Sep 13, 2016
Mambo Matatu Madogo Yanayoua Ubunifu Wako.
Kati
ya kitu ambacho unalazimika kukijua vizuri, ili kikusaidie kuongeza thamani
kubwa ya maisha yako ni ubunifu. Hiyo ikiwa na maana, katika kila eneo la
maisha yako ambalo lina ubunifu mara nyingi mafanikio ni ya wazi.
Hebu
jaribu kuangalia ubunifu unaofanywa na kampuni mbalimbali. Ukipita mtaani ukawa
na jicho la kichunguzi, utagundua vipo vitu vingi sana vinavyobuniwa kila
kukicha.
Je,
ulishawahi kujiuliza hata mara moja, kwa nini kampuni kubwa nyingi zimeng’ang’ana
na ubunifu sana? kama bado hujawahi kujiuliza, je unafikiri wanapoteza muda wao
kwa kubuni huko?
Kwa
kile ambacho wengi hawajui, ipo siri kubwa sana ya mafanikio iliyofichika
kwenye ubunifu. Ndio maana, kwenye kila kitu unachofanya ili kukuletee
mafanikio umekuwa ukisisitiziwa lazima uwe mbunifu kwanza.
Lakini
pamoja na umuhimu mkubwa wa ubunifu katika suala zima la kutupa mafanikio, bado
wengi si wabunifu. Na kwa sababu hiyo maisha yao huendelea kuwa duni kadri siku
zinavyokwenda.
Hebu
leo hii kwa kusoma makala haya naomba tuangalie mambo machache ambayo huua
ubunifu. Kwa kujifunza mambo hayo itakusaidia sana kuchukua hatua na hatimaye kuweza
kusonga mbele.
1. Kushindwa kupata usingizi wa
kutosha.
Kitaalamu,
binadamu wa kawaida anatakiwa kupata usingizi kwa wastani wa saa saba hadi nane
kwa siku. Inapofika mahali ukakosa kulala kwa muda huo, huwa yapo matatizo
ambayo yanaweza kujitokeza kama ya kiafya na kukosa ubunifu.
Mara
nyingi unapokosa usingizi wa kutosha na kwa muda mrefu, polepole unaua ubunifu
wako bila kujijua. Hili ndilo linalotokea kwa wengi, hasa wale ambao kwao
usingizi hawapati wa kutosha.
Kutokuwa tayari kujifunza, ni chanzo cha kuua ndoto zako. |
Kikawaida
sio rahisi kufikiria vitu vya maana kama kichwa chako kimejaa usingizi, zaidi
utakuwa unawaza kulala. Hivyo, kama unataka kuongeza ubunifu wako jitahidi sana
kupata usingizi wa kutosha.
Ndio
maana, ukilala vizuri na kupata usingizi wa kutosha akili yako inakuwa ina
nguvu sana ya kubuni mambo na inakuwa inafikiria kwa ufasaha. Jambo la
kuzingatia hapa, hakikisha unapata usingizi wa kutosha ili usiue ubunifu wako.
2.
Kutokuwa tayari kujifunza.
Watu
wengi wanafanya vile wanavyofanya lakini hawako tayari kujifunza kwa undani
mambo hayo wanayoyafanya. Kwa mfano, utakuta mtu ni mfanya biashara, lakini
hayuko tayari kujua kwa undani sana biashara anayoifanya.
Sasa
katika hali ya kawaida inakuwa ni ngumu sana kuweza kuwa mbunifu, kama hata
jambo unalolifanya hauko tayari kujifunza changamoto zake na uzuri wake kwa
undani. Na kwa sababu hii, wengi hujikuta wakiua ubunifu wao na ndoto kwa
pamoja.
3.
Kutokuwa karibu na watu wabunifu.
Pia
jambo lingine ambalo linaonekana ni la kawaida, lakini linaua ubunifu wengi ni
kule kukaa mbali na watu wabunifu. Ili uwe mbunifu mzuri ni lazima ujifunze na
kuwa karibu na wabunifu wenzako.
Haiwezekani
lengo lako ni kukuza ubunifu, halafu ukaendelea kukaa na watu wa kawaida ambao
hawana maono hayo. Kwa wale wote ambao wako mbali na wabunifu wengine, ni wazi
ubunifu wao hupotea siku hadi siku.
Kwa
kumalizia makala haya, ni vyema ukatambua hayo ndiyo mambo yanayochangia kuua ubunifu wako kwa sehemu kubwa. Chukua hatua kubadili mambo haya na endelelea
kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama
makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la
Whats App ili uweze kujifunza. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO YANGU, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA
KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni
wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,
0713 04 80 35
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.