Jan 11, 2017
Jifunze Mambo Haya Muhimu Ya Mafanikio Yakupe Nguvu Ya Kufanikiwa.
1. Kama unataka kufanya mabadiliko madogo katika
maisha yako ni vyema ukaanza kubadili tabia zako. Ila kama unataka kufanya
mabadiliko makubwa katika maisha yako, anza kubadili imani uliyonayo juu ya
mafanikio. Hapo ndipo mabadiliko makubwa yanapoanzia.
Watu wengi sana wanajaribu kuanza kubadili tabia
zao kabla hawajabadili imani waliyonayo juu ya mafanikio. Kubadili tabia peke
yake hakutakusaidia sana ni lazima kubadili tabia kuambatane na kubadili imani ulionayo juu ya
mafanikio, hapo utaona unafanikiwa sana.
2. Watu wengi katika maisha wanavuta mambo yale sio
wanayoyataka, bali ni watu wa kuvuta mambo kama vile jinsi wao walivyo. Picha
iliyo kwenye mawazo yako ndio inayokupa hicho unachokitaka katika maisha yako
na sio kinyume cha hapo.
Kama unawaza mafanikio muda mrefu, ni wazi
utayapata mafanikio hayo bila shida yoyote. Kama unawaza kushindwa, ni wazi
utashindwa sana katika maisha mpaka utabaki unashangaa.
Jenga picha sahihi ya kile unachokitaka kwenye
mawazo yako na utafanikiwa. Ukiwa huna picha sahihi ya unataka nini maishani
mwako utaishia kushindwa na maisha yako yatakuwa mabaya kila wakati.
3. Acha kuuchanganya ubongo wako kwa kuupa vitu
ambavyo huvihitaji. Kwa lugha rahisi
waza vitu ambavyo unavihitaji katika maisha yako. Tofauti na hapo utakuwa unajichanganya
sana kwa kuufanya ubongo wako ushindwe kuelewa kipi unachokitaka na kipi
hukitaki.
Unataka mafanikio tulia, tambua ni kipi
unachokitaka na ukifanyie kazi hicho kila siku. Ila ukiwa ni mtu wa tamaa mara
unataka hiki mara kile itakupelekea
kupata matokeo ambayo siyo sahihi katika maisha yako na usishangae ukishindwa
kufanikishakaribu kila kitu. kumbuka kila wakati Contradicting desires create contradicting results.
4. Mafanikio makubwa sana utayapata kama unafanya
kitu ambacho unakipenda sana toka moyoni. Ikiwa hukipendi kile unchokifanya
yaani unakifanya kitu hicho kwa kujilazimisha uwe na uhakika, hutafanikiwa
sana.
Hivyo kila wakati pata
muda wa kujiuliza je, ni kitu gani ambacho unakipenda? Kisha baada ya hapo
kifanye kitu hicho kwa nguvu zote. Kumbuka siku zote mafanikio makubwa yanakuja
kwa kufanya kile kitu unachokipenda.
5. Ni rahisi kufanikiwa
na kupata karibu kila kitu unachokihitaji katika maisha yako ikiwa utakuwa
tayari kuwasidia wengine nao kuweza kufanikiwa. Ndio maana mara nyingi watu
wenye mkono wa ‘birika’ si rahisi sana
kuweza kuwaona wakifikia viwango vya mafanikio makubwa.
Jiulize kitu gani
ulichonacho ambacho unaweza ukakitoa na kikawa msaada mkubwa kwa wengine? Kama
kitu hicho unacho hebu kitoe, acha kukaa nacho tu wewe peke yako, washirikishe
na wengine ili kiwe baraka kwenu wote.
6. Kitu kibaya katika
maisha yako ni kule kujishusha na kujiona ni mdogo kumbe wakati hata hauko
hivyo. Wengi wanatabia ya kujishasha sana na kujiona ni kama wadudu kumbe ni
wakubwa sana kuliko fikra zao hizo.
Hebu jiulize ni kwa nini
unajishusha sana na kujiona hufai? Je, unafikiri kuna kitu ambacho umekikosa
hadi ikapelekea ukajiona mnyonge kiasi hicho. Sikiliza hujaumbwa ili uwe
mnyonge au uwe mdogo kama unavofikiri, wewe ni mtu tofauti sana.
Amini unaweza ukapata
mafanikio mara kumi ya hapo ulipo sasa. Unashangaa, ndio unaweza kufanikiwa
zaidi ya mara kumi ya hapo ulipo wala hutakiwi kujiwekea mipako. Kila kitu kinawezekana
kwako ukiweka nia na kuamini, itakuwa.
7. Kila wakati jiulize ni
kwa namna gani kupitia kile unachokifanya utakwenda kubadilisha maisha ya
wengine na kuwafanya wawe watu wa mafanikio. Jitahidi kila siku uwe baraka kwa
wengine. Weka juhudi si za kukusaidia wewe tu ila mpaka kuwasadia wengine pia.
Kwa hiyo unapotafuta pesa
kumbuka zote sio zako, tenga angalau kidogo ambazo unaweza ukampa yule ambaye
hajiwezi. Kama ambavyo nasema mara kwa mara, wakati mwingine mafanikio makubwa
yanakuja kupitia utoaji wako. Je, unatoa kiasi gani kuwasaidia wenye uhitaji
hapo ndipo mafanikio yako yalipo.
8. Sumu kubwa sana
inayowazuia wengi kuwa matajiri ni kung’ang’ania kila kitu kufanya wao. Kama
upo hivyo huwezi kuwa tajiri kwa sababu unakuwa huna uwezo wa kutengeneza faida
ya kutosha peke yake ni lazima uanhitaji msaada.
Ni jambo la muhimu sana
kwa kila mjasiriamali kutengeneza mfumo ambao unakuwa unaingiza pesa hata
kipindi ambacho wewe haupo moja kwa moja. Ukitengeneza mifumo kama hii ni
rahisi kufikia utajiri.
Acha kuniambia habari ya
kuibiwa. Kila biashara duniani ina ‘risk’
zake. Kikubwa jifunze ni kwa namna gani ambavyo unamudu kuweza kutawala hizo
hali hatarishi, kuliko kukaa na kutaka kukumbatia kila kitu, hapo utakwama
sana.
Endelea
kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama
makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja
tena kwa ukaribu. Kujiunga tuma neno THE
UNIVERSITY OF WINNER’S, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA
KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni
wako rafiki,
IMANI
NGWANGWALU,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.