Jan 16, 2017
Chukua Hatua Mapema, Usiruhusu Kufa Na Ndoto Yako.
Hebu
waza upo hospitalini na umelala kitandani ukiwa hoi kusubiri kifo chako. Kila kitu
kuhusu wewe kimeshathibishwa na madaktari kwamba, ni lazima utakufa kutokana na
ugojwa unaokusumbua.
Wakati
ukiwa kwenye kitanda chako cha kifo, ghafla unakumbuka ndoto na mipango ya aina
mbalimbali ambayo ulikiwa hujaikamilisha. Unatamani japo uongezewe muda kidogo
ili ukakamilishe mipango hiyo.
Tuchukulie
hali hiyo ndiyo imekukuta wewe leo,
je,swali la kujiuliza upo tayari kufa na ndoto zako? Jiulize ni ndoto
zipi au kipaji kipi ulichonacho ambacho hupendi kuona ukifa nacho bila
kukufanyia kazi?
Ikiwa
kuna wazo au kitu cha kufanya leo kwa nini usifanye kitu hicho ili kukusogeza
kwenye ndoto zako kuliko kuendelea kusubiri?
Je,
unajua kitu kinachokuzuia wewe na watu wengine pia kuchukua hatua za haraka
kuelekea kwenye ndoto zao?
Chukua hatua mapema. |
Woga.
Kitu
gani hasa kinachokufanya ushindwe kuchukua hatua za kutimiza ndoto zako? Unaogopa
utashindwa. Unaogopa ikiwa utafanya halafu ukashindwa kufanikiwa utachekwa na
watu.
Wengi
utakuta wanaogopa mambo mengi ambayo kiuhalisa yanawarudisha nyuma na kuua
ndoto zao kabisa. Woga ni sumu kubwa sana ya mafanikio kwa wengi.
Hatua
za kufanya kuondoa woga huu.
Hakuna
dawa nyingine ya kushinda woga unaokuzuia ushindwe zaidi ya kuchukua hatua
mapema za kuelekea kwenye ndoto yako.
Kila
nafasi unayoipata itumie vizuri kuhakikisha ndoto na mipango yako inatumia
wakati ukiwa una nguvu.
Ila
ukisubiri sana mambo yameharibika ndio uanze kuchukua hatua utakuwa ni sawa na
mtu ambaye anajichelewesha yeye mwenyewe.
Tekeleza
ndoto na mipango yako kwa malengo huku ukichukua hatua mapema. Usiruhusu kufa
na ndoto zako fanya mambo yako mapema.
Endelea
kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama
makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja
tena kwa ukaribu. Kujiunga tuma neno THE
UNIVERSITY OF WINNER’S, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA
KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni
wako rafiki,
IMANI
NGWANGWALU,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.