Sep 7, 2016
Namna Ya Kukiendeleza Kipaji Chako.
Siku kaadha zilizopita kama utakuwa ni mfuatiliaji wa safu hii
nilieleza kwa kina namna ya kugundua kipaji chako, hivyo naomba nifanye
mwendelezo wa maada hiyo kwa kueleza ni jinsi gani ya kuendeleza kipaji chako
ili kisife maana watu wengi hufa na vipaji vyao.
Kama ambavyo nilieza ya kwamba kipaji ni uwezo ambao mtu
huzaliwa nao (talanta). Talanta hiyo imegawanyika katika makundi mbalimbali na
kumfanya mtu aweze kufikiri, kubuni, kuvumbua au kusanifu kitu fulani, vilevile
kipaji huusisha kwa asilimia kubwa na viungo vya mwili katika kufanya jambo
fulani kama vile ufundi, kucheza na vitu vingine vingi.
Pia watu wengi hujiuliza kipi kinaanza kati ya ndoto na kipaji?
Ukweli ni kwamba kipaji huanza kisha ndoto kufuata. Kwa mfano leo unaweza ukawa
una kipaji cha kucheza mpira lakini ndoto yako ni kuwa mchezaji mkubwa wa
mpira afrika mashariki na kati.
Pia ikumbukwe ya kwamba kipaji huwa hawasomei maana ni uwezo
ambao mtu huzaliwa nao mtu, hivyo elimu hutumika kama nyenzo ya kukuza na
kupalilia kipaji hicho.
Zifuatazo ndizo
mbinu za kukuza kipaji chako.
1.Tafakari kila
unachokiona na kusikiliza.
Hii ni mbinu bora sana katika suala la ukuzaji wa kipaji chako
kwa sababu ulimwengu wa leo una vitu vingi hivyo ni lazima ujue ni vitu gani
ambavyo unapenda kusikiliza na kukiona zaidi na kuachana na vitu ambavyo
havikusaidii.
Kwa mfano, kama leo unataka kuwa muigizaji bora wa filamu ni
lazima mara kwa mara upende kutazama filamu za watu mbalimbali pia ni lazima
masikio yako yawe tayari kusikiliza mambo yote ya muhimu yahusuyo masuala ya
filamu.
Vivyo hivyo kwa kuutazama mfano huo ni lazima ujue ni kipi kwako
ni cha muhimu katika kukupa taarifa sahihi katika ukuzaji wa kipaji chako.
2. Tafuta mtu wa
kukuongoza.
Hili ni tatizo kubwa sana kwa watu wengi, watu wengi wana vipaji
ambavyo vina uwezo mkubwa wa kuibadili jamii na maisha yake kwa kiwango
kikubwa, lakini changamoto kubwa ambayo inawakabili watu hao ni kwamba hawana
mtu sahihi ambaye ana husika kwa asilimia kubwa katika kumuongoza katika tasnia
ambayo anayoifanya.
Watu wengi wanapenda kukomaa peke yao katika vipaji vyao na
mwisho wa siku vipaji hivyo hufa.
Inawezekana ukawa unadhani nazungumzia mtu ambaye anakuvutia
ambaye mnafanana kipaji, la hasha mimi nazungumzia mtu ambaye atakupa ‘network’
ya kukuza kipaji na hatimaye kutengeneza pesa.
Siku zote ukumbuke unahitaji mtu sahihi wa kukuongoza na
kukisimamia kipaji chako ili uweze kutimiza ndoto zako, hiyo ni ya muhimu sana
kuliko neno lenyewe.
3. Jiunge katika vikundi
mbalimbali.
Ili uweze kuwa bora zaidi katika kipaji chako huna budi kujiunga
katika vikundi mbalimbali ambavyo vinajihusisha na vitu ambavyo vinalandana na
kipaji chako.
Kwa mfano, unapenda kuwa mwanamziki bora ni lazima ufuatane na
watu wenye vipaji vya mziki kwani kufanya hivyo ni kujifunza mengi kutoka kwao,
pia ukumbuke ule usemi kutoka kwa wahenga wetu ambao husema penye wengi pana
mengi.
4. Hudhuria semina.
Kama una amini katika kujifunza, bali endelea kujifunza kwa kuwa
karibu na watu ambao huendesha semina ambazo zinaendana kwa asilimia kubwa na
kipaji chako.
Kufanya hivi kutakupa hamasa na ufanisi wa kiutendaji ili
kuhakikisha ya kwamba ndoto ya kipaji chako inakwenda kuwa kweli baada ya muda
mfupi hasa pale ambapo utachukua jukumu ya yale uliyojifunza kuyaweka katika
matendo.
5. Kujifunza vitu
vipya.
Kujifunza vitu vipya ndipo ambapo siri ya mafanikio kila mmoja
wetu ilipo, nimesema kujifunza vitu vipya kila kwa sababu ulimwengu wa sasa
kila siku kuna uvumbuzi wa vitu mbalimbali kila itwatayo leo hivyo fanya
makusudio ya dhati kuweza kujifunza.
Hivyo wito wangu kwako ni uwe karibu sana na vyombo mbalimbali
ambavyo vitakupa taarifa sahihi hususani suala zima la jinsi gani utaweza
kukuza kipaji chako na hatimaye kupata pesa.
Dunia ni pana, ila ina maneno machache naomba kwa leo niishie
hapo tukutane katika makala iyayo, pia usisite kumshirikisha mwingine kama
ambayo mimi nimeamua kufanya kwako.
Endelea kujifunza zaidi kupitia dirayamafanikio.blogspot.com
kila siku kwa kujifunza.
Ndimi: Afisa Mipango Benson Chonya.
0757-909942.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.