Aug 22, 2018
Jambo Hili Ni Muhimu Sana Katika Ukuaji Wa Biashara Unayoifanya.
Katika biashara yeyote ile unayoifanya ni lazima uweze kujifunza mbinu maridhawa zitakazokufanya uweze kukua katika biashara hiyo, hii ni kwa sababu moja kati ya changamoto kubwa ambayo inawakumba wafanyabiashara wengi kutofanya vizuri katika biashara wanazozifanya ni kwamba wanashindwa kujifunza mbinu mpya za kibiashara zitakazowasaidia wao kuweza kukua katika biashara husika.
Kama
na wewe ni miongoni mwa watu watu ambao wanakumbwa na sakata hilo basi nakuomba
usipepese macho mahala pengine bali
endelea kusoma makala haya kwani leo nimekusogezea makala muhimu sana kwako
itakayokufanya wewe uendeleee kufanya vizuri katika biashara ambayo unaifanya.
Tunafahamu
fika ulimwengu wa sasa ni ulimwengu wa biashara hivyo bila kujiongeza katika
biashara tunayoifanya tutashindwa kufikia malengo yetu ya kibiashara, hivyo ndugu
yangu kwenye biashara yeyote ile ili uweze kufanikiwa ni lazima ujifunze
kujitengenenezea soko lako maalamu.
Pia
ninapozungumzia alama nina maana ubobezi katika eneo fulani, yaani kwa
mfano mtu akisikiaa neon “kwa Beny
fashion” basi ajue moja kwa moja huyu anahusika na nini. Kama wewe ni muuzaji wa viatu vya dukani
basi hata jina lako likitamkwa mbele ya masikio ya watu basi watu hao wajue
fika wewe ni muuzaji wa viatu.
Kufanya
hivi ndiyo kitendo ambacho huitwa kutengeneza soko lako maalum. Pia kitendo
hiki kinapochukuliwa hatua stahiki ndicho kinawafanya wafanyabiashara wengi
waliofanikiwa waendelee kuyakumbatia mafanikio ya biashara zao.
Hivyo
mpenzi msomaji wetu kila wakati ni lazima uweze kujifunza kutengeneza
soko lako maalumu katika kila eneo unalolifanyia kazi, ni lazima wateja wako
watambue kuwa wewe ni mbobezi zaidi katika eneo gani? Kitendo hiki kitawafanya
wateja wako wasambaziane taarifa kwa haraka sana kwa kile unachokifanya.
Lakini
pia ni lazima ikumbukwe ya kwamba neno mafanikio sio uchawi kama wengi
wazaniavyo, bali ni matokeo ya vitu vidogovidogo ambavyo wengi huvipuuza. Hivyo
kuanzia sasa jifunze kuchua hatua kwa vitu vidogo vidogo ambayo unaona fika
havina mchango wowote wa kufanikiwa kwako, kwani vitu hivyo ndivyo vitavyokupa
mafanikio unayoyataraji.
Hivyo
kila wakati ni vyema ukajifunza kujitengenezea soko lako maalum ili uweze
kufanikiwa katika biashara.
Ndimi; Afisa Mipango: Benson Chonya
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.