Oct 1, 2017
Changamoto Ulizonazo Sio Sababu Kubwa Ya Wewe Kushindwa.
Moja
ya tatizo kubwa walilonalo watu wengi hasa linapokuja swala la kutafuta
mafanikio, ni kule kuchukulia changamoto ni kizuizi kikubwa sana cha kuweza
kufanikiwa kwao. Utakuta mtu anaposhindwa jambo atakupa sababu au changamoto
nyingi sana zilizomfanya ashindwe.
Ni
kweli sikatai changamoto hizo zinaweza zikawa ni nzuri na za kweli kabisa kwao,
lakini je, hiyo hasa ndio sababu ya kushindwa kwao kwa watu hao? Au je, kila
anayefanikiwa ni mtu ambaye hana changamoto kabisa na wanaoshindwa ndio wana
mzigo mkubwa wa changamoto maishani mwao?
Ukifanya
uchunguzi utagundua kitu hiki, hizo changamoto ambazo zimekuwa zikitajwa sana
kama ndio sababu zimekuwa zikitumiwa kama kisingizio tu cha kushindwa kufanikiwa
kwao. Lakini ukweli sababu kubwa ya kushindwa kufanikiwa zipo ndani mwao
wenyewe na si kinyume cha hapo.
Pengine
wamekuwa wakishindwa kufanikiwa kwa sababu ya tabia zao mbovu au kukosa
kuwajibika au hata wamekuwa wakishindwa kufanikiwa kwa sababu ya kukosa maarifa
sahihi ya mafanikio. Hivi ni vitu vidogo vinavyoweza kumfanya mtu akashindwa
lakini kwa sababu ya kutokujua akasingizia changamoto tu.
Ukiangalia
miongoni mwa watu wenye mafanikio, wanafanikiwa sana si kwa sababu hawana
changamoto au vizuizi vinavyowazuia kufanikiwa, bali wanafanikiwa kwa sababu
wanaweza kupambana na changamoto hizo na kuzishinda. Kuendelea kung’ang’ania
kukabiliana na changamoto ndiko kunakowasaidia.
Kila
siku watu hawa wamekuwa ni watu wakuchukua hatua kwenye zile changamoto zao,
bila kujali changamoto hizo ni ndogo au kubwa na kwa kufanya hivyo imekuwa
ikiwasaidia sana kuweza kuwa washindi kimafanikio. Watu hao waliofanikiwa si
watu wa kulialia ni wanapambana na changamoto zao kweli.
Unaweza
ukajiuliza mwenyewe changamoto zako ni zipi zinazokuzuia ushindwe kufanikiwa?
Je, unaziona changamoto hizo ndio kama kizuizi kikubwa kabisa cha kukufanya
ushindwe kufanikiwa? Au unapokutana na changamoto ni kitu gani hasa ambacho
unakuwa unakiwaza sana?
Labda
nikukumbushe tu hivi, kila mtu aliyepo duniani anakutana na changamoto kwa wakati
wake, lakini wanapigana na kuzishinda. Kama changamoto zingekuwa ndio sababu
kubwa ya kushindwa, basi hakuna mtu ambaye angekua kafanikiwa duniani, kila mtu
angekuwa kashindwa.
Sasa
jiulize ushindi unakujaje katikati ya changamoto? Ushindi unakuja kwa kuendelea kupambana na changamoto lakini pamoja na kuongeza juhudi zaidi na zaidi. Na huo ndio ukweli, bila changamoto huwezi kukua sana, lazima changamoto ziwepo ili zikukomaze na kukupa nguvu ya kusonga
mbele kwa kishindo kikubwa.
Kwa
hiyo unapokutana na changamoto yoyote usihuzunikie au kulia. Tafuta njia ya
kuondokana na changamoto hiyo hadi kufanikiwa. Kama usipotafuta njia hiyo huwezi kufanikiwa. Kila
kitu unachokifanikisha ukumbuke kina changamoto zako. Kama hilo lipo pigana na
changamoto zako uwe mshindi na usizifanye zikawa sababu ya kushindwa kwako.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.