Sep 1, 2016
Njia 3 Za Kugundua Fursa Za Kibiashara Mahali Ulipo.
Uhali gani mpenzi msomaji wa safu hii ni matumaini yangu
makubwa u mzima wa afya tele nami kwa upande wangu sijambo na tunakila sababu
ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia afya njema.
Katika makala haya ya leo nataka tujikite zaidi namna ya
kugundua fursa katika eneo unaloishi, si kugundua tu na kuzifanya fursa hizo
kuwa pesa. Watu wengi huwa tunaangalia vitu katika taswira ambayo kwa namna
moja ama nyingine imekuwa haibadili maisha yetu.
Na ukichunguza sababu ya kutokea kwa
hali hiyo ni kwamba hakuna uhusiano wa macho na ubongo, huenda ukawa
haujanielewa ila ukweli ni kwamba tumekuwa
wavivu wa kufikiri. Hivyo nikusihi ya kwamba kila kitu ambacho unakiona mbele
ya macho yako ni lazima ukitafakari katika ubongo usio kuwa wa kawaida, maana
yangu ni kwamba kila kitu unachokiona lazima uwaze kitakupaje pesa.
Pasipo kupoteza radha ya maada yangu ya leo nadhani
nijikite zaidi kwa kuangalia njia ya kuzitambua fursa katika eneo lako unaloishi.
1. Tafuta mahitaji ya watu.
Kila mahali unapoishi kwa namna moja ama nyingine watu
huwa wanahitaji huduma au bidhaa fulani. Hivyo ni vyema ukaa chini na
kutafakari ni vitu gani unadhani watu wanahitaji nini zaidi ? Baada ya kupata
majibu ni wakati wako muafaka wa kuweza kuvisogeza kwa watu hao na wao
wakanunua.
Kufanya hivyo ni njia nzuri ya wewe
kupata pesa. Pia watu wengi hupenda Huduma ambayo inapatikana kwa rahisi hivyo
fanya uchunguzi wa kutosha na kuona watu wanapenda nini zaidi kuzisogeza huduma
hizo kwa watu.
2. Toa majibu ya changamoto za watu.
Kuna swali la msingi sana la kuujiuliza juu ya maisha
yako. Swali lenyewe ni kama lifuatavyo hivi ni kwa nini huna pesa? Ukipata
majibu ya swali hilo ni nusu ya kupata mafanikio.
Moja ya tafiti ambazo ziliwahi kufanywa ni kwamba watu
wengi hawana pesa kwa sababu kuu mbili, mosi kwa sababu hawatatui matatizo za
watu. Sababu ya pili watu wengi hawana pesa kwa sababu wanatatua matatizo
machache, hivyo siri ya kubwa ya mafanikio yako ipo katika kutatua matatizo ya
watu wengi katika njia ya tofauti na walivyozoea wengine.
3. Rahisisha majibu ya kazi.
Watu wengi hupenda vitu ambavyo havina ugumu katika
kufanya kazi, wetu wengi tunapenda kufanya kazi kwa kutumia njia rahisi na
kupata majibu kamili tunayoyatarajia.
Hebu angalia moja ya tajiri mkubwa dunia bwana Steve Job ambaye ni
mmliki wa kampuni ya Apple, yeye alitazama jinsi watu ambavyo walikuwa
wanatumia vifaa vya kietroniki kama simu za butani, desktop computer ambazo
kimsingi zilikuwa ni vigumu hata kutembea nazo.
Hivyo Steve Job akaamua kutengeneza
vitu hivyo hivyo kwa kuongeza thamani leo hii tunafurahia simu za apple na
laptop za apple ambazo zina mambo mengi pia zinasaidia kurahisisha kazi na
kuifanya dunia kama kijiji.
Kwa hiyo kama alivyofanya tajiri huyo
ni wakati mwafaka kufikiri ni zipi kazi ngumu ambazo zinawakabiri watu na
kuweza kuzipa majibu ya ugumu huo.
Ndimi afisa mipango Benson Chonya.
Simu; 0757-909942
bensonchonya23@gmail.com
dirayamafanikio.blogspot.com
bensonchonya23@gmail.com
dirayamafanikio.blogspot.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.