Sep 15, 2016
Mambo Ya Msingi Ya Kuzingatia Katika Kufanya Uchunguzi Wa Kibiashara.
Moja ya changamoto kubwa
inayowakabili wafanyabiashara wengi ni kutokujua kwa undani jinsi ya kufanya
utafiti wa kimasoko katika biashara ambayo anaifanya au anataraji kuifanya, na
kutokana na changamoto hiyo, imepelekea
biashara nyingi kushindwa kukua na hata kupelekea baadhi ya biashara nyingine
kufa kabisa.
Hivyo ni jambo jema ukayafahamu mambo
ya msingi yahusuyo masuala ya masoko katika kibiashara ili kuweza kukuza
biashara yako na hatimaye kupata faida.
Yafuatayo ndiyo mambo ya msingi ya
kuzingatia katika kufachanya uchunguzi wa masoko.
1. Nani atakuwa ni mteja wako?
Hili ni swali la msingi la kujiuliza.
Kwa mfanyabiara yeyote ni lazima aweze kutafakari kwa makini zaidi ni nani
ambaye atanunua bidhaa au huduma ambayo unaitoa. Katika kujiuliza swali hili ni
lazima uweze kumchanganua mteja wako kwa kuangalia mambo yafutayo;
Uwezo wa kiuchumi kwa wahitaji wa bidhaa au huduma.
Kwa kutazama uwezo wake wa kifedha ni
vyema ukajiuliza je kwa bidhaa au huduma ambayo ninaiuza mteja wangu ana uwezo
wa kununua?. Kwa mfano, huwezi ukafungua biashara ya ‘supermarket’ maeneo ya
vijijini kwani hali ya maeneo mengi ya vijinini hawana uwezo Wa kuweza kununua
bidhaa kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na mjini.
Angalia ukubwa wa soko lako katika kuchunguza biashara. |
Umri na jinsia.
Ni vyema ukajiuliza kuhusu watumiaji
wa bidhaa au huduma yako kwa kuangalia uhitaji wa bidhaa yako kwa kujiuliza je,
ni umri gani ambao watatumia zaidi bidhaa yako? Na ni lazima ujiulize ni jinsia
gani watapendelea zaidi kutumia bidhaa yako? Ukipata majibu sahihi ndipo
utakapojua ni biashara gani utaifanya katika eneo husika.
2. Upi ukubwa wa kisoko?
Hili pia ni suala la msingi la kuweza
kuzingatia hususani suala zima la kufanya biashara yenye ubora na yenye kukua.
Watu wengi huwa hawalizingatii hili na hivyo kupelekea biashara kufa, lakini
kujua ukubwa wa soko huusisha masuala ya uhitaji wa bidhaa au huduma, kufanya
hivi kutakusaidia kwa kiwango kikubwa kujua uwezo wa kuzalisha kwa kiwango gani
kulingana na uhitaji wa wateja wako.
Soma; Mawazo Muhimu Unayotakiwa Kuwa
Nayo Ili Kukuza Biashara Yako.
3. Bei itakuwa ni kiasi gani?
Kwa mjasiriamali yeyote ni vyema
ukajua namna ya kupanga bei katika biashara yeyote ambayo unaifanya au unataka
kufanya, kama utakuwa ni mdau mzuri wa mtandao huu nilieleza namna ya kuweza
kupanga bei katika biashara yako.
Kwa harakaharaka nikukumbushe ya
kwamba katika upangaji wa bei ni lazima uangalie uhitaji wa bidhaa, gharama za
uzalishaji na uendeshaji na pia ni lazima uwatazame washindani wenzako
wanafanyaje katika biashara hususani suala zima la kupanga bei.
Soma; Mbinu Bora Za Kupanga Bei
Katika Biashara.
4. Namna ya kufikisha huduma/bidhaa
kwa walengwa.
Hili ni jambo muhimu kuweza
kulifahamu. Katika biashara yeyote ile kuna njia mbili za kufikisha huduma au
bidhaa kwa wateja. Jambo la kwanza ni kuweza kufikisha bidhaa moja kwa moja kwa
mteja, njia hii humkutanisha mzalishaji na mteja.
Na jambo la pili kuweza kufikisha
bidhaa kupitia ununuzi rejareja au kwa jumla, njia hii haimkutanishi mzalishaji
na mteja. Mfano mzuri kama tufanyavyo kununua vitu kwa madukani kwa mangi.
Hivyo katika kufanya utafiti wa kimasoko ni lazima ujue namna na mbinu ambazo
zitakufanikisha kufanya biashara kwa ufanisi hatimaye kupata faida.
Endelea kutembelea mtandao huu kila
Mara ili kujifunza vitu vitakavyobadili Maisha yako kwa namna moja ama
nyingine.
Kama makala hii
imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili
uweze kujifunza. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO
YANGU, kisha ikifutia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
Ndimi; Benson Chonya
0757909942
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.