Jan 15, 2017
Tiba Na Kinga Asilia Za Maradhi Mbalimbali Ya Kuku.
Linapokuja suala la ufugaji hasa wa kuku kuna wakati
zinahitajika dawa nyingi ambazo
inatakiwa zitumike kutibu kuku mpaka waweze kukua vizuri.
Kuna wakati mfugaji kutokana na hali ya kiuchumi hujikuta hana
pesa ya kununuliwa dawa za kuweza kutibu kuku wake mpaka wapone.
Sasa kitu cha kujiuliza mfugaji huyu anapokosa pesa anafanyaje
wakati kuku wana ugonjwa wa aina fulani?
Jibu ni rahisi tu ni lazima atafute tiba mbadala ili kuwakinga
kuku. Kinga zipi mbadala? fuatana nasi leo hii katika makala haya kujua aina ya
mimea inaweza kutibu maradhi mbalimbali ya kuku.
A. Sehemu za
mimea zinaweza kuwa:-
Majani, Magome, Mbegu, Maua au Matunda
B. Umuhimu wa
kutumia tiba zenye asili ya mimea.
Hupatikana kwa urahisi.
Ni rahisi kutumia.
Gharama nafuu.
Zinatibu vizuri.
Hazina madhara.
C. Baadhi ya
mimea inayotibu Maradhi ya Kuku:
1. Mwarobaini
(Majani, Mizizi, Magome).
Hutibu magonjwa yafuatayo:
Typhoid.
Kuzuia Kideri.
Kuhara.
Mafua.
Vidonda.
Mwarobaini. |
2. Shubiri
Mwitu (Aloe vera).
Chukua majani 3-5 makubwa, katakata na loweka ndani ya maji lita
10 kwa masaa 12 hadi 16. Wape kuku kwa siku 5 - 7.
Isiyotumika mwaga na tengeneza nyingine baada ya masaa 12.
Mchanganyiko huu unaweza kutibu:
Kideri/Mdondo (Mdonde/Chikwemba/Kitoga/Chinoya/Sotoka)
- inyweshwe kabla kwa kinga.
Homa ya matumbo (Typhoid).
Mafua (Coryza).
Kipindupindu cha kuku (Fowl Cholera).
Shubiri mwitu. |
3. Mtakalang’onyo
(Euphorbia).
Chukua Majani makubwa 3-5, ponda, weka katika lita 10 za maji
kwa masaa 12-16, chuja na wape kuku. Isiyotumika mwaga na tengeneza nyingine.
Mtakalang’onyo hutibu:
Kideri/Mdondo (Mdonde/Chikwemba) - inyweshwe kabla kuzuia
Gumboro.
Ndui.
Kuhara damu (Coccidiosis).
Mtakalang'onyo. |
4. Mbarika
(Nyonyo).
Hutibu Uvimbe.
Weka majani ya mbarika ndani ya majani ya mgomba kisha weka
ndani ya jivu la moto, kisha kanda sehemu yenye uvimbe kwa kutumia majani hayo
ya mbarika.
Nyonyo. |
5. Mlonge
(Mlonje).
Ina vitamini A na C.
Chukua majani ujazo wa mikono miwili (gao mbili). Kisha
yapondeponde na kuyaweka katika lita 10 za maji na iache kwa masaa 12-16, chuja
na wape kuku. Isiyotumika mwaga na tengeneza nyingine.
Mlonge hutibu:
Mafua.
Kideri - inyweshwe kabla kwa kukinga
Kipindupindu cha kuku (Fowl Cholera).
Homa ya matumbo
Ini.
Mlonje. |
6. Konfrei.
Ina madini na vitamini nyingi.
Hutibu vidonda na majipu.
Konfrei. |
7. Ndulele (Dungurusi,
Makonde, Tura/Ndula).
Majani hutibu Minyoo.
Matunda hutibu Vidonda.
Ndulele. |
8. Papai
(Majani).
Chemsha magao mawili ndani ya maji lita 6 hadi ubakie na lita 1.
Poza kisha chuja.
Hutibu: Minyoo
Papai. |
9. Mwembe.
Majani magao mawili, ponda na chemsha ndani ya lita 6 za maji
hadi ibaki lita 1. Wape kwa siku moja.
Mwembe hutibu:
Homa ya matumbo.
Mafua.
Kinga ya Kideri/Mdondo.
Embe. |
10. Mpira.
Chemsha majani au mizizi.
Mpira hutibu:
Tumbo
Vidonda na majipu
11. Minyaa
(Cactus).
Hii ni aina yenye majani manene-hadi kufikia nusu nchi na mapana
hadi kufikia upana wa viganja viwili vya mikono.
Minyaa hutibu: (Angalia inaunguza au kubabua).
Vidonda.
Ngozi.
Uzazi.
12. Pilipili Kichaa.
Pondaponda kiasi kisha changanya na maji na wawekee kuku wawe
wanakunywa kwa muda wao. Inasemekana inasaidia kutibu Mdonde (lakini mapema
kabla maradhi kuingia).
Endelea kujifunza kupitia
dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama makala hii
imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja
tena kwa ukaribu. Kujiunga tuma neno THE
UNIVERSITY OF WINNER’S, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
mbna maelezo juu ya kuuandaa muarubaini hamna?
ReplyDeleteMaelezo mazuri nimeyapenda kweli
ReplyDeleteYaaah kazi nzurii
ReplyDelete