Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Wednesday, March 8, 2017

TAFITI: Chanzo Cha Kufa Kwa Mahusiano Mengi Ya Kimapenzi.

No comments :
Pindi wapendao wanapoanza mahusiano ya kimapenzi huwa zinajitokeza kila aina za starehe ambazo zinafanya mtu amini anapendwa.  Na aina hizi za starehe wataalamu wa mahusiano wanatuambia ya kwamba hizi ni " fujo za mapenzi".
Huitwa fujo za mapenzi kwa sababu pindi mahusiano hayo yanapoanza huanza kwa mbwembwe nyingi ila kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo mahusiano yanavyozidi kushuka thamani.
Na kutoka na kushuka kwa thamani ya upendo baina ya wapendao, tumekuwa mashuhuda wazuri katika kuona mambo ya mahusiano yanavyozidi kupoteza nuru hatimaye kuzizima kabisa kama taa ambayo imekosa mafuta.
Na baina ya chanzo cha kutokea kwa hali hiyo ya kufa kwa mahusiano hayo ya kimapenzi ni kutokuwepo kwa matarajio sahihi.

Mahusiano mengi yanakufa mapema kwa sababu ya kutokuwapo kwa matarajio sahihi. Kwa mfano mwanzoni mwa mahusiano watu huwa na matarajio chana juu ya huyo mwezi wake. 
Kwani upendo unapoanza  huwa na ahadi nyingi za uwongo. Ahadi hizi za uongo huenda sambamba na zawadi nyingi ambazo huifanya uwongo huo kuwa ni ukweli.
Kwa mfano watu wengi wamekuwa wakiwadandanya wapenzi wao katika kipindi cha kumtaka mpenzi huyo,  kwa kumwambia yeye ni mfanyakazi wa ‘bank,’ anamiliki kampuni yake na bla bla nyingi kama hizo.
Lakini uongo unapokuwa ukweli baada ya muda fulani ndipo unapofanya penzi hilo lizizime kama taa.
Kabla ya kuweka nukta siku ya leo naomba nikwambie ya kwamba japo tunasema ya kwamba mapenzi ni "uwongo". Hivyo mimi nakusihi ya kwamba achana na dhana hiyo kama kweli unataka kumpata mpenzi wa kweli.
Hivyo jitahidi kuwa mkweli hasa katika kipindi cha kumtafuta mpenzi huyo. Kwani  "ukweli humuweka mtu huru".
Ukifanya hivyo itakusaidia sana katika kuanzisha mahusiano yaliyo bora,  kwani utakuwa umemweleza kila kitu huyo ambaye unampenda hususani habari zote zinazokuhusu wewe.
Kuendelea kumdanganya ni sawa na bure kwani katika dunia hii huwezi kuficha kitu chochote kwani ipo siku ukweli utajulikana.  Ukificha ukweli ipo siku itajulikana.
Nakutakia siku njema yenye baraka na mafanikio tele.  Endelea kutembelea mtandao wetu wa dira ya mafanikio kila mara, ila kupata maarifa sahihi.
Ndimi Afisa Mipango: Benson Chonya,

No comments :

Post a Comment