Jan 7, 2017
Siri Ya Kumudu Kuzungumza Mbele Ya Watu Vizuri.
Wapo baadhi ya wasomaji wangu
walikuwa wakiniuliza "eti nifanye
nini ili kuwa mzungumzaji mzuri mbele ya watu wengine?” Swali hili
kiukweli limekuwa likiwatatiza watu wengi sana kwa namna moja ama
nyingine.
Na kutokana na hali hiyo kumewafanya
watu hao hao kuwa katika hali unyonge, kwani huishi watachekwa na sababu
nyingine kama hizo za kushindwa kuzungumza mbele ya watu.
Lakini ukweli ni kwamba endapo
utazijua siri hizi kuwa mzungumzaji bora zitakwenda kukusaidia kutoka katika
hali uliyonayo hatimaye kuwa mzungumzaji mzuri na bora kabisa.
Je, unajua ni mbinu zipi ambazo
zinaweza unaweza kuzitumia na kuwa mzungumaji bora mbele ya watu wengine?
Kuwa na taarifa za uhakika na
kutosha.
Moja ya njia bora ya kuwa
mzungumzaji mzuri ni kuwa na utajiri wa vitu vingi katika kibubu cha ubongo
wako . Watu wengi wanajiona hawawezi kuchangia maada yeyote ile mbele ya
wengine hii ni kwa sababu wamekuwa hawana taarifa sahihi na za uhakika za
kuweza kuzungumza.
Hivyo kama endapo nia yako ni kutaka
kuzungumza mambo mbalimbali katika jamii yako ni lazima ujue vitu hivyo kwa
undani zaidi.
Kama unataka kuwa mzungumzaji juu ya
masuala ya michezo ni lazima uweze kufuatilia taarifa mbalimbali za michezo
kutoka vyanzo mbalimbali ambavyo hutoa taarifa za michezo. Kutokuwa na taarifa
nyingi za kutosha zimefanya watu mbalimbali kufanya vitu vile vile kila
wakati.
Watazame wasanii mbalimbali katika nchi wameshindwa kuwa wabunifu katika kazi zao kwa sababu waliyonayo wanahisi yanatosha. Ila ukweli ni kwamba kujifunza vitu vipya hakuna mwisho.
Na daima kumbuka ule usemi usemao "no research no right to speak"
kama hauna utafiti wa kutosha huna haki ya kuzungumza, hivyo ukitaka kuwa
mzungumzaji mzuri ni lazima ufanye utafiti wa kutosha juu ya jambo hilo.
Lazima uwe msikilizaji mzuri.
Hii pia ni siri mojawapo ya kuwa
mzungumzaji mzuri mbele ya watu wengine. Huwezi kutaka kuwa mzungumzaji bora
kama hujui kusikiliza. Matokeo ya kuzungumza chanzo chake hutokana na
kusikiliza vizuri anachokizungumza mtu mwingine.
Pia tatizo hili la kutojua kusikiliza
limekuwa likiwaathiri watu wengi sana. Kwa tafiti zinaonyesha ya kwamba msikilizaji
ndiye ambaye hutumia nguvu nyingi katika kuelewa kuliko mzungumzaji.
Kama ndivyo hivyo hakikisha unatumia
nguvu nyingi sana katika kusimamia akili yako katika kusikiliza, kama kweli
unahitajj kuwa mzungumzaji mzuri.
Kujiamini
Suala kubwa ambalo limekuwa
likiwaathiri watu wengi katika kuzungumza ni kushindwa kujiamini. Wengi
wamejenga na hofu ambayo imekuwa haiwasaidii.
Wengi huona ya kwamba Watachekwa,
watazomewa na vitu vingine vingi kama hivyo. Lakini hali hii imekuwa ikizuka
kwa baadhi ya watu ambao kwa asilimia kubwa imejengeka tangu wakiwa wadogo.
Na hofu hiyo umekufanya ujione
mnyonge sana, hata wakati mwingine umekuwa ikihisi huna thamani mbele ya
watu wengine. Ila ninachotaka kukwambia njia bora ya kuondokana na hofu hiyo
uliyonayo ni kufanya kitu ambacho unakiogopa.
Kama umekuwa unashindwa kuzungumza
mbele za watu anza leo. Kwani kama nilivyosema hapo awali njia bora ya Kuwa mtu
mwenye mafanikio ni kufanya kitu ambacho unakiogopa.
Anza kufanya mazoezi ya kuzungumza.
Huwezi kuwa mzungumzaji bora kama
hutaki kufanya mazoezi ya kuwa hivyo inavyokata. Hivyo mazoezi ni chanzo cha
ushindi. Kama ilivyo kwa wachezaji wa mpira kama hawajaanza kucheza mechi ni
lazima wafanye mazoezi.
Hivyo, hata wewe unahitaji kutenga
walau nusu saa ya kuzungumza. Unaweza ukachugua maada fulani na
ukafanya mazoezi angalau nusu saa ya kuzungumza maada hiyo ukiwa peke yako.
Endapo utafanya hivyo kutakusaidia
kujenga uwezo wa kukufanya uwe mzungumzaji mzuri na kwa watu wengine.
Yawezekana kabisa suala hili la
kutokuwa mzungumzaji linakuhusu wewe ambaye unasoma makala haya,
nichotaka kukwambia kila kitu kinawezekana na utakwenda kuwa mzungumzaji
mzuri mbele ya watu wengine endapo tu yote ambayo nimeyaeleza utaamua
kuyafanyia kazi.
Ndimi afisa Mipango Benson Chonya,
bensonchonya23@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.