Aug 30, 2018
Tabia Za Kiutendaji Zinazowatofautisha Matajiri na Maskini.
Leo nitazungumza na wewe kuhusu tabia kuu ambazo huwatofautisha watu waliofanikiwa na wale wasiofanikiwa, hivyo naomba ukae mkao wa kula kwani chakula hiki ni adimu sana pia ni maalum sana kwako wewe msakatonge mwenzangu.
Sababu kubwa ya watu wengi waliofanikiwa na ambao
wanaishi ndani ya ndoto zao ni kwamba watu huamini sana kile ambacho
wanakifanya. Kuamini kile wanachokifanya ndicho kilichowapelekea watu hao
waendelee kuishi ndoto zao kila jua lichomazapo.
Sababu nyingine ambayo inawafanya watu wenye mafanikio
waendelee kufanikiwa ni kwamba watu hao mara baada ya kuona changamoto fulani
wao walitafuta njia ya kutafuta majibu ya changamoto husika.
Hiyo ni kwa upande waliofanikiwa, ila unapokuja upande
huu mwingine ni kwamba watu wengi wameshindwa
kuziishi ndota zao kwasababu, mosi ni kwamba watu hao huwa hawamini kile
ambacho wanakifanya.
Hivi hujawahi kukutana na mtu fulani kisha akakwambia
nafanya jambo hili kwa kujaribu tu? Bila shaka utawakuta umeshawahi kukutana na
watu wengi wenye kauli kama hizi. Ukichunguza kauli kama hizi utagundua bayana
ya kwamba ni wazi kabisa watu hawa hata kile wanachokifanya hawakiamini, kwa
mtindo huu mafanikio yapo kweli?
Pamoja na kutoamini kile wanachofanya lakini pia watu
hawa ni wazuri sana wakutafuta sababu, na sababu hizi ni zile zisizokuwa na
msingi yaani watu hawa ni wazuri sana kwa kutafuta visingizio.
Ukimuuliza hivi kwani hujafanya hivi? Mtu huyo atakuja na
majibu ya kwa sababu ya.........., majibu ya kwa sababu mara nyingi katika
safari ya mafanikio huwa si ya majibu ya msingi bali huwa ni majibu ya kujikatiza
tamaa tu.
Hivyo ndugu yangu kama ni kweli unataka mafanikio ya
kweli unatakiwa kufahamu ya kwamba kama
kweli umeamua kufanya jambo fulani wewe
fanya ila kama hauhitaji mafanikio basi endelea kutafuta sababu za kutofanya.
Mpaka kufikia nukta hiyo sina la ziada nikutakie siku
njema na mafanikio mema.
Ndimi: Afisa Mipango
Benson Chonya.
Aug 29, 2018
Faida Tatu Muhimu Za Kuchukua Hatua Kwa Kile Unachotaka Kukifanya.
Ili kufikia mafanikio yako, kuwa na mipango mizuri au mikakati iliyobora ni jambo zuri sana ikiwa kama utachukua hatua. Kama usipochukua hatua mipango yako hiyo mizuri haitasaidia kitu itakuwa ni sawa na kazi bure.
Kitu
cha msingi kwako ili mipango yako ieleweke ni kwa wewe kuchukua hatua mapema za
kukusaidia kuweza kutimiza ndoto zako. Zipo faida za wewe kuchukua hatua kwa
kile unachotaka kukifanya, haijalishi umefanikiwa kwa jambo hilo au hapana.
Elewa
hivi, mbali na faida kubwa ya kufanikisha lengo husika la kile unachotaka
kukifanya, lakini zipo faida nyingine tatu muhimu, ambazo
tu wewe utazipata kama utachukua hatua ya kufanya. Faida hizi huwezi kuzipata au kuziona mpaka uchukue hatua.
1. Utawajibika zaidi.
Kile
kitendo cha wewe kuchukua hatua tu, kitakufanya wewe kuwa mtu wa kuwajibika
zaidi tofauti na ambavyo kama usingeweza kuchukua hatua. Najua hutataka mambo
yako yaende hovyo ila utawajibika na kujituma sana ili ufanikiwe.
Hiki
ndicho kitu cha kwanza au faida ya kwanza ambayo utaipata endapo utachukua
hatua. Utashangaa jinsi unavyopata shauku ya kuendelea kutaka kufanya zaidi na
zaidi ukumbuke yote hayo hayaji kwa bahati mbaya ila ni kwa wewe kuchukua
hatua.
2. Utajifunza kutokana na makosa.
Hauwezi
kujifunza kutokana na makosa kama haujachukua hatua. Kuchukua hatua ni lazima
ili ujifunze kutokana na makosa yako yaani ujue ni wapi ulipokosea na ni wapi
unatakiwa kupaboresha zaidi na zaidi hadi uweze kufikia lile lengo lako.
Wengi
wanaoshindwa kufanikiwa sana hawachukui hatua na ni watu wa kusitasita sana na
kwa sababu hiyo inawafanya washindwe kujifunza kutokana na makosa yao. Chukua hatua
leo, uone jinsi utakavyojifunza kutokana na makosa yako.
