuandaa
mazingira ya kuwapatia wagonjwa tiba.
Kufanya hivo ni kushughulika na matokeo ya tatizo na kuacha
chanzo cha tatizo ambacho kwa mujibu wa wataalamu wa afya ni wananchi kuendelea
kuishi kwenye mazingira machafu yanayotoa mwanya watu kula vinyesi kitendo
kinachosababisha with kuugua ugonjwa huo.
Tukifuata kanuni hii ya kuangalia chanzo kisha tuangalie
matokeo, kuna uwezekano mkubwa wa kushinda changamoto zinazotukabili katika
shughuli zetu za kila siku iwe kwenye biashara, kazini, masomoni na maeneo
mengine.
Pia naomba usemi huu kila mara "usizibe ufa uktani kabla ya
kujua chanzo cha ufa huo"
Endelea kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila
siku. Kama makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye
kundi la Whats App ili uweze kujifunza. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO YANGU, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
Ndimi: Benson chonya
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.