Jan 4, 2017
Falsafa Bora Ya Fedha Unayotakiwa Kuitumia Kila Wakati…Ili Kufanikiwa.
Ili kufanikiwa kifedha, ipo falsafa ya mafanikio ambayo inatumika
kuwaongoza watu na hadi kufikia mafanikio hayo makubwa sana ya kifedha. Falsafa
hiyo ndiyo inayopelekea wengine wakawa na pesa na wengine wakawa hawana,
wengine wakawa matajiri na wengine wakawa maskini.
Kwa mfano, falsafa kubwa ya watu wenye mafanikio
hasa linapokuja suala la pesa, ukilinganisha na wale ambao hawajafanikiwa iko
hivi; watu wenye mafanikio falsafa yao ipo kwenye kuwekeza kila aina ya pesa
wanayoipata hata iwe ndogo vipi. Na kile
kiasi kidogo kinachobakia hukitumia katika katika matumizi ya kawaida, lakini
mara baada ya kuwekeza.
Wakati watu ambao hawajafanikiwa nao pia falsafa
yao ya pesa ni kutumia kila pesa wanayoipata na kiasi kidogo kinachobakia hicho
ndio huanza kujaribu kuwekeza. Watu wasio na mafanikio, matumizi ndio kipau
mbele cha kwanza kabisa kabla ya uwekezaji wowote ule.
Bila kujali shida zetu tulizonazo, changamoto
mbalimbali, Ili kufanikiwa unatakiwa kujiwekea falsafa ya pesa kama
wanavyofanya matajiri, ni lazima uanze kuwekeza kwanza hata kwa pesa kidogo,
halafu matumizi yatafuata, kinyume cha hapo utakwama sana na utashindwa kufikia
uhuru wa kipesa.
Je,
unavyofikiri kwa falsafa hizo mbili, je, hali ya maisha inaweza ikawa sawa kwa
watu hao wawili kutokana na matumizi ya hizo falsafa? Najua majibu mpaka hapo
unayo kwamba falsafa ipi ni sahihi. Kama utatumia falsafa ya pesa ya watu
wasiofanikiwa, tambua utakuwa hivyo na ukitumia falsafa ya pesa ya watu wenye
mafanikio, utafanikiwa pia.
Endelea
kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama makala hii
imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja
tena kwa ukaribu. Kujiunga tuma neno THE
UNIVERSITY OF WINNER’S, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI
KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.