3. Utapata msaada wa ziada.
Kutokana
na kile ambacho umeamua kukifanya na umeamua kuchukua hatua, hiyo itakusaidia
sana kuweza kupata msaada kwa watu wengine ambao hukutegemea. Msaada huo huwezi
kuupata kama umejikalia tu na huchukui hatua.
Kama
unafikiri nakutania chukua hatua leo, halafu uone kama utakosa watu wa
kukusaidia kwa lile lengo lako. Unakosa watu wa kukusaidia kufanikisha kwenye
lengo lako kwa sababu hujachukua hatua. Ukichukua hatua watu hao utawapata.
Hizi
ni faida tatu nyingine muhimu ambazo utazipata kama utachukua hatua ya kufanya
jambo lile unalotaka kulifanya. Je, hapo ulipo unasubiri nini kuchukua hatua. Chukua
hatua za kuwajibika ili utimize ndoto zako mapema.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama
wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa
vifaranga wa kuku aina ya KUROILER,
SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao
kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na
wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Aug 27, 2018
Huu Ndio Ukweli Unaouma Utakaofanya Maisha Yako Yawe Bora.
Ni jambo la kawaida kwa watu wengi kuwa na ndoto na malengo, lakini ipo tofauti kubwa sana kati ya watu ambao wanafanikisha malengo yao na wengine wanashindwa kufanikisha malengo yaani hawa wanakuwa wanaota tu pasipo kufikia malengo.
Kwa nini
hali hii inakuwa inatokea wengine wanakuwa na uwezo wa kufanikisha malengo yao
na wengine wanakwama kufanikisha? Hapa ndipo unatakiwa ujue ukweli mgumu,
ukweli unaouma ambao utafanya maisha yako yawe bora.
Je,
nikuulize hapo ulipo upo tayari kuupokea ukweli mchungu ambao utabadilisha
maisha yako? Kama uko tayari nyosha mkono, nikupe ukweli huu, ila mara baada ya
kupokea ukweli huo, utakusaidia sana kukubadilisha maisha yako kwa ujumla.
1. Hatua ya kwanza ni ngumu
kutekelezeka.
Inaeleweka
siku zote ili kufanikisha jambo lazima kuchukua hatua. Hata hivyo kwa bahati mbaya
sana siku zote hatua ya kwanza mara nyingi inakuwa ni ngumu sana kuweza
kutekelezeka. Kama usipoweka juhudi na kujituma sana huwezi kuchukua hata hatua
ile ya kwanza. Kuna watu wanakuwa wanakwama hata kabla hawajachukua hatua ya
kwanza. Fanya ufanyalo, tumia nguvu zote na kuhakikisha unaanza.
2. Wewe ndie sababu ya kujirudisha nyuma
sana.
Hakuna
mtu mwenye mchango mkubwa sana wa kukurudisha nyuma zaidi yako. Unajirudisha nyuma
kutokana na hofu ambazo unazo, unajirudisha nyuma kwa sababu ya kushindwa
kuchukua hatua mapema na pia unajirudisha nyuma kwa sababu ya visingizio. Unatakiwa
uyaepuke haya yote ili ufanikiwe.
3. Mambo makubwa yanataka muda na juhudi
ili kuyafanikisha.
Hakuna
jambo kubwa ambalo unaweza ukalifanikisha kwa haraka na upesi kama unavyotaka. Siku
zote mambo makubwa yanataka muda na juhudi kubwa sana ili yaweze kutimia. Kama una
haraka zako na hutaki kuweka muda katika kutimiza makubwa, utaishia kupata vitu
vidogo sana maishani mwako.
4. Sio kila mtu yupo tayari kukusaidia.
Pamoja
na kwamba unaweza ukaona unazungukwa na watu wengi wema, lakini nikwambie tu
unapopata changamoto si kila mtu yupo tayari kukusaidia kufanikiwa na kufika
juu. Wapo wengine watakudidimiza chini na hutaamini, ili usitape tabu weka
akilini hii, si kila mtu yupo tayari kukusaidia kama unavyofikiri wewe iko
hivyo.
5. Huwezi kufanikiwa bila kujitoa mhanga.
kama
unafikiri utafanikiwa tu kirahisi pasipo kuhatarisha baadhi ya mambo basi
utakuwa ni mtu ambaye unajidanganya sana. Lazima ifike muda au wakati uhatarisha
baadhi ya vitu kwa ajili ya mafanikio yako. Hatari haziwezi kutoka kabisa ila
kama unafikiri mafanikio ya namna hiyo yapo huwezi kuyapata katu maishani.
6. Huwezi kutawala kila kitu.
Ukweli
huu unakuja hasa pale unapotaka kutawala tabia na matendo ya watu. Huwezi hata
siku moja kutawala tabia na matendo ya watu. Vipo vitu unavyoweza kutawala
lakini si kutawala tabia zao na ukazimiliki kwa jinsi wewe unavyotaka iwe. Tawala
yale unayoyaweza lakini si kutawala kila kitu utashindwa na hautaweza kufanya
hivyo.
