Jan 10, 2017
Mambo Mawili Muhimu Kwa Mjasiriamali Wa Sasa.
Asilimia
kubwa ya watu wengi wanaoanza biashara zao, hujikuta wakishindwa mapema hata
kabla ya kuanza kufaidi yale matunda ya biashara zao vizuri.
Yapo
mambo mengi yanayosababisha hali hiyo kutokea ikiwa ni pamoja na hali ya
kiushindani katika biashara, ukosefu wa elimu ya kutosha hasa juu ya kuendesha kibiashara na mambo mengine madogo
madogo.
Lakini
hata hivyo hali hiyo pia ya kushindwa katika biashara mapema bila shaka inatuonyesha
au inatupa picha kwamba hali ya ufanyaji wa
biashara ya sasa hivi sio sawa na ile ya zamani.
Katika
dunia ya sasa ili upate faida nzuri kwenye biashara yako hakuna tena ule
ufanyaji wa biashara wa kimazoea ambao utakupa faida moja kwa moja. Ni lazima
ufanye kazi ya ziada.
Kwa
mfano leo hii, ukianzisha biashara sehemu fulani, usishangae kesho ukaikuta
mtaa wa pili au mkajikuta watu zaidi ya kumi mna biashara ya aina moja katika
mtaa mmoja.
Itumie mitandao ya kijamii vizuri ili ikusaidie uwe mshindi katika biashara. |
Sasa
haya ni moja ya mambo yanayomfanya mjasiriamali mdogo kuweza kushindwa mapema
hata kabla ya kufaidi matunda ya biashara yake na kujikuta ameacha.
Inawezekana
kuna kitu unajiuliza ,ni kitu gani ambacho kinachotakiwa kifanyike? Ni kweli
kabisa upo ulazima wa kila mjasiriamali wa leo kuweza kubadilika na kufanya biashara
kwa kisasa ili kukabiliana na kila hali ya ushindani.
Nina
sema upo ulazima wa kubadilika nikiwa na maana kwamba bila kufanya hivyo, suala
la kushindwa katika biashara litakuwa ni la wazi kabisa na hutaweza kufanikiwa
na kufika mbali sana kimafanikio.
Leo
hii kupitia makala yetu haya nataka nikushirikishe mambo mawili ambayo ambayo
ni ya lazima sana kwa mjasiarimali wa sasa au mjasirimali wa ‘digital’ ili kuweza kufikia mafanikio
makubwa.
Jambo
la kwanza ni tovuti/’website’, kwa mjasirimali wa kileo ni muhimu sana
kutengeneza tovuti yako au blogu ambayo inakuwa inawafikia watu wengi na
kukusaidia kutangaza bishara zako moja kwa moja.
Kama
unaona kufungua tovuti au ‘website’
ni gharama hilo halina shida sana unaweza ukaanza hata na blogu. Kupitia huko
kwenye tovuti ni rahisi sana kuwapata wateja wengi ambao wako mbali na wewe.
Haijalishi
sana ni kitu gani ambacho unauza lakini ni muhimu sana kutengeneza tovuti kwani
ndiyo dunia ya sasa iliko na inataka mabadiliko kama hayo, hivyo ni muhimu sana kuwa nayo.
Mwanzoni
inaweza isifahamike lakini siku zinavyozidi kwenda itajulikana na kuwa sehemu yako
ya kukuzia na kuuzia bidhaa zako muhimu. Lichunguze hili na lifanyie kazi mara
moja.
Jambo
la pili la mjasiariamali wa sasa ni kutumia mitandao ya kijamii kwa faida. Mbali
na mitandao ya kijamii kutumika kama 'kuchati' lakini inaweza ikakuingizia pato
kubwa kama utaitumia kwa faida.
Ni
muhimu sana kuitumia mitandao ya kijamii pia kutangaza biashara zako maeneo
tofauti tofati. Kwa mfano unaweza ukafungua ukurasa wa ‘facebook’ ambao unahusiana na biashara zako tu ambazo unazozifanya.
Pia
kupitia ukurasa wako unaweza ukaweka matangazo na bidhaa zako hapo kwa hali hiyo ni
lazima utajikuta unazidi kukuza biashara yako pole pole kadri siku zinavyozidi
kwenda.
Kama
nilivyoanza katika makala haya ni muhimu sana kwa mjasirimali wa sasa, kutumia
na kutawala mambo hayo mawili yaani tovuti na mitandao ya kijamii ili
kufanikiwa kwa viwango.
Endelea
kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama
makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja
tena kwa ukaribu. Kujiunga tuma neno THE
UNIVERSITY OF WINNER’S, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA
KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni
wako rafiki,
IMANI
NGWANGWALU,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.