Jan 18, 2017
Ukizingatia Vizuri Maamuzi Haya, Yatabadilisha Maisha Yako Kabisa.
Si
kile kinachokutokea sasa au kile kilichotokea jana ndicho kinachoamua maisha
yako ya kesho yatakuwaje. Kitu kinachoamua maisha ya kesho yakuwaje kipo kwenye
maamuzi yako.
Kwa
sababu ya maamuzi, hapa ndipo unaweza kujua kama kweli unaweza ukafa maskini au
ukafa ukiwa ni mtu mwenye mafanikio. Wengi huwa ni watu ambao hawazingatii sana
kuhusu maamuzi yao.
Kutokana
na maamuzi ieleweke kwamba ndio hupelekea wengine kuwa na maisha mazuri na
wengine kuwa na maisha ya hovyo. Na maamuzi tunayo yazungumzia hapa
yamegawanyika katika sehemu tatu.
1.
Maamuzi ya kile unachokizingatia.
Kitu
unachoamua kukizingatia katika akili yako mara kwa mara ndicho kinachokufanya
ufanikiwe au ushindwe. Huwezi kufanikiwa kama kila wakati unafanya maamuzi ya kuzingatia mambo ambayo hayakusaidii.
Siri
ya kuweza kufanikiwa ipo kwenye kuweka nguvu yote ya mawazo kwa kile kitu
unachokitaka kwenye maisha. Kwa hili hakuna ubishi usipofanya maamuzi hayo huwezi
kufanikiwa.
Fanya maamuzi ya kufanya kilichobora kwako, upate matokeo bora. |
2.
Maamuzi ya kile unachokifanya.
Kila
wakati unahitaji kufanya maamuzi ya kile unachotaka kukifanya. Kile ambacho
umechagua kukifanya hicho ndicho kinachoamua maisha yako kuwa bora au ya hovyo.
Hebu
kila wakati jiulize je, unafanya maamuzi sahihi hasa kwa kile unachokifanya? Au
unafanya maamuzi ambayo hata wewe mwenyewe ukiangalia tena yanakuwa yanakuumiza
kwa namna fulani?
3.
Maamuzi ya jinsi unavyotafsiri mambo.
Pia
yapo maamuzi ya jinsi unavyopokea mambo. Kwa mfano, unapokuwa umeshindwa
kichwani mwako huwa unapokea vipi taarifa hizo au pengine huwa unajisikiaje.
Ili
kufanikiwa jifunze kuchukua maamuzi ya kutafsiri mambo au taarifa kwa chanya
zaidi. Unapokuwa unatafsiri mambo kwa chanya itakufanya uweze kufanikiwa, kwa
sababu utakuwa unafanya maamuzi bora.
Kwa
kifupi, haya ndiyo maamuzi ya msingi sana kwa mtu yoyote anayetaka kufanikiwa. Mafanikio
au kushindwa kwa namna yoyote ile msingi wake mkubwa unatokana na mamauzi hayo
ambayo umejifunza.
Endelea
kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama
makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja
tena kwa ukaribu. Kujiunga tuma neno THE
UNIVERSITY OF WINNER’S, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA
KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni
wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.