7. Huwezi kufanya kila kitu mwenyewe.
Kama
ambavyo huwezi kutawala kila kitu wewe, basi huwezi kufanya kila kitu mwenyewe.
Yapo majukumu inabidi uwaachie watu wakusaidaie, vinginevyo ukiwa wewe kama
wewe yatakushinda. Wale wanaong’ang’ania kufanya mambo yao peke yao wanashindwa
kutoka au kuweza kufanikiwa kabisa kwa sababu ni ngumu hiyo.
8. Kukosea ni lazima.
Huwezi
ukafanya jambo lolote pasipo kufanya makosa. kukosea ni lazima kutokee kila
wakati unapoelekea ndoto zako. Na kunapotokea kukosea kwa namna yoyote
usichukie, amua kujifunza kupitia kukosea huko ambako unashindwa na si kuchukia
na kuona kila kitu ndio kimeishia hapo na huwezi kufanikiwa tena.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama
wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa
vifaranga wa kuku aina ya KUROILER,
SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao
kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na
wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Aug 26, 2018
Jinsi Unavyoweza Kuboresha Maisha Yako Hatua Kwa Hatua Kila Siku.
Kuboresha maisha yako kila siku na kwa kidogo kidogo ni jambo la muhimu sana kwako kuliko kuharibu maisha yako kila siku hata kama ni kwa kidogo pia. Kuboresha maisha yako kila siku ni jambo la muhimu sana kulifanya.
Unapoanza kufikiria juu ya
kuboresha maisha yako, acha kuwaza juu ya kuchukua hatua kubwa sana itakayoleta
matokeo ya ghafla na ya kushangaza
wengi. Unachopaswa kufikiria ni kuleta mabadiliko ya kila siku hata kama
ni kidogo.
Kwa mfano, kubadilisha
maisha yako kwa asilimia moja kla siku ni kitu ambacho unaweza usikione kina
faida, lakini ukifanya mabadiliko hayo kila siku na kwa muda mrefu mabadiliko hayo
huanza kuonekana tena kwa uwazi.
Hapo unaona kilicholeta
utofauti ni yale mabadiliko kidogo kidogo na maamuzi kidogo sana na ndivyo
unabadilisha maisha yako na kuwa ya tofauti na kuwaacha watu wengine
wakikushangaa eti ulifanyaje hadi hayo yakatokea.
Kama kuboresha maisha yako
kila siku ni jambo la mujimu na ambalo linaweza kukufikisha kwenye kilele cha
mafanikio, je, ni kitu gani kifanyike ili uwe na uhakika wa kuweza kuboresha
maisha yako hatua kwa hatua na kila siku.
1.
Fanyia kazi zaidi mambo yaletayo matokeo chanya.
Usijajidanganye kufanya
mambo ambayo hayakupi matokeo mazuri. Yale mambo yanayoleta matokeo mazuri
yafanye zaidi. Hata kwenye mpira kikosi kinacholeta matokeo bora hicho ndicho
kinachopangwa kila wakati.
Kaa chini na angalia ni
mambo gani ambayo yanaleta matokeo mazuri kwako na yafanye mambo hayo kila
siku. Nasema hivi, usipoteze muda wako kufanya mambo ambayo hayakupi matokeo
chanya, utakwama, kabisa.
2.
Epuka kufanya makosa madogo madogo yasiyo ya lazima.
Unaweza usione matokeo yake
kwa sasa, lakini makosa madogo madogo yanaathari kubwa sana katika kujenga au
kuharibia maisha. Unatakiwa kujua kuepuka kupoteza pesa ndogo ulizonazo, muda
kidogo ulionao na kila siku.
Kwa kadri jinsi unavyomudu
kuepuka kufanya makosa madogo madogo, ambayo kwa dhahiri hayawezi kukupa
matokeo chanya, ndivyo unajikuta upo kwenye wakati sahihi wa kufanikiwa. Makosa
madogo au ‘tinny losses’ ni lazima
kuyaepuka.
Kwa kuepuka kufanya mambo
yasiyo leta matokeo na pia kuepuka kufanya makosa madogo madogo kila siku
utajikuta unaboresha maisha yako na mwisho wa siku utajikuta unatengeneza maisha
yako na kuwa bora zaidi na zaidi.
Kikubwa ambacho unatakiwa
kukumbuka hapa, ni kuamua kuvaa jukumu la kuboresha maisha yako kila siku.
Ukiamua kuboresha maisha yako na kwa kila siku uwe na uhakika utafanikiwa hata
kama mabadiliko hayo hayaonekani leo, kesho yataonekana.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama
wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa
vifaranga wa kuku aina ya KUROILER,
SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao
kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na
wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Aug 25, 2018
Mambo Matano (5) Muhimu Yatakayokusaidia Kufikia Kilele Cha mafanikio Yako
Siri
kubwa iliyopo katika kuyafikia mafanikio yako ipo katika kuzifahamu mbinu
zitakazokusaidia kuweza kuyafikia mafanikio hayo. Wengi tumebweteka kimwili na
kiakili huku tukizani labda mafanikio chanzo chake huwa ni bahati nasibu, uchawi na mengineyo mengi
yasiyokuwa na ukweli wowote ndani yake.
