Jan 13, 2017
Jenga Mahusiano Bora Na Mteja ili Kukuza Biashara Yako.
Habari ndugu msomaji wa makala haya
na msaka mafanikio? Ni matumaini yangu makubwa u mzima wa afya tele na
unaendelea na michakato yako ya kila siku. Kwa upande wangu mimi ni mzima wa
afya tele, naendelea vyema na pilikapilika za kila siku ili kuhakikisha mafanikio
makubwa yanakuwa upande wangu.
Nichukue fursa hii adhimu na kwa moyo
mkunjufu kuweza kukukaribisha tuweze kujifunza kwa pamoja kuhusu ukuaji wa
kibiashara hususani katika suala zima la mahusiano bora kati yako na mteja
wako.
Kimsingi ni kwamba biashara yeyote
ile ni mjumuisho kati ya mfanyabiashara na mteja. Pindi inapotokea mtafaruku
kati yao, mfanyabiashara hali yake huwa ni ngumu kibiashara. Lakini kinyume
chake ni kwamba pindi pawapo na mahusiano mazuri kati ya mfanyabiashara na
mteja, mfanyabiashara huneemeka kutoka kwa mteja huyo.
Lakini Ukichunguza kwa umakini kati
ya mfanyabiashara na mteja utagundua ya kwamba mteja huwa ni mtu wa kujishusha
sana pindi akutanapo na mfanyabiashara katika suala zima la kubadilishana
huduma. Hata ule usemi usemao mteja ni mfalme hukaa kushoto kwa wakati huo.
Ndio maana mteja akienda kununua kitu
fulani atasema naomba kitu fulani na mwisho siku mteja huyo atatoa na hela
licha ya kutanguliza neno. Lakini pamoja hayo wapo wafanyabiashara ambao
wamekuwa wakiwafukuza wateja wao bila wao wenyewe kujua.
Mjali mteja ili ukuze biashara yako kwa uhakika. |
Na kutatokea kwa hali kumesababishwa
biashara nyingi kudolola huku chanzo ikiwa mfanyabiashara mwenyewe. Unakuta
mfanyabiashara hata "biashara kauli" hata siku moja,
Ukichunguza kwa umakini itaniunga mkono kwa hiki ninachosema.
Hivi hujawahi kwenda dukani ukakuta
mhudumu hana muda na wewe? Achilia mbali hilo hivi hujawahi kwenda dukani kwa
ajili ya kupata huduma fulani ukajibiwa vibaya? Bila shaka hilo litakuwa
si geni Kwako. Sasa tujiulize huo usemi usemao mteja ni mfalme upo wapi sasa?
Bila shaka haupo.
Hivyo kwa kuwa unataka kukua
kibiashara huna budi kujenga utamaduni bora na mahusiano mazuri kati yako na
mteja wako. Kwani kutokuwepo kwa mahusiano mazuri ya mteja na mfanyabiashara na
chanzo kikubwa cha kufa kibiashara.
Hapa ndipo ambao huwa nakumbuka
mwalimu wangu wa ‘personal brand’
Charles Nduku siku moja aliwahi kuniambia ya kwamba "ukimuhudumia mteja
mmoja vizuri mteja huyo anauwezo wa kukuletea wateja wapya kumi, lakini
ukimuhudumia vibaya mteja mmoja anauwezo kuwapoteza wateja wapya kumi na
kuwazuia wateja wengine watano uliowazoea. Hapo sasa inakubidi uchague
mwenyewe".
Hapo ndipo nikagundua ya kwamba mteja
mmoja ana thamani kubwa sana katika biashara yako. Hivyo mteja mpya ambaye
atakuja kwako leo kwa ajili ya kupata huduma yeyote ile, hakikisha ya kwamba
humpotezi, kwani mteja huyo ana uwezo wa kuja na wateja wapya wengi endapo
utamhudumia vizuri.
Haya ni baadhi ya maneno ambayo
yatamfanya mteja wako ajisikie vizuri zaidi:
# Karibu sana jisikie upo nyumbani.
# Samahani sijui unahitaji/
tukuhudumie nini.
# Karibu tena kwetu mteja ni
mfalme.
# Asante sana na karibu tena.
# Kwa chochote usisite kuwasiliana
nasi kupitia mawasiliano yetu.
Pia kama una uwezo wa kumpa mteja
wako zawadi pindi anunuapo bidhaa au huduma jaribu kufanya hivyo kwani kitendo
hicho humfanya mteja asihame kwenda kupata huduma sehemu nyingine. Pia kufanya
hivyo humfanya mteja ajione yeye ni wa thamani sana mbele yako.
Nimalizie kwa kusema ya kwamba
Kauli Mbiu Ya Mwaka 2017.
Itakoyokufanya ukue kibiashara ni
"Mjali Mteja"
Endelea kujifunza kupitia
dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama makala hii
imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja
tena kwa ukaribu. Kujiunga tuma neno THE
UNIVERSITY OF WINNER’S, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
Ndimi afisa Mipango Benson Chonya,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.