Sep 28, 2016
Hatua Muhimu Za Kutengeneza Uhuru Wa Kifedha.
Ili
uweze kuishi maisha ya mafanikio makubwa kwako na kuwasaidia wengine ni lazima
kwanza uwe huru kifedha. Unapokuwa upo huru kifedha ni hatua inayokufanya
kuweza kutekeleza mahitaji yako yote ya kifedha, ikiwa pamoja na hata kusaidia
wengine bila tatizo lolote lile.
Hivyo
mpaka hapo unaona kwamba, ni lazima sana kuufikia uhuru wa kifedha ili kuishi
maisha yenye manufaa kwetu na kwa wengine wanaotuzunguka. Sasa jambo la muhimu
kuelewa hapa, tunawezaje kuufikia huo uhuru wa kifedha? Ni hatua zipi ambazo
tunatakiwa tuzifuate?
Zifuatazo
Ni Hatua Muhimu Za Kutengeneza Uhuru Wa Kifedha.
1.
Jiwekee malengo ya kifedha.
Tambua kwamba Ili
kufikia uhuru wa kifedha, kabla ya kuanza kuwekeza, kuweka akiba, kutengeneza
bajeti au kuweka pesa ya dharura, kitu cha kwanza unachotakiwa kufanya ni
kujiwekea malengo ya kifedha. Hiki ni moja ya kitu muhimu sana katika kuufikia
uhuru wa kifedha.
Jiwekee malengo ya kifedha. |
Jiwekee
malengo ya kifedha yaliyowazi na yanayoeleweka. Kwa mfano, unaweza ukajiwekea
malengo kwamba baada ya miaka mitano ijayo
nataka kumiliki milioni mia moja. Pengine unaweza ukajiwekea malengo ya kifedha
kwamba ili kutimiza lengo hilo, kila mwaka ni lazima niingize milioni ishirini.
Unapokuwa
na malengo ya wazi kama hivi ya kifedha, inakuwa ni rahisi kwako kuufikia uhuru
wa kifedha. Unajua ni kwa nini? Ni kwa sababu unakuwa unajua unakotaka kufika
kifedha na pia inakuwa sio rahisi kwako kupoteza pesa zako kwa mambo yasiyokusaidia
kuufikia uhuru huo unaotaka.
Kwa
hiyo, ili uweze kuufikia uhuru wa kifedha, jambo la kwanza la kuzingatia,
jiwekee malengo ya kifedha. Tafuta daftari lako la kumbukumbu na andika
unahitaji pesa ngapi kwa mwaka, unahitaji pesa kiasi gani baada ya miaka
mitano. Kwa kufanya hivyo utaufikia uhuru wa kifedha kwa sababu juhudi zako
zitakuwa kubwa sana kukusaidia kutimiza lengo lako.
2.
Tengeneza bajeti.
Mara
baada ya kujiwekea malengo ya kifedha, hatua inayofuata ni kutengeneza bajeti yako. katika hiyo bajeti
utakayoitengeneza ni lazima uifuate na kuitekeleza kila siku. Unapokuwa
unaifuata bajeti yako inakusaidia zaidi kuwa karibu na lengo lako la kuufikia
uhuru wa kifedha.
Ili
kufanikisha hili vizuri, kabla hujapata pesa andaa orodha ya vitu
utakavyokwenda kununua kabla. Kisha baada ya hapo fanya manunuzi kama orodha
yako inavyosema na sio kinyume chake. Kwa hiyo unaona, Kila unapokuwa na bajeti
yako na ukaitekeleza, inasaidia kuokoa pesa ambazo zingepotea bila sababu na
inakuwa ni chanzo cha kuufikia uhuru wa kifedha.
3.
Weka akiba.
Kwa
kiasi chochote cha pesa unachokipata hata kiwe kidogo vipi, jifunze kuweka
akiba angalau kwa sehemu. Watu wengi hili ni somo gumu sana kulielewa juu ya
uwekaji wa akiba na ni kiwazo kikubwa cha kuufikia uhuru wao wa kifedha.
Sasa
kwa lugha rahisi ili uweze kuufikia uhuru wa kifedha ni lazima uweke akiba. Unapokuwa
unaweka akiba inakuwa inakusaidia sana kutengeneza mtaji kidogo kidogo kama
huna mtaji huo au unaazia chini kabisa kimaisha.
4. Jiwekee pesa ya dharura.
Hata
uwe unaingiza pesa nyingi vipi lakini moja ya jambo ambalo unatakiwa kulifanya
ili uweze kuufikia uhuru wa kifedha ni kutenga fedha ya dharura. Kiuhalisia binadamu
tunachangamoto nyingi sana. Hivyo ni lazima pesa hii uwe nayo unapoelekea
kwenye uhuru wa kipesa.
Hakuna
sababu ya kusema sina mtaji au sijawekeza katika hili kwa sababu pengine
niliumwa na nikatumia pesa zote. Ili kuepuka ‘majanga’ kama hayo unatakiwa kujiwekea pesa ya dharura. Pesa hiyo
inakuwa mkombozi wako kwa lolote linatokea ambalo hukupanga.
5.
Wekeza.
Sasa
baada ya hatua hizo ambazo tumetoka kuzijadili, ili kuufikia uhuru wa kifedha
kiuhakika hatua inayofuata ni kuwekeza. Bila kuwekeza itakuwa ni kazi ngumu
sana kuweza kuufika uhuru wa kifedha.
Hapa
ni lazima ukae chini na kutafuta ni kitu gani ambacho unakiwa ufanye au uwekeze
na kikakuletea pesa nyingi. Kwa kitu hicho utakachokichagua, anza kukitekeleza mara
moja kwani kitakufanikisha na kukupa uhuru wa kifedha.
Kama
kweli nia yako ni kuufikia uhuru wa kifedha, unalazimika sana kujiwekea malengo
ya kifedha, kutengeneza bajeti yako, kutenga pesa za dharura, kuweka akiba na
kuwekeza katika eneo ambalo litakupa faida kubwa. Hizo ndizo hatua muhimu za
kutengeneza uhuru wa kifedha.
Endelea
kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama
makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la
Whats App ili uweze kujifunza. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO YANGU, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA
KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni
wako rafiki,
IMANI
NGWANGWALU,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.