Hata
hivyo ukweli ni kwamba yapo mambo muhimu ambayo yatakusaidia kuweza kufikia
kilele cha mafanikio, na mambo hayo ni:
1. Chukua hatua kila siku.
Mafanikio
ni mchakato usiokuwa na mwisho, hivyo basi kwa kila kitu ambacho unadhani
kinakupa mwanga wa kuelekea kwenye kutimiza malengo yako ni vyema ukachukua
hatua za utekelezaji wa jambo hilo.
Watu
wengi sana ni wazuri sana wa kuwaza mambo mengi sana ya msingi ila linapokuja
sula la kuchukua hatua wamekuwa ni watu wavivu sana wakuweza kufanya hivyo na matokeo
yake watu hayo wamekuwa wakijitengenenezea ukata wao wenyewe. Hivyo kila wakati
jifunze kuchua hatua sahihi kwa kile unachokifanya au unachotaka kufanya.
2. Jifunze kuweka viupambele.
Kazi
yeyote inayofanywwa isiyokuwa na
vipaumbele ni uchafua, kama ulivyo uchafu mwingine, unashangaa wala usishangae
huo ndio ukweli.
Watu
wengi wanashindwa kutuliza kiu ya umaskini hii ni kwa sababu watu hao
wameshindwa kutambua ni kwa namna gani wanaweza kupanga viupembele kwa vile
vitu wanavovifanya.
Kupanga
vipaumbele humsaidia mtu husukia kufahamu na kutambua ni kazi gani ianze
kufanyika na ipi ifuate. Hivyo kama kweli umeuchoka umaskini jifunze kupanga
vipaumbele kwa vitu unavyofanya kwa kuangalia nini kianze kufanyika, lini na
kwa wakati gani.
3. Jifunze kuyaweka malengo yako katika
nyakati.
Malengo
uliyonayo ni lazima uyaweke katika nyakati kabla hujaanza kufanya, na nyakati
hizi ni lazima uwe ni wakati uliopo na wakati ujao.
Jambo
hili linahitaji maamuzi magumu, yaani amua kwamba jambo hili ni lazima
nitafanya wakati huu au aumua jambo hili ni lazima nitalifanya muda fulani.
Katika kipengele hiki ugopa sana tabia ya kugharisha kufanya kwani ndiyo
inayoendelea kukuua taratibu bila wewe kujua.
4. Andika kila kitu ulichokifanya au
unachotaka kufanya.
Kuandika
mambo yako uliyoyafanya au unayotaka kufanya humpa mtu hamasa za kiutendaji
kwani mara kwa mara anakuwa anakumbuka ni kitu natakiwa kufanya na kwa wakati
gani? .
Ogopa
kufanya mambo ya msingi kwa kukurupuka kwani hii ndiyo ambayo husababisha watu
wengi kutokufanya maumizi sahihi. Hivyo kila nyakati jifunze kuweka kila kitu katika maandishi ili uweze kujijengea fikra
thabiti.
5. Fahamua kile unachokitaka.
Maisha
sio bahati nasibu bali maisha ni vile unavyotaka kuwa na muamuzi wa mwisho ni
wewe, hivyo kaa chini na tafakari kwa makini ni nini hasa unachokitaka kisha
uanze kuchua hatua stahiki juu ya jambo hilo.
Lakini
pia ikumbukwe kufahamu kile unachokitaka pasipo kuchukua hatua za kiundeji ni
sawasawa na bure, hivyo amua sasa kubadilika kwa kuchukua hatua za kiutendaji
kwa kile unachokifanya.
Mwisho
naomba nihitimishe kwa kusema ya kwamba endapo ukiyazingatia hayo yote
niliyokwisha yaeleza jiandae kuishi maisha yenye tija katika hii dunia.
Ndimi Afisa Mipango Benson Chonya
Aug 24, 2018
Hii Ndiyo Kanuni Ya Mafanikio Iliyosahaulika Na Wengi.
Mafanikio hayatengenezwi na kanuni moja tu, bali ni mjumuiko wa kanuni za kimafanikio tofauti tofauti na hizi ndizo ziletazo mafanikio. Zipo kanuni za wazi kabisa za kimafanikio ambazo zinafahamika na wengi na zipo ambazo hazifahamiki.
Kwa mfano,
kufanya kazi kwa bidii, kuwa na nidhamu, kutengeneza nguvu ya uzingativu,
naweza kusema ni moja ya kanuni za mafanikio au misingi ya mafanikio ambayo
inaeleweka na wengi kwamba ukiifata lazima ufanikiwe.
Hata
hivyo inabidi ieleweke hivi, zipo kanuni nyingi za kimafanikio ambazo unatakiwa
uzifanyie kazi sana ili ufanikiwe, na kwa bahati mbaya zipo ambazo huzijui au
umezisahau kwa kutokujua lakini zipo na zinafanya kazi kwa matokeo makubwa.
