Jan 17, 2017
Funguo Tano Za Mafanikio Ya Mjasiriamali Wakati Wote.
Kitu
kizuri kwa mjasiaramali yoyote yule uwe unaanza au tayari safari hiyo ulishaanza ni kujiandaa kuwa mshindi. Ni muhimu
sana kujua wewe ni mshindi kwa kile unachokifanya bila kujali ni changamoto zipi
unakutana nazo.
Lakini
hata hivyo huwezi kuwa mshindi kama hutaweza kujua siri ya ushindi huo utaupata
vipi. Kutokana na hilo sasa hapo ndipo unalazimika kuzijua funguo tano za mafanikio ukiwa kama mjasiriamali.
Hizi
ni funguo tano kweli kwa mjasiriamali ambazo ukizitumia, zitakupa mafanikio na kukufikisha kule unakotaka kufika . Funguo
hizo ni zipi, fuatana nasi katika makala yetu ya leo kujifunza.
1.
Weka kushindwa nyuma kabisa.
Kwa
kawaida huwa yapo makosa na kushindwa
kwingi hasa pale unapoanza biashara au hata pia unapokuwa unaendelea na biashara
yako. Yote hayo yanapotokea ikiwa kweli wewe ni mjasiriamali uliyenuia hebu
yasahau.
Kitu
kukubwa kwako angalia kule unakokwenda. Makosa ni sehemu pia ya kukusaidia
kufanikiwa kule unakokwenda ikiwa utajifunza. Acha kuamini kwamba utashindwa
kirahisi. Amini utashinda kwa hicho unachokifanya.
Jifunze kila siku. |
2.
Weka juhudi nyingi kila siku.
Anza
siku yako kila siku kwa kujua kwamba unakwenda kuweka juhudi nyingi sana ambazo
kwa vyovyote vile zitakuletea matunda. Jione mshindi kila iitwapo leo. Acha kujiona
mnyonge.
Unapokuwa
mjasiriamali unayejitambua ni lazima uelewe hili kwamba mafanikio yako
yanategemea sana pia kutokana na juhudi unazoziweka. Hakuna kubahatisha ni
kuweka juhudi ndiko kutakapokupa matokeo chanya.
3.
Jifunze na jirekebishe kila siku.
Usiruhusu
kutokujifunza, kila siku jifunze unapokuwa kwenye safari yako ya ujasiriamali. Kuna
njia nyingi za kujifunza kama semina, mitandao na hata kutumia vitabu, hapo
chagua njia iliyo bora kwako na ujifunze kila siku.
Kujifunza
kunakusaidia sana kuchukua taarifa kutoka kwa wajasiriamali waliobobea kutoka
sehemu mbalimbali duniani na kunakufanya na wewe kuzidi kuwa bora. Tumia muda
hapo japo kidogo kujifunza na usiache.
4.
Fuatilia biashara yako kwa ukaribu sana.
Ni
vyema kutambua upo umuhimu wa wewe kuifatilia biashara yako kwa ukaribu sana
kuliko unavyofikiri. Acha kufanya sana biashara yako kwa simu, kuwa karibu nayo.
Hata
pale inapotokea umeajiri watu wengine, hiyo isiwe eti ndio basi kila kitu kimeishia
hapo. Upo ulazima pia wa wewe kufatilia hatua zingine nazo kwa ukaribu zaidi
kila wakati.
5.
Kataa kushindwa mapema.
Kukutana
na magumu katika kitu chochote ni jambo la kawaida. Sasa najua wewe ni
mjasiamali mkomavu jipe ahadi kwamba hata ikitokea magumu vipi, kukata tamaa
mapema lisiwe jambo rahisi kwako.
Kila
wakati ukijifunza kutumia funguo hizi tano za mafanikio katika safari yako ya
mafanikio utafanikiwa.
Endelea
kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama
makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja
tena kwa ukaribu. Kujiunga tuma neno THE
UNIVERSITY OF WINNER’S, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA
KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAF ANIKIO.
Ni
wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.