Jan 12, 2017
Unapokosa Hamasa Ya Kile Unachokifanya, Kumbuka Mambo Haya.
Katika
maisha kuna wakati mwingine pamoja na kuweka juhudi nyingi sana kwa kile kitu
unachokifanya tena kwa muda mrefu lakini unakuwa bado hupati matokeo ya kile
unachokitaka.
Kwa
mfano, utakuta umeweka juhudi kubwa kwa jambo fulani tena kwa muda mrefu ,
lakini hauoni mafanikio makubwa sana. Kwa hali kama hii hukupelekea moja kwa
moja kuanza kukosa hamasa na kukata tamaa.
Kukosa
huko hamasa na hali ya kukata tamaa huanza kujitokeza hasa pale unapoona wale
ambao wanafanya jambo hilohilo tena wakiwa wameanza muda si mrefu wakifanikiwa.
Wengi
wanapokutana na hali kama hiyo ile hamasa ya kufanya jambo hilo hupungua sana siku
hadi siku na mwisho hujikuta kabisa wameachana na jambo hilo kwa kuona eti haliwafai.
Sasa
basi kila wakati kumbuka hamasa ndio chachu kubwa ya kuweza kukufikisha kwenye
mafanikio yoyote yale. Kwa maana hiyo ninachotaka kukwambia kila unapokosa hamasa kumbuka sana mambo haya.
1. Tambua vizuri sababu za kuanza jambo
hilo.
Sina
shaka kabisa zipo sababu ambazo zilipelekea ukaanza hicho unachokifanya. Hebu fanya
zoezi la kuziandika sababu hizo na kuzipitia kila wakati.
Kwa
jinsi utakavyokuwa unazipitia sababu hizo ni rahisi sana kukupa hamasa upya na
kuona haipo sababu ya kukata tamaa kama sababu zako zinajitosheleza.
Kwa
mfano, pengine ulianza jambo hilo ili kuwasaidia wengine. Kama iko hivyo, hiyo
ina maana kukosa kwako hamasa na kukata tamaa kutapelekea hao wengine usiwasaidie.
Kabla hujakata tamaa kumbuka ulikotoka. |
Hivyo, dawa ya kurudisha hamasa hapo ni kwa wewe kuendelea kufanya hata kama matokeo hupati mazuri. Kupitia kujifunza tena na kujua sababu kwa nini ulianza zitapelekea wewe kufanikiwa.
2. Hakuna mafanikio kama unakata tamaa
mapema.
Inawezekana
unakosa hamasa kwa sababu hupati matokeo ya haraka. Unachotakiwa kukikumbuka
hapa mapema ni kwamba Kufikia mafanikio yoyote inahitaji juhudi na nguvu nyingi
tena sio kwa muda mfupi.
Hakuna
mafanikio ambayo unaweza kuyapata kama unakata tamaa mapema. Weka juhudi zako
kwa muda mrefu huku ukijua kupata mafanikio itakuwa ni lazima kwako na itakuwa
hivyo.
3. Acha kujishusha.
Hata
kama hupati matokeo makubwa kama wengine wanayoyapata kwenye jambo unalolifanya
lakini kitu kikubwa cha kuangalia acha kujidharau na kujishusha kabisa.
Unaweza
tena kufanikiwa ikiwa utatumia njia nyingine na kujaribu tena. Mafanikio yanakuja
kwako sio mara moja bali ni kwa kufanya tena na tena mpaka unapata matokeo chanya.
4. Tafuta msaada.
Pia
kama unaona hamasa unaikosa kabisa ni vyema ukatafuta msaada hasa kwa
kuwangalia wale waliofanikiwa kwa kiasi kikubwa hasa kwa hilo jambo ambalo
unalifanya sasa.
Kwa
kuzingatia mambo hayo yaani kujua sababu zilizokufanya ukaanza jambo hilo
unalolifanya, kuacha kujishusha na kutafuta msaada ni moja ya mambo yatakayokusaidia
kurudisha hamasa ya mafanikio yako upya.
Endelea
kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama
makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja
tena kwa ukaribu. Kujiunga tuma neno THE
UNIVERSITY OF WINNER’S, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA
KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni
wako rafiki,
IMANI
NGWANGWALU,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.