Na mojawapo
ya kanuni rahisi ya mafanikio ambayo wengi hawaijui au wameisahau, ni
kanuni ya kuwa na shukrani. Inaeleweka kwamba kwa mtu yeyote ambaye ana
shukrani, na huku akawa ni mtu wa kuchukua hatua kufanikiwa ni lazima kwake.
Sasa
linakuja tatizo la watu wengi ni wabinafsi na hawana shukrani, kama unafikiri
natania nianze na wewe, je, wewe ni mtu wa shukrani, je, wewe ni mtu wa
kukumbuka kule ulikotoka na kushukuru hapo ulipo na kwa maisha uliyonayo.
Mara
nyingi utakuta watu wengi hawana shukrani sana, si watu wa kukumbuka watu wale waliowasaidia
na wapi, hata kama ni kwa kidogo na matokeo yake wanajikuta ni watu ambao
wanaiweka kanuni hii pembeni na mwisho wake hushindwa kufanikiwa sana.
Kama
nia yako ni mafanikio makubwa kweli, pia unatakiwa kuchukua shukrani kama mojawapo
ya kanuni ya kimafanikio. Kila wakati unapochukua hatua za kiutendaji, lakini hakikisha shukrani iwe karibu na kinywa chako
kwa chochote kitakachotokea.
Kuna
watu wana midomo kama ya ‘laana’
wanapochukua hatua, kwa mfano kufanya biashara ya aina fulani halafu wakapata
hasara, midomo yao inakuwa inaongea mengi sana na kulalamika, sasa hii sio
nzuri na haikusadii, shukuru kwa chochote.
Unaweza
ukawa upo kwenye wakati mgumu shukuru kuna kitu cha kujifunza, unaweza ukawa
umepata hasara kweli shukuru, hii ni kanuni ya kimafanikio na ambayo pia ni
kanuni ya kiroho, pasipo kushukuru mambo yako hayawezi kwenda sawa saana.
Inawezekana
sasa unajiuliza nashukuru kwa mambo yapi, hilo lisikupe tabu. Yapo mengi sana ambayo
unaweza ukaanza kuwa na shukrani nayo lakini kwa kuanza tu, unaweza ukaanza na
kushukuru kwa mambo haya na yatakusaidia sana kufanikiwa.
1. Shukuru kwa uhai ulionao.
Kwa
sababu ile tu unaishi, kwa sababu ile tu umepewa uwezo wa kuishi unatakiwa
kushukuru sana kwa hilo kwanza. Amka asubuhi na sali kwa kwa sababu umepewa
uwezo wa kuishi na muumba wako na hicho ni kitu kizuri sana.
Kitendo
cha kushukuru kwa uhai ulionao kitakupa nguvu hata ya kutenda mambo mengine
makubwa maishani mwako ambayo moja kwa moja yatakusaidia kuweza wewe kufanikiwa
kwenye maisha yako moja kwa moja.
2. Shukuru kwa afya yako.
Tofauti
na kushukuru juu ya uhai ulionao, huna budi kushukuru kwa sababu ya afya uliyonayo.
Sote tunajua afya ni msingi mkubwa sana wa mafanikio yako, hiyo ikiwa na maana
kama huna afya ujue kabisa na mafanikio huna.
Shukuru
kwa afya uliyonayo, kama kuna sehemu unaona unaumwa shukuru pia kwa sehemu
zingine za mwili ambazo huumwi. Kwa kushukuru huku uponyaji una uwezo wa
kusambaa na sehemu zingine za mwili kwa njia ambayo hata wewe huijui.
3. Shukuru kwa fursa zilizopo.
Tunaishi
katika dunia kwa sasa ambayo fursa zipo nyingi sana. Nakwambia hivi ni kwa
sababu tunaishi katika dunia ya habari. Kama upo hapo na huoni fursa basi ujue kuna shida
sehemu kwako au ‘umepigwa upofu’, macho yako hayaoni.
Shukuru
kwa sababu ya fursa zilizopo, ukishindwa kuchukua hatua fursa hii basi elewa ipo
fursa nyingine kule, kikubwa ni kutuliza sana akili yako na kutumia fursa hizo
za kimafanikio ziweze kukusaidia wewe na wengine wanaokuzunguka.
4. Shukuru kwa watu wanaokuzunguka.
Unalazimika
kuwa na shukrani kwa watu wanaokuzunguka, watu hawa wanaweza kuwa ni ndugu, rafiki
zako au jamaa zako lakini watu hawa wanamchango mkubwa wa kubadili maisha yako
na inabidi uwatumie vizuri kukusaidia katika hilo.
Kama
huna shukrani na watu wanaokuzunguka basi utakuwa unakosea na unajiweka katika
wakati mbaya wa kutokuendelea kufanikiwa. Haujaja duniani wewe kama
wewe,unaishi na kuzungukwa na watu, basi kuwa na shukrani na watu hao.
5. Shukuru kwa wakati mgumu.
Ni vyema
pia ukawa na shukrani hata katika kipindi kigumu cha maisha yako. Kipindi kigumu
cha maisha yako ni mwalimu mzuri wa kukufundisha na kukupa uzoefu wa wewe
kukusaidia wewe kuweza kufanikiwa.
