Aug 24, 2018
Hii Ndiyo Kanuni Ya Mafanikio Iliyosahaulika Na Wengi.
Mafanikio hayatengenezwi na kanuni moja tu, bali ni mjumuiko wa kanuni za kimafanikio tofauti tofauti na hizi ndizo ziletazo mafanikio. Zipo kanuni za wazi kabisa za kimafanikio ambazo zinafahamika na wengi na zipo ambazo hazifahamiki.
Kwa mfano,
kufanya kazi kwa bidii, kuwa na nidhamu, kutengeneza nguvu ya uzingativu,
naweza kusema ni moja ya kanuni za mafanikio au misingi ya mafanikio ambayo
inaeleweka na wengi kwamba ukiifata lazima ufanikiwe.
Hata
hivyo inabidi ieleweke hivi, zipo kanuni nyingi za kimafanikio ambazo unatakiwa
uzifanyie kazi sana ili ufanikiwe, na kwa bahati mbaya zipo ambazo huzijui au
umezisahau kwa kutokujua lakini zipo na zinafanya kazi kwa matokeo makubwa.
Na mojawapo
ya kanuni rahisi ya mafanikio ambayo wengi hawaijui au wameisahau, ni
kanuni ya kuwa na shukrani. Inaeleweka kwamba kwa mtu yeyote ambaye ana
shukrani, na huku akawa ni mtu wa kuchukua hatua kufanikiwa ni lazima kwake.
Sasa
linakuja tatizo la watu wengi ni wabinafsi na hawana shukrani, kama unafikiri
natania nianze na wewe, je, wewe ni mtu wa shukrani, je, wewe ni mtu wa
kukumbuka kule ulikotoka na kushukuru hapo ulipo na kwa maisha uliyonayo.
Mara
nyingi utakuta watu wengi hawana shukrani sana, si watu wa kukumbuka watu wale waliowasaidia
na wapi, hata kama ni kwa kidogo na matokeo yake wanajikuta ni watu ambao
wanaiweka kanuni hii pembeni na mwisho wake hushindwa kufanikiwa sana.
Kama
nia yako ni mafanikio makubwa kweli, pia unatakiwa kuchukua shukrani kama mojawapo
ya kanuni ya kimafanikio. Kila wakati unapochukua hatua za kiutendaji, lakini hakikisha shukrani iwe karibu na kinywa chako
kwa chochote kitakachotokea.
Kuna
watu wana midomo kama ya ‘laana’
wanapochukua hatua, kwa mfano kufanya biashara ya aina fulani halafu wakapata
hasara, midomo yao inakuwa inaongea mengi sana na kulalamika, sasa hii sio
nzuri na haikusadii, shukuru kwa chochote.
Unaweza
ukawa upo kwenye wakati mgumu shukuru kuna kitu cha kujifunza, unaweza ukawa
umepata hasara kweli shukuru, hii ni kanuni ya kimafanikio na ambayo pia ni
kanuni ya kiroho, pasipo kushukuru mambo yako hayawezi kwenda sawa saana.
Inawezekana
sasa unajiuliza nashukuru kwa mambo yapi, hilo lisikupe tabu. Yapo mengi sana ambayo
unaweza ukaanza kuwa na shukrani nayo lakini kwa kuanza tu, unaweza ukaanza na
kushukuru kwa mambo haya na yatakusaidia sana kufanikiwa.
1. Shukuru kwa uhai ulionao.
Kwa
sababu ile tu unaishi, kwa sababu ile tu umepewa uwezo wa kuishi unatakiwa
kushukuru sana kwa hilo kwanza. Amka asubuhi na sali kwa kwa sababu umepewa
uwezo wa kuishi na muumba wako na hicho ni kitu kizuri sana.
Kitendo
cha kushukuru kwa uhai ulionao kitakupa nguvu hata ya kutenda mambo mengine
makubwa maishani mwako ambayo moja kwa moja yatakusaidia kuweza wewe kufanikiwa
kwenye maisha yako moja kwa moja.
2. Shukuru kwa afya yako.
Tofauti
na kushukuru juu ya uhai ulionao, huna budi kushukuru kwa sababu ya afya uliyonayo.
Sote tunajua afya ni msingi mkubwa sana wa mafanikio yako, hiyo ikiwa na maana
kama huna afya ujue kabisa na mafanikio huna.
Shukuru
kwa afya uliyonayo, kama kuna sehemu unaona unaumwa shukuru pia kwa sehemu
zingine za mwili ambazo huumwi. Kwa kushukuru huku uponyaji una uwezo wa
kusambaa na sehemu zingine za mwili kwa njia ambayo hata wewe huijui.
3. Shukuru kwa fursa zilizopo.
Tunaishi
katika dunia kwa sasa ambayo fursa zipo nyingi sana. Nakwambia hivi ni kwa
sababu tunaishi katika dunia ya habari. Kama upo hapo na huoni fursa basi ujue kuna shida
sehemu kwako au ‘umepigwa upofu’, macho yako hayaoni.
Shukuru
kwa sababu ya fursa zilizopo, ukishindwa kuchukua hatua fursa hii basi elewa ipo
fursa nyingine kule, kikubwa ni kutuliza sana akili yako na kutumia fursa hizo
za kimafanikio ziweze kukusaidia wewe na wengine wanaokuzunguka.
4. Shukuru kwa watu wanaokuzunguka.
Unalazimika
kuwa na shukrani kwa watu wanaokuzunguka, watu hawa wanaweza kuwa ni ndugu, rafiki
zako au jamaa zako lakini watu hawa wanamchango mkubwa wa kubadili maisha yako
na inabidi uwatumie vizuri kukusaidia katika hilo.
Kama
huna shukrani na watu wanaokuzunguka basi utakuwa unakosea na unajiweka katika
wakati mbaya wa kutokuendelea kufanikiwa. Haujaja duniani wewe kama
wewe,unaishi na kuzungukwa na watu, basi kuwa na shukrani na watu hao.
5. Shukuru kwa wakati mgumu.
Ni vyema
pia ukawa na shukrani hata katika kipindi kigumu cha maisha yako. Kipindi kigumu
cha maisha yako ni mwalimu mzuri wa kukufundisha na kukupa uzoefu wa wewe
kukusaidia wewe kuweza kufanikiwa.
Unaweza
ukawa hupendi sana nyakati hizi ngumu lakini kumbuka kipindi kigumu, hicho
ndicho kinachokukomaza wewe na kukusaidia kuweza kufanikiwa. Unatakiwa uelewe
nyakati ngumu hazipo kukuangusha bali kukusaidaia wewe kusimama kimafanikio.
Haya
ndio mambo ya msingi unatakiwa uanze kuwa na shukrani nayo ili kanuni ya
shukrani ifanye kazi kwako vizuri. Hata maandiko matakatifu yameandika juu ya
shukrani. Wale walioshukuru walipokea muujiza zaidi maishani mwao.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama
wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa
vifaranga wa kuku aina ya KUROILER,
SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao
kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na
wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.