Jan 5, 2017
Fanyia Kazi Utajiri Wa Mabonde Haya Ukusaidie Kujikwamua Kiuchumi.
Ni majira ya saa tisa alasiri ambapo
nimekaa kandokando ya ufukwe wa bahari huku nikitazama viumbe mbalimbali ambao
wapo mahali hapa, mara ghafla akili yangu inahama na kuzama katika dibwi
la mawazo, naanza kutafakari ukuu wa Mwenyezi Mungu na uwepo wake katika dunia
hii.
Mawazo yangu yanazidi kuwa makubwa
zaidi nagundua ya kwamba Mungu wetu anatupenda sana kwani ameweza kuviumba vitu
mbalimbali kwa ajili ya matumizi yetu wanadamu. Na vitu hivi ndivyo
vinavyotufanya tuendelee kuishi. Asante Mungu.
Nayatazama maji ambayo kiukweli
yanavutia kwa macho kwani ya rangi ya kupendeza. Naendelea kuyatazama maji kwa mbali naona kuna vitu
ambavyo ndani kuna watu, najaribu kuvichunguza kwa umakini nagundua ni
mashua, mitubwi na natazama mbele naona kuna meli kubwa za mizigo na abiria.
Wakati naendelea kutazama unakuja ule
usemi usemao "shilingi yazama meli yaelea" hapa napata majibu ya kwamba
mwenyezi Mungu ana makusudio yake katika ulimwengu huu hasa kwa sisi waja wake.
Kwani wavuvi hupata pesa kupitia bahari hii, mizigo mbalimbali husafirishwa
kupitia bahari hii na mambo mengi hufanywa kupitia bahari hii.
Nautazama udongo ambapo mi nimekaa
juu yake, kwa macho unavutia sana halikadhalika na upepo uliopo mahali
hapa unasahaulisha matatizo kwa muda. Kweli Tanzania nchi yangu ni nzuri
sana, nilalapo nakuwaza wewe.
Kwani umejaliwa kila aina ya
rasilimali ambazo kiukweli hata sehemu nyingine rasilimali hizi hazipo. Mmmh
kweli jamani najivunia kuwepo katika nchi hii. Pamoja kila aina ya
rasilimali tulizonazo najiuliza mbona hutajafanikiwa sana, ikiwa rasimali
ambazo tunazo ni mtaji tosha? Kwa kweli nakosa majibu sahihi.
Akili yangu inazidi kuwaza huku
nikifikiria zaidi kuhusu rasilimali za nchi yangu ya Tanzania. Nawaza kuhusu
rasilimali ardhi ambayo viumbe vyenye uhai na visivyo na uhai vipo juu yake.
Tanzania yangu imejaaliwa kuwa ardhi
tosha ambayo inafaa kwa matumizi mengi sana ikiwa ni pamoja na
1. Makazi
2. Kilimo
3. Majani kwa ajili ya malisho
4. Ardhi kwa ajili ya kujenga huduma
za jamii.
5. Ardhi kwa ajili ya kutengeneza
miundo mbinu kama barabara.
Pamoja na matumizi mengineyo.
Pamoja na matumizi mbalimbali ya
ardhi tuliyonayo, kwa kuwa nchi yetu idadi kubwa ya watu wake huishi kijijini
na idadi kubwa ya watu hao hutegemea zaidi kilimo na ufugaji kama shughuli za
kiuchumi. Pamoja na yote hayo mbona tunalalamika umaskini, pamoja na
njaa. Hivi tunakwama wapi wakati hakuna foleni na rasimali ardhi
ipo ya kutosha?
Lakini pamoja na hayo kiukweli ni
lazima tuweze kuitumia vyema rasimali ardhi ili tuweze kukua kiuchumi kupitia
kilimo.
Zipo pia pamoja na sera mbalimbali
zinazoeleza kuhusu kilimo tangu kipindi cha miaka ya nyuma mpaka hivi sasa hii
ikiwa ni pamoja na " sera ya kilimo cha siasa, kilimo cha kufa na
kupona, kilimo ni uti wa mgongo pamoja na sera ya kilimo kwanza.
Sera hizo zote zimekuwa zikifanya
kazi katika kuhakikisha watanzania waamini katika kilimo, hasa katika ukuaji
huu wa kiuchumi. Nazidi kuwaza na kuwazua kuhusu kilimo cha Tanzania nakosa
majibu sahihi.