Unaweza
ukawa hupendi sana nyakati hizi ngumu lakini kumbuka kipindi kigumu, hicho
ndicho kinachokukomaza wewe na kukusaidia kuweza kufanikiwa. Unatakiwa uelewe
nyakati ngumu hazipo kukuangusha bali kukusaidaia wewe kusimama kimafanikio.
Haya
ndio mambo ya msingi unatakiwa uanze kuwa na shukrani nayo ili kanuni ya
shukrani ifanye kazi kwako vizuri. Hata maandiko matakatifu yameandika juu ya
shukrani. Wale walioshukuru walipokea muujiza zaidi maishani mwao.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama
wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa
vifaranga wa kuku aina ya KUROILER,
SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao
kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na
wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Aug 23, 2018
Mambo Ambayo Umekuwa Ukidanganywa Sana Kuhusu Pesa Na Uwekezaji.
Kati
ya kitu ambacho kinatafutwa sana na wengi hapa duniani ni pesa. Pesa imekuwa
ikitafutwa usiku na mchana karibu na watu wote. Hali hii imekuwa iko hivyo kwa
sababu ya umuhimu wa pesa katika kutusaidia kufikia malengo yetu.
Lakini
pamoja na pesa kutafutwa hivyo, bado watu wengi wamekuwa wana hadithi nyingi za
uongo kuhusiana na pesa hata swala la uwekezaji kwa ujumla. Kila inapotajwa pesa au uwekezaji wakati
mwingine kumekuwa na uongo mwingi sana wa kupotosha.
Ni
lengo la makala haya kukuwezesha kutambua mambo ambayo umekuwa ukidanganywa juu
ya pesa na uwekezaji. Mambo hayo ni yepi? Fuatana nami katika makala haya
mwanzo hadi mwisho tuweze kujifunza kwa pamoja:-
1.
“Unahitaji pesa nyingi ili kuwekeza”.
Wengi
wetu bado tunaendelea na fikra mgando za kuamini kwamba ili uweze kuwekeza ni
lazima uwe na pesa nyingi. Kutokana na uongo huo, tumekuwa tukisubiri tupate
mitaji na pesa nyingi ili tuweze kuwekeza.
Kwa
taarifa yako huo ni uongo ambao umekuwa ukidanganywa. Kwa dunia ya sasa jinsi
ilivyo, kitu kikubwa unachohitaji ni wazo na taarifa sahihi za mafanikio ili
kuwekeza. Kama ni mtaji unahitajika sio lazima uwe mkubwa sana kama
unavyofikiri.
Kwa
hiyo kama umesimama na huwekezi kwa kisingizio cha kukosa mtaji,
unajichelewesha mwenyewe. Zinduka kwenye huo usingizi na anza kutumia kidogo
ulichonacho kufanya uwekezaji unao faa kwako. Naamini kipo kitu ulichonacho
hata kidogo cha kukusaidia, hauwezi kukosa vyote.
2.
“Uwekezaji ni hatari”
Jambo
la pili ambalo wengi wamekuwa wakidanganywa sana kuhusu pesa na uwekezaji kwa
ujumla ni kwamba, uwekezaji ni ‘risk’
kubwa sana. Nafikiri umeshawahi kusikia hadithi za namna hii sana kuwa
uwekezaji ni hatari.
Kutokana
na wengi kupokea hadithi za namna hii na kuzikubali kupelekea kutokufanya
uwekaji wowote ule. Unajua ni kwa nini? Kwa sababu wameshaambiwa uwekezaji ni
hatari na ni ‘ risk’ kubwa sana.
Huu
ni uongo ambao umekuwa ukidanganywa kwa muda mrefu. Na kwa bahati mbaya umekuwa
ukijisahau pia kwamba uwekezaji sio hatari kubwa sana kama unavyofikiri, ila
unachangamoto zake na ni njia mojawapo nzuri ya kukufikisha kwenye uhuru wa
kipesa.
3.
“Mshahara ndio kila kitu”
Acha
kuendelea kuugua na kuamini hadithi za kwamba wale wanaolipwa mshahara ndio
kila kitu. Kama hicho ndio kilio chako na unaamini tosha kabisa kwamba eti kwa
sababu wewe hukusoma na hulipwi mshahara basi maisha yako yameharibika.
Sikiliza
nikwambie rafiki, maisha ni mipango. Jiwekee taratibu zako za kutengeneza
kipato na jiamini zaidi, utafanikiwa. Kama unafanya kazi acha kuwadanganya
wengine kwamba ukiwa na mashahara ndio uhakika wa mafanikio.
Mafanikio
ya kweli hayaji kwa sababu ya mshahara unaolipwa. Mafanikio makubwa na ya
uhakika yanakuja kutokana na mipango yako imara uliyojiwekea na kuifata kila
siku.
Ukiangalia
na kufuatilia hizo ndizo hadithi ambazo una danganywa sana kuhusu pesa na
uwekezaji. Mengi yamekuwa yakisemwa sana kuhusu pesa na wekezaji kitu ambacho
sio kweli.
