Sep 6, 2016
Magonjwa Sugu Yanayotibiwa Na Kitunguu.
Kazi
kubwa sana ya mbogamboga pamoja na viungo mbalimbali na matunda tunayokula ni kuilinda na
kuirekebisha mifumo mbalimbali ya ufanyaji kazi iliyoharibika mwilini.
Kuharibika
kwa mifumo hii kunasababishwa na uharibifu wa mazingira, uchovu wa mwili,
kuingia kwa vijidudu visivyotakiwa mwilini kama vile virusi au bacteria, na
wakati mwingine mifumo hii huharibiwa na sumu kutoka kwenye madawa ya kuulia
wadudu wa majumbani.
Nikisema
wadudu wa majumbani, nina maana inzi, mbu, mende, komba mwiko na wengine.
Hivyo
basi ni vyema tukawa waangalifu kwenye kilimo tusitumie mbolea kali sana au zenye
kemikali kwa wingi, vilevile tusitumie madawa makali kwenye kuua wadudu
waharibifu wa mazao kwa kuwa sumu hizi huchukua muda mrefu kuisha nguvu yake.
Mboga
mboga au matunda ili yalete afya iliyokusudiwa ni muhimu kutilia maanani usafi
kabla ya kutumia.
Kama
tunatumia mbogamboga na matunda kama dawa au
kinga kwa matatizo fulani, ni lazima mtumiaji aweke nia ya kufanya hivyo
na kufuata taratibu zake, kwani miaka mingi vitu hivyo vinatumika kwa namna
hiyo. Kumbuka kuwa pia mwili una namna yake ya asili ya kujikinga na kijitibu.
Hebu
tutazame kitunguu. Kitunguu ni kiungo kinachotumika kama dawa ya asili, kwa kuwekwa
kwenye chakula au mboga wakati wa kupika, vilevile huwekwa kwenye kachumbari.
Kuna
aina kama tatu hivi za vitungu maji. Kuna vile vyeupe, vyekundu na vya njano.
Aina
nzuri sana na yenye manufaa kwa afya zetu ni vitunguu vyeupe. Inaaminika kuwa
asili ya vitunguu hivi ni Asia ya kati, inawezekana kuwa ni Iran au Pakstani.
Kitunguu
kimekuwa kikitumika kama dawa na kinga nzuri kwa muda mrefu bila wengi kujua. Kwa
mfano, kitunguu kina protini kiasi, kimejaa madini ya calcium na riboflavin kwa
wingi sana.
Kwa
kila gram 100 kuna majimaji asilimia 86. 6, protini asilimia 1.2, mafuta
asilimia 0.1, nyuzinyuzi asiimia 0.6, wanga asilimia 11.1, madini mengine
yaliyomo ni pamoja na phosphorus, chuma, carotene, thiamine, nicin
na vitamin C.
Kwa
hiyo tunapokuja katika suala la tiba, kitunguu kinaweza kutibu matatizo kama;
kifua kikuu. Juisi ya kitunguu ikitumika kijiko cha chai asubuhi na jioni
inaondoa tatizo hili. Unaweza ukachanganya na asali au sukari guru.
Pia
matatizo kwenye njia ya hewa (upumuaji). Kitunguu kinayeyusha mgando kwenye
mishipa ya damu na kuzuia isikae kwenye njia ya hewa, hivyo hutibu kikohozi,
mafua na matatizo ya mapafu.
Vijiko
vidogo vitatu vya juice yake, vilivyochanganywa sawasawa na asali mara mbili
kwa wiki ni dawa tosha.
Vitunguu
vina madini ya chuma yanayoyeyuka kirahisi sana mwilini na hiyo ni vizuri sana
kutibu ukosefu wa damu.
Magonjwa
ya moyo. Kwa kuwa kitunguu kina mafuta asili, madini mabalimbali pamoja na vitamin
kadhaa, kinasaidia kuondoa sumu zinazoweza kuudhuru moyo na hivyo kuondoa
mchafuko kwenye mishipa ya damu.
Ni
vyema kutumia gram 100 za kitunguu kwa siku.
Kindupindu;
chukua gramu 30 za vitunguu na pilipili manga 7. Pondaponda kwa pamoja, mpe
mgonjwa. Unaweza kuongeza asali au sukari kidogo.
Huleta
kiu, kuchoka na kuzuia au kupunguza kutapika.
Matatizo
ya meno; pia matataizo haya huweza kutibika kwa kutafuna ganda moja la kitunguu
kwa siku, huuwa vijidudu vibaya kinywani na kwenye meno.
Matatizo
ya ngozi; kitunguu kinachachatika kwenye ngozi na kinaamsha mzunguko wa damu. Tatizo
la kwenye ngozi lilosababishwa na virusi, chukua kitunguu kikate katikati,
halafu sugua kwenye ngozi iliyoliwa.
Kitunguu
kinafaa kwa mambo mengi sana, tukitumie hasa kikiwa kibichi, kwani kikipikwa
kinakuwa kigumu kusagwa mwilini.
Endelea
kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kujifunza kila siku.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki,
Imani
Ngwangwalu,
Simu;
0713 048035,
Email;
dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.