Kwani ikiwa tunasema kilimo kwanza ni
jitihada gani ambazo zimekuwa zikifanywa kuweza kukuza kilimo hiki? Kwani tangu
miaka ya nyuma tunatumia jembe la mkono pamoja na mvua.
Pamoja na kuendelea kuisubiria mvua
hii kuna wakati mvua zinagoma kunyesha huku njaa ikiendelea kumtawala . Wapo
wale ambao wanaona mvua hazinyeshi wanadiliki kusema hata mvua zipo kwenye
uhakiki. Mmmh sijui ni kweli mvua zinahakikiwa nazo?
Mawazo yangu yanakuja na jibu mvua
hazihakikiwi ila kutoka tumezoea kufanya kilimo kwa mazoea kwa kutegemea mvua,
pale ambapo mvua hizi kutoka na mabadiliko ya tabia ya nchi zinashindwa
kunyesha tunajikuta tunashindwa kuendana na mazingira.
Mwisho wa siku tunajikuta tunatangaza
njaa. Mmmh jamani! Ni kweli kutokunyesha kwa mvua kunasababisha njaa?
Kwa majibu ya haraka utasema ni ndio. Lakini ukweli ni kwamba pamoja na kuwepo
kwa uwepo ya vijito, mito mabwawa na visima hivi kweli tumeshindwa
kufanya kilimo cha umwagiliaji? Usinipe jibu
Bila shaka naamini tunaweza kufanya
kilimo cha umwagiliaji kwani tanzania yetu imebarikiwa kuwa na mito mingi
lakini haina faida kwa wananchi wake kwa asilimia kubwa. Ifike mahali Serikali
ijenge miundombinu ya mabomba ya umwagiliaji ikiwapelekea wananchi kwenye
mashamba na wao watalima bila kutegemea mvua.
Kwani hapa Tanzania yapo mabonde
yaliyopo huko Kilombero Malindi,, mvumero, Kilosa mbarali, Isimani,
songea, rukwa, Tanga na sehemu nyinginezo ambazo kilimo kama hiki
kinaweza kufanywa na watu tukaneemeka kwa kilimo hiki bila kutegemea mvua. Jiulize,
utajiro wote ulioko kwenye mabonde haya tunaufanyia nini?
Kipo pia kilimo cha matone ambacho
hakihitaji uwepo wa mvua. Kama ndivyo hivyo ni kwanini tutangaze njaa?
Bila shaka majibu ya kutangaza njaa kwa mkoa wowote ule ni kwamba tumezoea
kuishi kimezoea. Nafikiri wizara husika ikishirikiana wakuu wa mikoa, wilaya
pamoja na wataalamu wa kilimo waweze kuona umuhimu juu ya hili. Ilikuwa
kufikia malengo ya kilimo ya mwaka 2025.
Kama endapo tutashindwa kushirikiana
kwa pamoja juu ya mbinu mbadala kwa ajili ya ukuzaji wa kilimo katika nchi yetu
tutaendendelea kuishi katika maisha yale yale kila wakati. Najua
mapinduzi ya kilimo yanawekana. Tanzania pamoja na rasimali ardhi tuliyonayo
tunauwezo mkubwa sana wa kuweza kuwasaidia mataifa mengine. Kwa kuuza mazao ya
biashara ambayo tutayazalisha mahali hapa.
Mawazo yangu kwa leo naomba yaishie
hapa, ila kila mmoja wetu kwa hayo niliyoyaeleza yakamguse huku tukitegemea
yakaleta "mapinduzi makubwa ya kilimo". Kwani najua kila kitu
kinawezekana tena kwa asilimia mia moja. Kizazi kijacho matumizi ya mvua
pekee na jembe la mkono libakia historia kama matumizi ya zana za mawe.
"kabla jua halijazama natumaini
ya kwamba tutaleta mapinduzi ya kilimo" kila mmoja afikirie juu kufanya
mapinduzi ya kilimo
MUNGU IBARIKI TANZANIA WABARIKI NA
WATU WAKE.
Ni wako mkeleketwa wa maendeleo na
mafanikio Afisa Mipango Benson chonya,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.