Endelea
kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Napenda
pia kuchukua fursa hii kukukaribisha kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja na kwa ukaribu zaidi. Kujiunga
tuma neno MAFANIKIO YANGU, kisha
ikifutia na namba yako kwenda 0713 04 80
35 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA
KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni
wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,
Aug 22, 2018
Jambo Hili Ni Muhimu Sana Katika Ukuaji Wa Biashara Unayoifanya.
Katika biashara yeyote ile unayoifanya ni lazima uweze kujifunza mbinu maridhawa zitakazokufanya uweze kukua katika biashara hiyo, hii ni kwa sababu moja kati ya changamoto kubwa ambayo inawakumba wafanyabiashara wengi kutofanya vizuri katika biashara wanazozifanya ni kwamba wanashindwa kujifunza mbinu mpya za kibiashara zitakazowasaidia wao kuweza kukua katika biashara husika.
Kama
na wewe ni miongoni mwa watu watu ambao wanakumbwa na sakata hilo basi nakuomba
usipepese macho mahala pengine bali
endelea kusoma makala haya kwani leo nimekusogezea makala muhimu sana kwako
itakayokufanya wewe uendeleee kufanya vizuri katika biashara ambayo unaifanya.
Tunafahamu
fika ulimwengu wa sasa ni ulimwengu wa biashara hivyo bila kujiongeza katika
biashara tunayoifanya tutashindwa kufikia malengo yetu ya kibiashara, hivyo ndugu
yangu kwenye biashara yeyote ile ili uweze kufanikiwa ni lazima ujifunze
kujitengenenezea soko lako maalamu.
Pia
ninapozungumzia alama nina maana ubobezi katika eneo fulani, yaani kwa
mfano mtu akisikiaa neon “kwa Beny
fashion” basi ajue moja kwa moja huyu anahusika na nini. Kama wewe ni muuzaji wa viatu vya dukani
basi hata jina lako likitamkwa mbele ya masikio ya watu basi watu hao wajue
fika wewe ni muuzaji wa viatu.
Kufanya
hivi ndiyo kitendo ambacho huitwa kutengeneza soko lako maalum. Pia kitendo
hiki kinapochukuliwa hatua stahiki ndicho kinawafanya wafanyabiashara wengi
waliofanikiwa waendelee kuyakumbatia mafanikio ya biashara zao.
Hivyo
mpenzi msomaji wetu kila wakati ni lazima uweze kujifunza kutengeneza
soko lako maalumu katika kila eneo unalolifanyia kazi, ni lazima wateja wako
watambue kuwa wewe ni mbobezi zaidi katika eneo gani? Kitendo hiki kitawafanya
wateja wako wasambaziane taarifa kwa haraka sana kwa kile unachokifanya.
Lakini
pia ni lazima ikumbukwe ya kwamba neno mafanikio sio uchawi kama wengi
wazaniavyo, bali ni matokeo ya vitu vidogovidogo ambavyo wengi huvipuuza. Hivyo
kuanzia sasa jifunze kuchua hatua kwa vitu vidogo vidogo ambayo unaona fika
havina mchango wowote wa kufanikiwa kwako, kwani vitu hivyo ndivyo vitavyokupa
mafanikio unayoyataraji.
Hivyo
kila wakati ni vyema ukajifunza kujitengenezea soko lako maalum ili uweze
kufanikiwa katika biashara.
Ndimi; Afisa Mipango: Benson Chonya
Aug 21, 2018
Huu Ndio Uongo Unaokuzuia Ushindwe Kuchukua Hatua.
Uwe unajua au hujui unatakiwa kujua kuna wakati upo uongo unaojijaza mwenyewe na kwa bahati mbaya sana uongo huo ndio unaokuzuia ushindwe kuchukua hatua za kuelekea kwenye mafanikio yako uliojipangia kuyafikia
Inawezekana
unajiuliza inawezekanaje na kivipi mtu ukajijaza mwenyewe uongo, ndio
inawezekana kabisa kwamba ukajidanganya mwenyewe na ukajipoteza kutokana na
mawazo ambayo unajisemea mwenyewe kila wakati.
Hapa
kupitia makala haya nataka nikuonyeshe uongo ambao unajiambia wewe mwenye na
kwa uongo huo unakuzui wewe kuweza kuchukua hatua za kufikia mafanikio yako. Je,
uongo huo ni upi unaojiambia?
1.”Siko
tayari kufanya jambo hili kwa sasa.”
Kuna
watu ambao wanajidanganya katika hili nakuona kile wanachotakiwa kukifanya kwa
sasa hawako tayari, nikiwa na maana watu hawa wanakuwa wanadai maandali mengine
zaidi bado yanahitajika ili waweze kuchukua hatua.
Matokeo
yake watu hawa huendelea kujiandaa wee na mwisho hushindwa kuchukua hatua
kabisa. Sasa huu ni uongo ambao wengi wanajidanganya, wakati unatakiwa kuchukua
hatua hata kama unajiona hauko tayari lakini wewe chukua hatua.
2. “Natafuta
wazo bora zaidi.”
Moja
ya kizuizi kinachowazuia watu wengi kushindwa angalau kuchukua hatua ya kwanza
tu kwa kile wanachokifanya ni kutokana na wao kuendelea kutafuta wazo bora
zaidi la kibiashara badala ya kulifanyia kazi lile walilonalo.
