Jan 2, 2017
Siri Ya Mafanikio Yako Mwaka 2017.
Habari za muda huu mpenzi msomaji wa makala hii ya DIRA YAMAFANIKIO. Siku ya leo ningependa kuchukua fursa hii niweze kukushirikisha
mambo mbalimbali ambayo yataweza kukuondoa kutoka sehemu moja hadi nyingine ya
kimafanikio hasa mwaka huu wa 2017.
Kwa kawaida yapo mambo mbalimbali ambayo unaweza ukajifunza binafsi hata pia kupitia watu waliofanikiwa. Mafanikio
ya kimaisha huja kwa kuiweka akili yako kuweza kupambana na changamoto za
kimaisha na hatimaye kuona mwanga wa mafanikio.
Naamini una kiu kubwa ya kutaka kuona mwaka 2017 ukiisha ukiwa na mafanikio makubwa. je, unajua siri ya mafanikio yako kwa mwaka 2017 iko wapi?
Naamini una kiu kubwa ya kutaka kuona mwaka 2017 ukiisha ukiwa na mafanikio makubwa. je, unajua siri ya mafanikio yako kwa mwaka 2017 iko wapi?
1. Tazama fursa
zilizopo.
Mpenzi
msomaji wangu wa makala hii jitahidi kuzitazama fursa zilizopo katika eneo lako
unaloishi au nje ya eneo lako unaloishi. Fursa zilizopo ni chanzo kikubwa cha
utajiri wa kimafanikio. Nasema hivi ni kwa na maana ya kwamba fursa mara
nyingine hutoka na changamoto zilizopo eneo fulani, fursa hizi huenda zikawa
aina mbalimbali za mahitaji ya watu.
Ikiwa
bado hujanielewa vizuri naomba nikupe mfano huu. Tuchukulie mtaani kwako kuna tatizo la eneo la kutupa
taka taka unaweza ukachukua kama fursa hiyo na kuanza kupita kwa makazi ya watu
na kuchukua taka hizo na kwenda kuzihifadhi eneo husika na hatimaye wakazi hao
kukulipa kiasi cha fedha . Na vilevile kila changamoto zilizopo eneo furani ni
fursa ya kuweza kupata kipato na hatimaye kuona fursa ya mafanikio.
Mafanikio
yote makubwa huja kutokana na kujiamini wewe mwenyewe na kuua hofu zote
zinazokukwamisha. Unapojiamini unajijengea nafasi nzuri sana ya kufikia
mafanikio yako makubwa. Ni muhimu sana kuweka jitihada zako wewe mwenyewe kuwa
unaweza kufanikiwa huku ukijiamini. Hata kama unachukua ushauri kwa wengine ni
jambo zuri sana lakini kikubwa jiamini.
Ili
uweze kuongeza uwezo mkubwa wa kujiamini ni vyema kuwa na mawazo chanya yenye
kuleta maono ya kufanikiwa hapo baadae. Hakuna dhambi kubwa kama kukata tamaa
jiamini kuwa unaweza ama hakika utafanikiwa maisha siyo magumu kihivyo kama
wengi tunavyofikiri ila sisi ndio wagumu na daima siku zote kitu rahisi ndicho
sahihi.
3. Acha kusikiliza maneno ya watu
wanaokukatisha tamaa.
Wapo
baadhi ya watu ambao wapo kwa ajili ya kuwakatisha watu wengine tamaa. Hivyo basi
kama wewe ni kweli unahitaji mafanikio najua yapo mengi yatasemwa juu yako kwa
ajili ya kukuvunja moyo. Wewe wasikilize tu watu hao lakini achana na mawazo
hasi ambayo hayana tija kimafanikio na sumu kubwa kwako.
Siku
zote jifunze kuwa ni mtu wa kusikiliza mawazo chanya yenye kuleta njia sahihi
ya kuona maono ya kimafaniko. Kuwa makini katika kuchagua marafiki sahihi wenye
mawazo yakinifu yenye kuleta mtazamo wa kimafaniko. Achana na watu wataokurudisha
nyuma kimafanikio kwa namna yoyote ile.
4. Kukabiliana na changamoto
zinazojitokeza.
Tambua
ya kuwa hakuna mafanikio yasiyo kuwa na changamoto.Hivyo jitahidi kuwa ni mtu
kukubaliana na changamoto hizo na kujua namna utakavyoweza kukumbana na
changamoto hizo .Usiwe ni mtu wa kukata tamaa sana.
Vile
vile siri kubwa ya mafanikio ni kujifunza na kutokuogopa kujaribu. Hautaweza
kufanikiwa kwa kukaaa tu na kutokuwa mbunifu na jinsi ya kupambana kimaisha na
changamoto za kimaisha na hatimaye kufanikiwa. Hakikisha unafanya kazi kwa
biidii ili malengo yako yaweze kutimia.
5. Fanya kazi kwa bidii.
Hiyo
ni nguzo kubwa katika mafanikio. Hakikisha unajituma zaidi katika kufanya kazi.Tumia
muda wako vizuri na kwa mapangalio mzuri ili kuhakikisha unapata mafanikio
unayoyahitaji. Tumia ujuzi,nguvu na maarifa uliyonayo katika kufanya kazi.
Ifanye
kazi iwe ndiyo msingi wa mafanikio yako. Mara kwa mara inapotokea unakosa
hamasa ya kufanya kazi, jipe hamasa na kuendelea kuchapa kazi bila kuchoka.
Ukichukua tabia hii, mafanikio makubwa yatakuwa upande wako. Hii ni siri nzuri
sana ya kukufikisha kwenye mafanikio makubwa.
6. Simamia maono yako.
Hakikisha
unasimamia malengo yako uliyojiwekea ili kuona ndoto zako zinatimia kwa muda
muafaka. Maono ni malengo yako ambayo wewe mwenyewe umejiwekea ambayo utapenda
kuyatimiza hapo baadae na kuona unayaona mafanikio. Kumbuka kufanya tathmini ya
malengo yako ni wapi ulishindwa kutimiza malengo yako, na utaweje kukumbana na
changamoto hizo na hatimaye kutimiza malengo yako.
Kwa
kujifunza mambo hayo itakusaidia sana wewe kuweza kufikia mafanikio makubwa
uliyojiwekea katika maisha yako kwa mwaka 2017..
DIRAYA MAFANIKIO inakutakia kila la kheri katika safari yako yako ya kuelekea
kwenye mafanikio.
Makala
hii imeandaliwa na:-
Afisa
mipango na mendeleo,
Mr.
Benson o. Chonya,
Mawasiliano,
Instragram;
Benson Chonya,
Twitter;
@bensonchonya,
Facebook;
Benson Chonya,
Whatsapp;
0757 90 99 42.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.