Jan 9, 2017
Ili Ufanikiwe, Unahitaji Kuondoa Mambo Haya Kwenye Maisha Yako Kabisa.
Ili uweze kufanikiwa upo ulazima wa wewe kuongeza
maarifa na tabia mpya za mafanikio kila kukicha. Hili ni hitaji la msingi sana
kwa mtu yeyote ambaye ana nia ya kufikia mafanikio makubwa maishani mwake.
Pamoja na ukweli huo ambao hauwezi kupingwa, lakini pia upo ulazima wa kuondoa tabia mbaya
zinazokukwamisha katika safari ya mafanikio. Tabia hizi mbaya ni lazima
kuziondoa ili kuzifanya mpya zifanye kazi vizuri.
Hautaweza kufanikiwa ikiwa kila wakati unaongeza
tabia mpya za mafanikio na kusahau kutoa zile tabia mbaya zinazokukwamisha kwa
namna moja au nyingine katika maisha yako.
Najua zipo tabia ambazo kwa kawaida zinaturudisha
nyuma sana kwenye mafanikio yetu. Hizo ndizo tabia ambazo unatakiwa uziangalie
kwa ukaribu na kuziondoa mara moja kwenye maisha yako.
Kuendelea kuzing’ang’ania tabia hizi ambazo ni
hasi, ni sawa na wewe mwenyewe kuamua kujitengenezea njia au kushindwa kwenye
maisha yako mwenyewe, hivyo ni muhimu sana kuzibadili.
Unataka kujua zaidi ni tabia zipi mbaya unatakiwa
kuziondoa, fuatana nami katika makala haya nikuangazie nukta kadhaa
zitakazokusaidia moja kwa moja kuweza kuondoa tabia ambazo ni sumu kwa
mafanikio yako.
1. Ondoa
visingizio.
Jifunze kuwajibika kwenye maisha yako kwa asilimia
zote. Kama kuna jambo umeshindwa kulifanya kubali tu umeshindwa ila acha
visingizio. Kuendelea kuwa na visingio kila siku hakutakusaidia kitu chochote.
Watu wenye mafanikio kila wakati ni watu wa kuwajibika.
Hakuna kitu ambacho wanasingizia kwamba kimewakwamisha zaidi yao wenyewe. Ukielewa
hili, litakusaidia kupiga hatua na kupelekea kuchukua hatua.
Ondoa woga kwenye maisha yako, ili kujihakikishia mafanikio makubwa. |
2. Ondoa
woga.
Hautaweza kufanikiwa kama ndani yako kila wakati
umejaa na woga. Unapokuwa na woga inakuwa inakufanya ushindwe kujaribu mambo
mengi ikiwa pamoja na fursa zinazoweza kujitokeza. Hakikisha leo unakula kiapo
cha kuondoa woga ili uweze kufanikiwa mara moja.
3. Ondoa
wazo la kufanikiwa upesi.
Mafanikio yote siku zote ni mipango. Mafanikio yanakuja
hatua kwa hatua. Sasa kama una wazo la kutaka kufanikiwa kwa haraka bila kuwa
na subira, huku unakoelekea ni kubaya. Jiwekee mipango, itekeleze kila siku,
utafanikiwa. Hakuna mafanikio ya kulala maskini, na kuamka tajiri. JIPANGE.
4. Ondoa
watu hasi.
Maisha yako yatakuwa ya mafanikio kama utakaa mbali
na watu hasi. Watu hasi ni sumu kubwa sana ya mafanikio yako. Hawa ni watu
ambao watakukatisha tamaa na kukufanya ushindwe kufanikiwa. Kwa hiyo, ni lazima
sana kwako wewe kuweza kukaaa nao mbali ili kujihahakishia mafanikio.
5. Ondoa tabia
ya kukubali kila kitu.
Epuka sana kuwa mtu wa kukubali kila kitu, hata
pale ambapo hutaki kitu fulani. Unapokuwa ‘Mr.
Yes or Mrs. Yes’ kila wakati ni hatari sana kwa mafanikio yako kwa sababu
kuna wakati utajiingiza kwenye makubaliano ambayo hukuyataka.
6. Ondoa
mawazo mgando.
Kila wakati kuwa mtu wa kutaka vitu vipya. Zile fikra
zako kuhusiana na jambo fulani jaribu kuzipima kila wakati, je, kwamba
zinakusaidaia kuweza kufanikiwa? Ukitoa mawazo mgando maishani mwako, utajua
mambo mengi na pia itakuwa ni njia rahisi ya kufanikiwa kwako.
Kumbuka kila wakati kutoa tabia mbaya
zinazokukwamisha ni jambo ambalo unatakiwa kulichunguza sana, ili kuweza kufikia
mafanikio yako.
Uwe na wakati mwema na siku njema katika harakati
zako za kufikia mafanikio makubwa.
Endelea
kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama
makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja
tena kwa ukaribu. Kujiunga tuma neno THE
UNIVERSITY OF WINNER’S, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
Ni
wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,
dirayamafanikio.blogspot.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.