Utakuta
mtu ana mawazo mazuri tu ya kibiashara lakini unaona mtu huyo anaendelea
kutafuta wazo lingine bora na kuacha kutumia hata lile wazo walilonalo. Huo ni
uongo mwingine wa kuamini lipo wazo bora zaidi la kufanyia kazi.
3. “Nimeshachelewa
kwenye mradi huu.”
Kati
ya mojawapo ya wazo linalopoteza wengi ni kule kwa wengine kuamini mradi wanaoufanya
tayari wameshachelewa wakiwa na maana kwamba mradi huo tayari unafanywa na watu
wengi na jambo ambalo si sahihi.
Kuendelea
kuwa na mawazo haya ni kujidanganya tu, hakuna kitu ambacho umechelewa wewe kufanya
kwa sehemu yako na weka juhudi vya kutosha na kuhakikisha hadi unaweza
kufanikiwa vya kutosha.
Kwa kumaliza
makala haya, tambua huo ndio uongo ambao wengi wanajidanganya na unawafanya
washindwe kuchukua hatua za kufikia mafanikio yao.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama
wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa
vifaranga wa kuku aina ya KUROILER,
SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao
kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na
wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Aug 20, 2018
Yajue Mambo Ya Muhimu Katika kurahisisha Safari Ya mafanikio Yako.
Shughuli zote zifanywazo na mwanadamu katika sayari hii ya dunia, kila mmoja baada ya kufanya shughuri hilyo ni lazima mtu huyo anategemea kupata pesa, unashangaa wala usishangae huo ndio ukweli halisi. Na miongoni mwa siri ambayo hujawahi kuijua kuhusu mafanikio ni kwamba kwa kila kitu ambacho unakifanya ni lazima uwaze kwa kina kitu hicho kinakuing’iziaje pesa?
Hii ni kwa sababu wapo baadhi ya watu hufanya vitu
visivyo vya msingi hii ikiwa ni kigezo cha kuiburudisha nafsi basi jiandae kupata tabu sana. Nimesema
hivyo kwa sababu mambo yamebadilika sana hivyo habari za kuufariji moyo katika
jambo unalolifanya pasipo kuingiza kitu chochote katika maisha yako kunajipoteza
mwenyewe.
Lakini pia unatakiwa kufahamu ya kwamba Maisha yako ni
mjuimuko wa mambo madogo madogo ambayo wewe kama dereva unapaswa kuyafahamu
vyema mambo hayo ili kuhakikisha maisha yako yaweze kusonga mbele kimafanikio,
au kwa maneno mengine siku zote ni lazima ufahamu ya kwamba hatma ya maisha
yako unayo wewe na si mtu mwingine.
Pia ikumbukwe ya kwamba unavyoonekana hivi leo ni matokeo
ya kwako mwenyewe ndiye uliyeamua kuwa hivyo ulivyo, usiruhusu nafsi pamoja na
kinywa chako kumlam mtu mwingine kukusababishia ugumu wa maisha, kwani nimeshasema
hapo awali ya kwamba wewe ndio dereva halisi wa maisha yako na si vinginevyo.
Wewe ndiye mwenye maamuzi sahihi ya kufanya jambo fulani
au usifanye. Mara nyingi watu wengi sana wanashindwa kukidhi matakwa ya maisha
yao kwa sababu wameruhusu watu wengine ndio wawe waamuzi wa kile wanachokifanya
na kitendo hiki ndicho kinachowapeleea watu hawa wazidi kulalama maisha ni
magumu, na kitendo hiki ndicho kinachotupoteza wengi.
Vile vile watu wengi wanashindwa kufanikiwa kwa sababu
wao pia wameshindwa kufanikiwa katika maisha yao hii ni kwa sababu wameshindwa
pia hata kuchagua hata marafiki sahihi wanaopaswa kuongozana nao katika maisha
yao.
Ni ninii kinatakiwa kufanyika ili kuishi maisha yenye
tija katika safari hii ya dunia katika kuyasaka mafanikio?
Mosi, unachopaswa
kukizingatia katika dunia hii ili uweze kuishi maisha ya mafanikio ni
kuhakikisha unakuwa ni mtu mwenye maamuzi yako sahihi ambayo yatakufanya uweze kutimiza
kusudio lako hapa duniani ili mradi usivunje sheria za nchi na sheria za
Mwenyezi Mungu.
Jambo la pili, kwa kila jambo unalolifanya ni vyema ukawa
ni mtu wa kujiuliza hivi jambo hili lina manufaa yeyote yale kwangu? Na je
napateje pesa kupitia jambo hili?
Jambo la tatu na la mwisho, ni vyema ukajifunza kuchagua
marafiki sahihi wataokusaidia kupiga hatua za kimafanikio za kule ambako unataka
kuelekea na si vinginevyo.
Kwa leo sina mengi, naomba niishie hapo nikutakie siku
njema na mafanikio mema.
Ndimi Afisa Mipango; Benson Chonya
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)